Saturday, February 7, 2015

Shakira ameonyesha picha za mtoto wake aliyejifungua…

sasha
Ni mara chache kwa mastaa wa kike wa muziki Marekani kuona wakiweka picha za watoto wao mara baada ya kutoka kujifungua.
Imewachukua muda mrefu mastaa kama Kim Kardashian, BeyonceKelly Rowland na wengine kuonyesha watoto wao wakiwa bado wachanga lakini kwa Shakira na mume wake Gerard Piqueimekuwa tofauti kwani ni wiki moja tungu wapate ugeni katika familia yao na wameamua kuonyesha picha za mtoto wao.
sasha 2Katika picha hiyo wawili hao waliandika kuwa wanafuraha kubwa kumkaribisha mtoto wa pili Sashakatika familia yao na kuwashukuru mashabiki wao kwa kuwatakia heri.

Mambo saba aliyoyazungumza Mrisho Mpoto kwenye Mboni Show…


mboni iii
Siku ya jana February 06 kwenye Mboni Show alikuwepo Mrisho Mpoto, amepiga story na audience kuhusu vitu vingi, ikiwemo family yake, siasa na uchaguzi 2015, kilichomkuta baada ya kusikika anataka kugombea Ubunge na namna anavyomzungumzia Rais Kikwete.
Alianza kuzungumzia kuhusu familia yake; “Nina watoto wawili.. huyo mmoja ndio mtata hata simuelewi anafanya nini.. huyo mdogo ni pasua kichwa, anasema siwezi kufanya unachokifanya wewe…
Hapa alizungumzia kuhusu kwanini hasikiki kuwa na skendo; “Maisha yanatofautiana mtu kama mimi nimekuwa kama icon, watu wengi wanapenda kujifunza kupitia kwangu. Kuna matamko ya nchi.. ya Serikali napewa mimi kwa hiyo ni vizuri sana usiingie kwenye maisha ya skendo… Najaribu kukimbia skendo.
Kuhusiana na ishu ya kujitambua; “Wewe ni nani, swali la pili unatakiwa kujiuliza nani sio wewe? Swali la tatu kujiuliza ni nani unayemuamini? Mtu pekee unayetakiwa kumuamini kwenye maisha yako ni wewe
Mpoto alizungumzia pia ishu ya kukutana wagombea Urais waliotangaza nia 2015; “Mwaka huu mashabiki wangu wanisamehe tu mwaka huu nina mambo mengi sana, wote hao unaowasikia 23 nimeshaonana nao.. kuna Mrisho Mpoto halafu kuna ‘Mjomba’, kule naenda kama Mrisho Mpoto. Unatakiwa usikie mawazo yao, mimi ni sauti ya watu nasikia mawazo yao halafu nitakuja kuwaambia watu

Mboni IV
Ishu ya kilichimkuta baada ya kutangaza kugombea Ubunge; “ Hizo simu nilizopigiwa, nikasema mmmh… ni kama unanitonesha kidonda ukiniuliza maswali hayo.. nakujibu kwa mkato sitaki hilo swali
Jitihada zake kuinua utamaduni; “najaribu kushikilia muhimili wa nchi yetu, napambana sana kuhusiana na lugha
Hapa aliulizwa kuhusu anavyomzungumzia Rais Kikwete; “Kama kuna nafasi kubwa ambayo tutakuja kuikumbuka ni utawala wa huyu mtu, akija kuondoka ndio watu watakuja kukumbuka

Alichokijibu Mbunge Mbatia kuhusu ishu ya kusema kuwa Mrema ni mgonjwa…

Mrema II
Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema (TLP) alitoa hoja binafsi Bungeni kwamba Mbunge James Mbatia amekuwa akipita Jimbo la Vunjo na kuwaambia wapigakura wasimchague Mrema kwa sababu ni mgonjwa.

