karibuni sana wasomaji wa blog hii usikubali kupitwa na habari tanzania na hata nje ya tanzania.
Wednesday, February 11, 2015
Tuesday, February 10, 2015
NSSF YAANZA MCHAKATO WA KUWASAKA WENYE VIPAJI VYA MPIRA WA MIGUU
Itakumbukwa kuwa mnamo tarehe 26/01/2015 Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) lilisaini mkataba maalum na timu ya Real Madrid ya Nchini Hispania ya kuanzisha na kuendesha kituo cha michezo (NSSF- REAL MADRID Sports Academy) kwa lengo la kuibua, kuendeleza na kukuza vipaji kwa mpira wa miguu.
Shirika la NSSF litajenga kituo hicho katika eneo la Mwasonga Kigamboni nje kidogo ya mji wa Dar es Salaam na wataalamu kutoka timu ya Real Madrid watatoa mafunzo kwa vijana wa umri wa miaka13 hadi 19 kwa madhumuni ya kukuza mpira wa miguu nchini, kupata wachezaji bora wanaouzika nje na ndani ya nchi pamoja na kulipatia mapato shirika na nchi kwa ujumla .
Akizungumza na Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya Habari Nchini, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Dr. Ramadhani K. Dau alisema mradi huo ukiwa kama sehemu ya uwekezaji wa NSSF ulianza maramoja baada ya kusaini mkataba.
NSSF imeanza utaratibu wa kuwabaini vijana walengwa ambapo kwa kuanzia utafutaji wa vipaji vya mpira wa miguu utaanzia mkoa wa Dar es Salaam kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 14. Utafutaji wa vipaji utafanyika kiwilaya kwa Wilaya za mkoa wa dar es salaam na utakuwa unafanyika katika viwanja vya Karume. Zoezi hilo litakuwa linafanyika kati ya saa 1 asubuhi hadi saa 9 alasiri kwa tarehe zilizoainishwa.
Uandikishaji wa washiriki utakuwa unafanyika siku za mwisho wa wiki ili kutoathiri wanafunzi watakaopenda kushiriki na utaanza rasmi tarehe 14 na 15,na tarehe 22 na 23 Februari 2015, na kufuatiwa na michezo ya majaribio tarehe 28 Februari,na Tarehe 1 Machi 2015 kwa wilaya zote za mkoa wa Dar es salaam ambapo kituo kitakuwa viwanja vya Karume kuanzia saa moja asubuhi hadi saa 9 alasiri.
Zoezi la Uandikishaji halitahusisha gharama zozote kwa washiriki, na uandikishaji wa washiriki utafanyika kwa kujaza fomu maalum na kupewa namba ya ushiriki na kila mshiriki atapata fursa ya kucheza katika awamu mbili za dakika 30. Kwa kuanzia washiriki watatakiwa kuja na vifaa vyao vya michezo.
Zoezi la awali litafanywa na wataalam wa ndani ya nchi ambapo Vijana 500 kati ya wote watakaofanyiwa majaribio wataingia katika awamu ya pili ya majaribio na watadahiliwa na wataalamu kutoka Klabu ya Real Madrid na hatimaye kupatikana vijana 30 amabo ndio wataingia katika shule maalum ya mafunzo kwa awamu ya kwanza.
Wakati wa uandikishwaji washiriki watatakiwa kuja na wazazi/walezi wao wakiwa na vitambulisho vyao,na kijana husika awe na Cheti halisi cha kuzaliwa na kopi yake pamoja na picha mbili za pasport rangi ya blue.Muda wa uandikishaji na majaribio unaweza kuongezwa kulinagana na mahitaji.
