Sunday, January 4, 2015

Yanga yashinda tena kwenye kombe la Mapinduzi.

yangaaa
Washindi wa pili wa ligi kuu soka Tanzania bara kwa msimu uliopita Dar-es-salaam Young Africans Yanga jioni hii wamepata ushindi wao wa pili mfululizo katika michuano ya kombe la mapinduzi inayoendelea huko visiwani Zanzibar.
Huku wakiwa kwenye kiwango chao bora Yanga walifanikiwa kushinda mchezo wa pili kwa idadi ya mabao manne dhidi ya timu ya Polisi Fc na kufikisha idadi ya mabao nane katika michezo miwili matokeo ambayo yameifanya timu hiyo kufuzu hatua ya robo fainali .
Mliberia Kper Sherman  alifunga bao la pili kwneye mchezo huu na bao lake la pili kwenye kombe la Mapinduzi.
Mliberia Kper Sherman alifunga bao la pili kwneye mchezo huu na bao lake la pili kwenye kombe la Mapinduzi.
Yanga ilianza mchezo huo kwa kasi na iliwachukua dakika karibu 25 kabla ya kuanzidka bao lao la kwanza mfungaji akiwa kiungo wa Kibrazil Andriy Coutinho ambaye alifunga bao hilo kwa shuti kali baada ya mpira kurushwa toka pembeni ya uwanja na kumzidi uwezo beki na nahodha wa Polisi .
Yanga ilifunga bao la pili kwneye mchezo huo kupitia kwa mshambuliaji raia wa Liberia Kper Sherman ambaye alifunga kwa shuti la chini baada ya kupewa pasi ya kichwa na Amisi Tambwe ambaye aliunganisha mpira mrefu uliopigwa na Simon Msuva .
Bao la tatu kwenye mchezo huo kwa Yanga lilifungwa baada ya Andriy Coutinho kupiga mpira wa adhabu ndogo ukitokea pembeni ya uwanja ambapo alipiga mpira huo kwa unfundi mkubwa ukimzidi ujanja kipa wa Polisi .
Kiungo Mbrazil Andriy Coutinho aliifungia Yanga mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Polisi.
Kiungo Mbrazil Andriy Coutinho aliifungia Yanga mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Polisi.
Bao la nne kwenye mchezo huo lilifungwa na winga Simon Msuva aliyemaliza mpira wa krosi toka pembeni mwa uwanja .
Bao la Msuva lilimfanya aweze kufikisha idadi ya mabao manne inayomfanya we mfungaji anayeongoza katika mashindano haya .
Katika mchezo uliopigwa hapo awali timu toka Uganda KCCA iliwafunga Mtende Fc ya Zanzibar kwa matokeo ya 3-0 .

Tags :

AJALI JIJINI DAR ES SALAAM

Wasamalia wema wakifanya utaratibu wa kumuokoa Dereva wa Gari aina ya Isuzu Trooper iliyopiga mweleka katika makutano ya Shule ya Msingi Oysterbay,mara baada ya kugongana na gari nyingine aina ya Toyota Vitz iliyokuwa ikitokea upande wa Coco Beach jijini Dar leo mchana na kupekea dereva wa Gari hii (alikuwa ni Mama mtu mzima ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja) kuumia sehemu ya kiuno na mkono.Gari hii ilikuwa linatokea upande wa St. Peter's kuelekea Morogoro Store naVitz ilikuwa ikitokea upande wa ufukweni na kuvuka ghafla barabara hiyo.
Mashuhuda wakiwa wameizunguka gari hiyo mara baada ya kufanikiwa kumtoa Mama aliekuwa akiendesha Gari hilo.
Hivi ndivyo ilivyo hii Toyota Vitz baada ya kuhongana na Isuzu Trooper iliyopinduka.
Huyu ndio Mama aliekuwa akiendesha Gari iliyopinduka.