Napenda kusema kuwa mimi ni mbunge halali wa Vunjo na Mbatia hatapata jimbo hilo na ninatangaza kuwa nitagombea tena na hafi mtu hapa“– Alisema Mrema wakati akimalizia kuwasilisha hoja yake hiyo.
Leo wakati wa kikao cha Bunge jioni, Mbunge Mbatia alipata nafasi kujibu kuhusu ishu hiyo; “Maelezo haya nayatoa kukanusha kwa moyo wangu wote matamshi yaliyotolewa ndani ya Bunge hili na Mheshimiwa Augustine Lyatonga Mrema, Mbunge wa Vunjo. Siku ya tarehe 05/02/2015 wakati wa kuahirisha Bunge Mheshimiwa Mrema alitoa maelezo ambayo sio sahihi alipoeleza kuwa mimiJames Francis Mbatia niliwahi kusema kuwa yeye ni mgonjwa anayeugua maradhi ya ukosefu wa kinga mwilini yaani UKIMWI
Maelezo yote aliyoyatoa sio sahihi na sijawahi na sitawahi kutamka maneno hayo…  Sijawahi kumnyanyapaa Mheshimiwa Mrema wala mtu yoyote aliyeathirika na maradhi ya aina yoyote
Mimi sina uadui na mtu yoyote akiwepo mheshimiwa Mrema hata sasa hivi amekaa kwenye kiti changu sina ugomvi nae. Nimezaliwa na nimekuzwa kwenye familia ya wacha Mungu siwezi nikafanya hivyo..  To grow old is mandatory but to be wise is optional…
Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi Mkuu ni rai yangu kwa watanzania wote wachague vionzozi wenye uwezo, wacha Mungu, wakweli na wenye kuchukia propaganda, ubaguzi, chuki, ubinafsi na ubinafsi
Baadhi ya viongozi wanadai kuwa wana hatimiliki ya maeneo wanayoongoza dhana hii sio sahihi, nataka kuwahakikishia Watanzania wenye hatimiliki ya nchi yao ni Watanzania wenyewe

SPLM YAANZA UTEKELEZAJI WA MAKUBALIANO YA ARUSHA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (wa tatu kutoka kushoto) akiwa kwenye mazungumzo na Ujumbe wa Viongozi wa Makundi ya Chama cha SPLM cha Sudan ya Kusini
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (wa tatu kutoka kushoto) akiwa kwenye picha ya na Ujumbe wa Viongozi wa Makundi ya Chama cha SPLM cha Sudan ya Kusini
Ujumbe wa Viongozi wa Makundi ya Chama cha SPLM cha Sudan ya Kusini yalifanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mjini Dar es Salaam jana.

WACHEZAJI WA SIMBA WAKIWA KATIKA MAZOEZI JIJINI TANGA

Kocha wa Simba, Goran Kopunovic (mwenye mpira) akitoa maelekezo kwa wachezaji wake katika mazoezi ya timu hiyo kujiandaa na mchezo wa leo dhidi ya Coastal union.
Kiungo mshambuliaji wa Simba, Emannuel Okwi (katikati) akijaribu kumtoka kiungo wa timu hiyo, Jonas Mkude na beki, Hassani Kessy kwenye Uwanja wa Popatlal, Tanga.(P.T)
Kocha wa Simba, Goran Kopunovic akifanya mazoezi pamoja na beki wa kushoto wa timu hiyo, Issa Rashidi 'Baba Ubaya' yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Popatlal, Tanga kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Coastal utakaopigwa leo.
Kocha, Goran Kopunovic akimuelekeza jambo kiungo wa timu hiyo, Mganda, Simon Sserunkuma baada ya mazoezi ya timu hiyo jijini Tanga.

WASTARA ATOA MANENO YA UCHUNGU, YAWAGUSA WENGI!