Shirika la NSSF linatoa wito kwa vijana kujitokeza kwani ni fursa kwao ya kuweza kujiendeleza kimichezo na kujiajiri katika tasnia hiyo
UTAFITI WAWABEBA VIJANA URAIS 2015 MWIGULU
SHIRIKA la Utafiti wa Maendeleo ya Elimu (TEDRO), limesema katika utafiti walioufanya kuhusu ushiriki wa vijana katika siasa na matarajio kuelekea uchaguzi mkuu 2015, umeonesha kwamba endapo mgombea urais kijana atapendekezwa atakubalika kwa asilimia 82.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa shirika hilo, Jacob Kateri alisema katika wananchi hao waliohojiwa pia asilimia 11 walisema vijana hawatakubalika na asilimia saba walisema hawajui.
Alisema utafiti huo umeandaliwa na kufanyika Tanzania Bara na maeneo yaliyohusishwa ni kanda za kijiografia ili kuwezesha uhusishwaji mpana wa Watanzania na katika kila wilaya wamehojiwa wananchi wa vijiji vitatu kwa kuzingatia siasa za eneo husika.
Aidha alisema utafiti huo umeonesha sababu mbalimbali zinazoweza kuwa kichocheo cha vijana kuingia katika siasa ambapo zilizochukua uzito ni uzalendo kwa asilimia 67 ambapo wananchi walisema vijana wengi wameingia katika siasa kwa sababu ya uzalendo.
“Sababu nyingine ni kimbilio baada ya kukosa ajira kwa asilimia 57, uwezo mdogo wa watangulizi wao katika nafasi husika kwa asilimia 60, mafanikio ya wanasiasa vijana walio mahiri asilimia 72, vyama vya siasa kuwapa nafasi vijana katika vyama vyao kwa asilimia 59 na kukubalika kwa vijana kwa asilimia 63,” alisema.
Aidha alisema wanasiasa vijana waliopendekezwa kupitia chama tawala aliyeoonekana kuongoza kwa kukubalika ni Mwigulu Nchemba kwa asilimia 38, Dk Emmanuel Nchimbi kwa asilimia 26, January Makamba kwa asilimia 24, William Ngeleja kwa asilimia 11 na Lazaro Nyalandu kwa asilimia 10.
Wengine ni Hamisi Kigwangala kwa asilimia saba, Deo Filikunjombe kwa asilimia tano, Esther Bulaya kwa asilimia 2 na waliosema hakuna anayefaa walikuwa asilimia 9 na asilimia 13 walipendekeza wengine wasio vijana.
Utafiti huo pia unaonesha kwamba kijana anayepewa nafasi kubwa endapo atasimamishwa kupitia upinzani anayeongoza ni Zitto Kabwe kwa asilimia 18, James Mbatia kwa asilimia 16, Tundu Lissu kwa asilimia 14, Halima Mdee kwa asilimia nne na David Kafulila kwa asilimia sita.
Wengine ni Julius Mtatiro kwa asilimia nne, John Mnyika kwa asilimia saba, Joshua Nassari kwa asilimia mbili, Moses Machali kwa asilimia nne na asilimia 11 ya wananchi walisema hawajui na asilimia 16 walisema hawaoni anayefaa.
Hata hivyo, utafiti huo ulionesha kwamba endapo wakishindanishwa vijana wote bila kujali itikadi zao anayeongoza kwa kukubalika ni Mwigulu Nchemba kwa asilimia 27, Zitto Kabwe kwa asilimia 19, January Makamba kwa asilimia 14, James Mbatia kwa asilimia 11 na Emmanuel Nchimbi kwa asilimia nane.
Wengine ni Lazaro Nyalandu kwa asilimia saba, Tundu Lissu kwa asilimia tano, Hamis Kigwangala kwa asilimia nne, wengine waliotajwa wasio vijana ni asilimia nne na wasiofaa walikuwa ni asilimia mbili.
Mapema Mkurugenzi wa Mafunzo wa Utafiti wa TEDRO, Jackson Coy alisema utafiti huo wameufanya bila shinikizo kutoka kwa mtu yeyote na waliufanya kuhusu siasa kutokana na kwamba mwaka huu utafanyika uchaguzi mkuu.