RIDHIWANI KIKWETE KUHARAKISHA MAENDELEO CHALINZE

    on linkedin
Ridhiwani akisisitiza jambo alipokuwa akihutubia katika kijiji hicho ambapo aliwataka kuacha tabia ya kukata miti ovyo kwa ajili ya mkaa ama sivyo vijiji vitageuka jangwa.
Mkazi wa Kijiji cha Kwaluhongo, Dustan Sangi akiuliza swali kwa Mbunge wake Ridhiwani Kikwete wakati wa mkutano uliofanyika kijijini hapo.
Ridhiwani akizungumza jambo na Khamis Ibrahim baada ya mkutano kumalizika katika Kijiji cha Kwaluhongo, wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kata ya Mbwewe, Chalinzi, wilayani Bagamoyo jana.
Ridhiwani akiteta jambo na Mzee Suleiman Kadagala baada ya kumalizika kwa mkutano huo.

JENGO LATEKETEA KWA MOTO KARIAKOO

Jengo la Ghorofa 8 likiwa linateketea katika ghorofa ya 4,Jengo hilo linamilikiwa na mfanyabiashara anayejulikana kwa jina la Haji Kube ,vitu mbalimbali zikiwemo Frem za Picha ,maua, vimeteketea kwa moto. ambapo mmiliki wa ofisi hiyo yuko nje kwa safari
Hapo wananchi wakikimbizana baada ya nguzo ya umeme kutowa mlipuko katika Barabara ya Huru na Kongo Dar es Salaam kama ilivyonaswa na mwandishi wa Jambo Leo alipokuwa akienda katika Jengo la Ghorofa 8 lililopo jirani na Msikiti wa Kiblateni .
Hapo wananchi wakikimbizana na kuondowa bidhaa zao baada ya nguzo ya umeme
kutoa mlipuko katika Barabara ya Uhuru na Kongo Dar es Salaam.

Manchester City yahusishwa na usajili wa nyota huyu.

man city
Siku chache baada ya kuhusishwa na mpango wa kumsajili mshambuliaji raia wa Ivory Coast Wilfred Bony , mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England Manchester City wametajwa kuongoza mbio za kumsajili kiungo wa Everton Ross Barkley na klabu hiyo imeandaa oa ambayo ina uhakika kuwa haitakumbana na kikwazo chocote toka Everton na kwa mchezaji mwenyewe .
Manchester City wanadaiwa kuwa wameandaaa ofa ya paundi milioni 45 kwa ajili ya mchezaji huyo huku wakiwa tayari kumvutia kwa dau nono la mshahara wa paundi 130,000 kwa wiki kiasi ambacho kitakuwa kinauzidi mshahara wake wa sasa kwa mara mbili .
Manchester City imemuandalia Ross Barkley mshahara wa paundi 130,000 kwa wiki .
Manchester City imemuandalia Ross Barkley mshahara wa paundi 130,000 kwa wiki .
Klabu ya Everton kwa upande wake iko tayari kumruhusu Barkley kuondoka ili mradi ihakikishiwe ada ya uhamisho ya paundi milioni 45 ambazo kwa upande wake itazitumia kuboresha kikosi cha kocha Roberto Martinez .
Hata hivyo Manchester City watakumbana na vita kali katika mbio za kumsajili Barkley kwani klabu kadhaa ikiwemo Liverpool ambayo imekuwa ikimtolea macho.
Nyota huyu wa timu ya taifa ya England pia anatakiwa na Liverpool.
Nyota huyu wa timu ya taifa ya England pia anatakiwa na Liverpool.
Hata hivyo itakuwa vigumu kwa Barkley kujiunga na Liverpool kutokana na historia ya upinzani wa jadi uliopo baina ya Liverpool na Everton upinzani ambao mara nyingi hufanya iwe vigumu kwa timu hizo mbili kubadilishana  wachezaji .
Tags :

Msiba mwingine mkubwa Kenya, siku chache baada ya mwaka 2015.