Alisema lengo la utafiti huo limechambua ushiriki wa vijana katika siasa kama wagombea, mchango wa wanasiasa vijana katika kufuatia misingi ya utawala bora na uwajibikaji, utekelezaji wa ahadi za wagombea kwa wapiga kura na matarajio ya wananchi kwa vijana katika kuelekea uchaguzi mkuu.
“Utafiti tunaoendesha ni mwendelezo wa uchambuzi wa changamoto za elimu, ndani ya dira ya TEDRO na programu ya mchango wa elimu katika kufungua fursa za ajira, siasa ikiwa ni mojawapo ya fursa zenye kimbilio la vijana,” alisema.
Hadi sasa TEDRO inaendesha utafiti wa Mitandao ya Kijamii inavyoathiri wanafunzi wa sekondari na kutazama njia rafiki katika kutumia mitandao hiyo kama njia ya kujifunzia na kuendeleza sekta nzima ya elimu.
Utafiti huu uliotarajiwa kuhusisha wilaya 24 Tanzania Bara, umeendeshwa katika wilaya 18, kila wilaya ikiwa imewakilishwa na wahojiwa 45 waliochaguliwa 15 kutoka kila kijiji; hivyo utafiti huu kuhusisha vijiji 54 kwa ujumla.
Wilaya ambapo utafiti umefanyika ni Njombe Mjini, Ludewa, Mbeya Mjini, Kilwa, Lindi Mjini, Mtwara Mjini, Morogoro Mjini, Kisarawe, Kinondoni, Tanga Mjini, Vunjo, Arumeru, Singida, Kasulu, Kigoma Mjini, Bukoba Vijijini, Biharamulo na Mwanza Mjini (Nyamagana).
Katika utafiti huu uliohusisha watu 910, taarifa binafsi za wahojiwa zilizokusanywa ni pamoja na zile zinazohusu umri wa wahojiwa, jinsia, hali ya ndoa, kazi, kiwango cha elimu na vyama vya siasa vinavyoongoza majimbo sehemu uchaguzi ulipofanyika.
Lakini wakati matokeo hayo ya utafiti yakianikwa, kwa upande wa CCM, Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni akiwa mjini Songea, Ruvuma alikokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 38 ya chama hicho, alisema chama chake bado hakina mgombea mpaka sasa.
Aidha, alitumia fursa hiyo kuwataka Watanzania kuwashawishi wanaoonekana kuwa na uwezo wa kuongoza huku wakiwa hawana ‘madoa’ waweze kujitosa katika uchaguzi mkuu wa baadaye mwaka huu.CHANZO:HABARI LEO
MBOWE ATETA NA RED BRIGADE DODOMA
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akizungumza na vijana wa ulinzi wa chama hicho maarufu kama Red Brigade, (RB), kutoka Kanda ya Kati ya Mikoa ya Dodoma na Singida kwenye makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma leo Jumatatu Februari 9, 2015. Vijana hao hutumika kulinda viongozi, mali za chama na kwenye mikutano ya hadhara na ile ya ndani ya chama.
WATANZANIA WAONYWA URAIS WA FEDHA, UDINI
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amewataka Watanzania kuwapuuza wanasiasa wenye kutaka kutumia fedha, dini, ukabila na aina yoyote ya ubaguzi kujijengea uhalali na kuombea kura katika uchaguzi mkuu ujao.
Akifunga Mkutano wa Kimataifa wa Utume wa Kanisa la Waadventista Wasabato, Dar es Salaam juzi, Membe ameliomba kanisa hilo kuzungumza na vijana wao na kuwakumbusha wajibu wao wa kulinda amani na kufanya uchaguzi sahihi na kutokubali kutumika.
“Nawasihi muwapuuze wanasiasa wenye mwelekeo huo... hawa ni hatari kwa umoja na upendo wetu. Tuwachague wale wenye ulimi wa upendo, unyenyekevu, utu na amani. Tumwepuke shetani na kazi zake za ufisadi, rushwa na maovu mengine,” alisema Membe.
Mkutano huo wa kimataifa wa utume maarufu kama ‘Mission Extravaganza’ ulianza Jumatano wiki iliyopita katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na uliwahusisha waumini wa kanisa hilo kutoka nchi 11 zilizoko katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, lengo lake likiwa ni kuwaandaa watu kiakili, kijamii na kiroho ili waweze kuishi maisha yenye uadilifu.
Zaidi ya watu 2,400 walibatizwa katika mkutano huo. Membe alisema mwaka huu, licha ya nchi kufanya uchaguzi mkuu lakini pia ina tukio lingine la kura ya maoni ya katiba, hivyo akasisitiza waumini wa kanisa hilo kuliweka taifa kwenye maombi.
“Nasisitiza hilo kwa kutambua kuwa kipindi kama hiki huja na migongano na mivutano katika nchi zenye demokrasia changa.”
Membe pia alitoa rai kwa waumini wa Kanisa hilo la Waadventista Wasabato kushiriki kikamilifu katika kutengeneza viongozi bora wa Serikali wanaozingatia misingi ya uadilifu, upendo na unyenyekevu.
Membe alisema kuwa dini na madhehebu yanayo nafasi kubwa katika kujenga jamii yenye maadili na hofu ya Mungu, wakiwemo viongozi na hivyo kusababisha taifa kuwa na amani, upendo na mshikamano.
Alieleza kuwa kama Waziri wa Mambo ya Nje, amejifunza kuwa diplomasia na hofu ya Mungu vikifanya kazi pamoja hakuna changamoto yoyote isiyoweza kukabiliwa.
“Dini na Diplomasia vinahusiana pale masuala ya amani, ulinzi na usalama yanapoguswa. Hivyo nawaomba mshiriki katika kutengeneza viongozi bora katika jamii zetu kwa misingi ya uadilifu ambao watasimamia amani na kujiepusha na vitendo viovu ikiwemo rushwa,” alisema Membe.
Aidha, alilipongeza kanisa hilo kwa kuwa mfano mzuri wa ustahimilivu na uvumilivu wa kidini hapa nchini. Alieleza kwamba kamwe hajawahi kusikia Kanisa la Waadiventista Wasabato limeingia katika mgogoro na Serikali, dhehebu au dini nyingine.
Alisema hilo ni funzo kubwa kwa Watanzania, kwamba kutofautiana kiitikadi, kidini, kikabila au rangi si sababu tosha ya kuwagombanisha na kuvuruga amani ya nchi.
“Nalipongeza kanisa lenu kwa kuwa mfano mzuri wa uvumilivu wa kidini na imani, mnaendesha mambo yenu kwa uvumilivu mkubwa na kushirikiana na dini zote na hili linatufundisha kuwa kutofautiana kwetu sio sababu tosha ya kugombana,” alisisitiza Membe.
Membe alilihakikishia kanisa hilo dhamira ya Serikali ya kuendelea kushirikiana nalo kwa ajili ya ustawi wa nchi na kufafanua kuwa Serikali itaendelea kulinda uhuru wa kuabudu kwa dini zote kama inavyoelezwa kwenye Katiba ya nchi.
“Serikali inao wajibu wa kusaidia dini na madhehebu kufanya kazi kwa uhuru. Bahati nzuri Katiba inayopendekezwa imezingatia kulinda uhuru huo hivyo tuiunge mkono,” alifafanua Waziri Membe.
Aidha, amelisifu kanisa hilo kwa kuanzisha miradi ya huduma zikiwemo Shule 15 za Sekondari na Msingi, Chuo Kikuu na Hospitali mbili ambavyo vinatoa mchango mkubwa kwa serikali na wananchi kwa ujumla.
Awali akimkaribisha Waziri Membe kufunga kongamano hilo, Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo duniani, Askofu Dk Ted Wilson alisema kuwa anawaombea viongozi wa Tanzania waendelee kuwa na maono kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na kwamba wakimtumaini Mungu atawawezesha kupata maono mapya kwa ajili ya kulitumikia Taifa hili.