PrezzoFidel Odinga katikati akiwa na marafiki zake
Prezzo akiwa na Fidel Odinga katikati na marafiki wengine
Simanzi kubwa imeikumba familia ya waziri mkuu wa zamani wa Kenya Raila Amolo Odinga baada ya kutoka kwa taarifa ya kifo cha mtoto mkubwa wa mwanasiasa huyo mashuhuri nchini Kenya asubuhi ya leo .
Mtoto huyo anayefahamika kwa jina la Fidel Odinga alikutwa akiwa amefariki dunia kitandani kwake asubuhi ya leo (jumapili) baada ya kurudi nyumbani kwake alfajiri akiwa anatoka kukutana na rafiki zake .
Mara ya mwisho Fidel aliripotiwa kukutana na baba yake usiku wa jumamosi kabla ya kuagana na kwenda kukutana na rafiki zake katika sehemu ambayo haijawekwa wazi na baada ya hapo alirudi nyumbani kupumzika hadi mauti yalipomkumba .
Mwili wa Fidel Odinga ulikutwa kitandani kwake baada ya kurudi nyumbani alfajiri akiwa anatoka kukutana na rafiki zake .
Mwili wa Fidel Odinga ulikutwa kitandani kwake baada ya kurudi nyumbani alfajiri akiwa anatoka kukutana na rafiki zake .
Hadi mauti yanamkumba Fidel Odinga alikuwa na umri wa miaka 42 na Polisi nchini Kenya wameanza uchunguzi wa kifo cha mtoto huyo wa mwanasiasa maarufu nchini Kenya huku bado kukiwa hakuna taarifa zozote kuhusiana na chanzo cha kifo chake .
Fidel ameacha mke mmoja na mtoto mmoja mwenye umri wa miaka miwili ambaye alizaa na mke wake Getachew Bekele ambaye ni raia wa Eritrea .
Fidel Odinga siku alipofunga ndoa na mkewe Getachew Bekele.
Fidel Odinga siku alipofunga ndoa na mkewe Getachew Bekele.
Saa chache baada ya habari za kifo cha Fidel makundi tofauti ya watu yalianza kufanya maandamano na vurugu maeneo ya Ngong nje kidogo ya Jiji la Nairobi wakipiga kelele za ‘Nani amemuua Fidel’ wakimaanisha kuwa kifo chake kimesababishwa na mtu huku wakishindwa kutaja sababu au chanzo kamili .

kijana mwananfunzi aliyemtukana rais uhuru kenyata mtandaoni atupwa jela


Mwanafunzi mmoja nchini Kenya amepewa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kumtukana rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika mtandao.
Alan Wadiu Okengo mwenye umri wa miaka 25 pia atalipa faini ya dola 2,200 la sivyo ahudumie kifungo chengine cha mwaka mmoja.

Alikuwa ameshtakiwa kwa kutoa matamshi ya chuki baada ya kusema kuwa watu wa kabila la rais la kikuyu wanafaa kuwekewa mipaka katika maeneo fulani.
Mwanablogu mashuhuri nchini humo pia alishtakiwa baada ya kumwita rais Uhuru Kenyatta 'rais ambaye hajakomaa'.

Wabongo Mpo? 

Umesoma makubwa yaliyoandikwa na Magazeti ya Tanzania leo Jan 4? Yako hapa


.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

RAIS KIKWETE ATEUA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI MPYA

Bwana George Mcheche Masaju, Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya.
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT'S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Rais ateua Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteuaBwana George Mcheche Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Uteuzi wa Bwana Masaju ulianza jana, Ijumaa, Januari 2, 2015 na ataapishwa keshokutwa, Jumatatu, Januari 5, 2015, Ikulu, Dar Es Salaam.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Masaju alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bwana Masaju pia amepata kuwa Mshauri wa Sheria wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
3 Januari, 2015

Hii ndiyo style mpya ya Nywele aliyoamua kuja nayo Joti 2015.

Asilimia kubwa ya mastar wengi wa duniani huwa wanapenda kutengeneza kitu ambacho kitakua tofauti na wengine ili kumtengenezea utambulisho wake popote anapokuwepo.
Tumeona style kadhaa za mavazi ambayo yanapovaliwa na mastar huwa yanachukua chart kwa kuvaliwa pia na watu wa kawaida ambao huwa wanavutiwa nayo.
Kingine ni style ya nywele ambazo mastar wamekuja nazo ikiwemo kiduku ambapo kwa sasa mastar wengi wananyoa hivyo,kuna wengine wanaachia nywele zinakua nyingi style hii wengi wao huita ‘Mwembe’ kwa wingi wa nywele kichwani.
Star kutoka kundi la Original Komed Joti yeye mwaka 2015 kaamua kuja na style hii ambayo hajasema inaitwaje ambapo kwenye ukurasa wake wa Instagram alipost picha akiwa ananyoa na alipomaliza.
Katika post yake ya kwanza aliandika>>’Kwaheri 2014′ hii alionekana akinyoa na katika post nyingine aliandika>>’Now karibu 2015,karibu babaaa…..my new style’.