Kwa upande wake, Kiongozi wa Kanisa hilo Kanda ya Afrika Mashariki na Kati, Askofu Blasius Luguri aliipongeza Tanzania kwa kudumisha amani ambayo imechangia kuichagua Tanzania kuwa mwenyeji wa Kongamano hilo lililoshirikisha Mataifa zaidi ya 20.
Aidha, alimwomba Waziri Membe kufikisha ujumbe kwa Rais Jakaya Kikwete kuwa wana imani na Tanzania kuwa ni nchi ya amani, usalama na utulivu.
Kanisa la Sabato ni kanisa linalokua duniani likiwa na waumini milioni 307 huku waumini milioni 30 wakiwa Afrika na takriban milioni 5 wakiwa Tanzania.CHANZO:HABARI LEO
Sunday, February 8, 2015
Saturday, February 7, 2015
Shakira ameonyesha picha za mtoto wake aliyejifungua…
Ni mara chache kwa mastaa wa kike wa muziki Marekani kuona wakiweka picha za watoto wao mara baada ya kutoka kujifungua.
Imewachukua muda mrefu mastaa kama Kim Kardashian, Beyonce, Kelly Rowland na wengine kuonyesha watoto wao wakiwa bado wachanga lakini kwa Shakira na mume wake Gerard Piqueimekuwa tofauti kwani ni wiki moja tungu wapate ugeni katika familia yao na wameamua kuonyesha picha za mtoto wao.
Mambo saba aliyoyazungumza Mrisho Mpoto kwenye Mboni Show…
Siku ya jana February 06 kwenye Mboni Show alikuwepo Mrisho Mpoto, amepiga story na audience kuhusu vitu vingi, ikiwemo family yake, siasa na uchaguzi 2015, kilichomkuta baada ya kusikika anataka kugombea Ubunge na namna anavyomzungumzia Rais Kikwete.
Alianza kuzungumzia kuhusu familia yake; “Nina watoto wawili.. huyo mmoja ndio mtata hata simuelewi anafanya nini.. huyo mdogo ni pasua kichwa, anasema siwezi kufanya unachokifanya wewe…”
Hapa alizungumzia kuhusu kwanini hasikiki kuwa na skendo; “Maisha yanatofautiana mtu kama mimi nimekuwa kama icon, watu wengi wanapenda kujifunza kupitia kwangu. Kuna matamko ya nchi.. ya Serikali napewa mimi kwa hiyo ni vizuri sana usiingie kwenye maisha ya skendo… Najaribu kukimbia skendo.”
Kuhusiana na ishu ya kujitambua; “Wewe ni nani, swali la pili unatakiwa kujiuliza nani sio wewe? Swali la tatu kujiuliza ni nani unayemuamini? Mtu pekee unayetakiwa kumuamini kwenye maisha yako ni wewe“
Mpoto alizungumzia pia ishu ya kukutana wagombea Urais waliotangaza nia 2015; “Mwaka huu mashabiki wangu wanisamehe tu mwaka huu nina mambo mengi sana, wote hao unaowasikia 23 nimeshaonana nao.. kuna Mrisho Mpoto halafu kuna ‘Mjomba’, kule naenda kama Mrisho Mpoto. Unatakiwa usikie mawazo yao, mimi ni sauti ya watu nasikia mawazo yao halafu nitakuja kuwaambia watu”
Ishu ya kilichimkuta baada ya kutangaza kugombea Ubunge; “ Hizo simu nilizopigiwa, nikasema mmmh… ni kama unanitonesha kidonda ukiniuliza maswali hayo.. nakujibu kwa mkato sitaki hilo swali”
Jitihada zake kuinua utamaduni; “najaribu kushikilia muhimili wa nchi yetu, napambana sana kuhusiana na lugha”
Hapa aliulizwa kuhusu anavyomzungumzia Rais Kikwete; “Kama kuna nafasi kubwa ambayo tutakuja kuikumbuka ni utawala wa huyu mtu, akija kuondoka ndio watu watakuja kukumbuka”
Subscribe to:
Posts (Atom)