Wastara Atoa Maneno ya Uchungu, Yawagusa Wengi!
Muigizaji wa filamu,Wastara Juma amewapa watu simamzi zito mtandaoni, baada ya leo kuandika maneno mazito ya uchungu akisema matatizo ya dunia yamemzidia na kubandika picha akiwa analia. Na hivyo kupelekea mashabiki wengi kumpa pole na kumtia moyo kuwa yote yana mwisho wake na Mungu ndio mpagaji wa yote.
"Hapa duniani kila mtu ana shida na matatizo lakini kwangu mimi yamezidi daaah eeeh Mungu nibadilishe basi hiyo nafasi ya mteso uliyoniweka muweke mwingine nami unipe furaha nicheke kama wengine maishani mwangu niache kulia eeeh Mungu baba jamani mimii mimiii aah".-Wastara aliandika baada ya kuweka picha hiyo hapo juu.
Hakuweka wazi nini hasa kimempata,lakini picha hii inaonekana imetoka kwenye moja ya kipande cha filamu.(P.T)
Chanzo:http://www.bongomovies.com/

TANZANIA YATANGAZA UTALII PARIS KUPITIA MAWAKALA WA UTALII

Baadhi ya wadau wa utalii wakimsikiliza Mh Balozi Begum Taj
Wageni wakionja baadhi ya vyakula vya kitanzania.
Ukarimu kwa wageni ni tunu ya watanzania.
Picha ya jumla ya walioshiriki katika hafla ya kuitangaza Tanzania.(P.T)

MAGAZETI LEO JUMAMOSI

Tuma Maoni

1000 herufi zilizobaki

Security code

Anzisha upya

TANZIA: MWAJUMA ABDALLAH 'MAMA MASHAKA' AMEFARIKI DUNIA.

TANZIA: MSANII wa maigizo aliyewahi kuwika na kundi la Kaole Sanaa Group, Mwajuma Abdallah 'Mama Mashaka' amefariki dunia.
Mama Mashaka amefariki usiku wa kuamkia leo majira ya saa tano za usiku katika Hospitali ya Amana iliyopo Ilala, jijini, Dar.GPL(P.T)

Friday, February 6, 2015

KUINGIA KWA SEKTA YA AFYA KATIKA BRN KUNALETA MATUMAINI MAPYA

kip1
Mtendaji Mkuu wa PDB Bw. Omari Issa akielezeaumuhimu wa sekta ya Afya kuingia BRN kuungana na sekta nyingine zilizotangulia zinazoendelea kuzaa matunda
kip2
Dr Linda Ezekiel ambae ni Mkurugenzi wa sekta za jamii (Afya, Elimu na Maji) PDB akiwasilisha mada kuhusu malengo ya kipaumbele sekta ya afya kwa miaka
kip3
Bw. Omari Issa akimkabidhi mwakilishi wa wahisani wa maendeleo mkakati wa sekta ya Afya chini ya BRN.
kip4
Mmoja wa wahisani akisisitiza umuhimu wa wizara ya afya kuwajibika ki BRN katika maeneo mengine yasiyo ya kipaumbele katika BRN
kip5
Dr Oberline Kisanga wa kitengo cha mageuzi katika wizara ya afya akifafanua ushiriki wa TAMISEMI katika mkakati huu wa afya chini ya BRN
kip6
Mwakilishi wa jumuiya ya wahisani akipongeza uamuzi wa serikari kuiweka sekta ya afya katika BRN
......................................................................................................
Annastazia Rugaba, PDB habari, 05 Februari 2015.
Mtendaji mkuu wa Ofisi ya Rais, usimamizi wa utekelezaji wa miradi (PDB) Bwana Omari Issa, leo amekabidhi rasmi taarifa ya mkakati wa kuboresha sekta ya afya chini ya BRN kwa jumuia ya wahisani wa maendeleo. Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za PDB ambapo jumuiya ya wahisani ilipata fursa ya kusikiliza kwa kina namna BRN inavyofanya kazi ya kuleta matumaini mapya kwa watanzania kupitia sekta za kipaumbele.
Sekta ya afya imekuwa ikijaribu kuboresha utendaji wake lakini kuingia katika BRN kutaleta tija Zaidi. BRN inaamini katika misingi mikuu ambayo ni kuweka vipaumbele, kuwa na adabu ya utekelezaji, uwajibikaji na uaminifu, ufuatiliaji wa kina na wa mara kwa mara na Mawasiliano thabiti kati ya watoa huduma na wapokea huduma. Hizi ni nguzo muhimu zitakazotufikisha katika dira ya maendeleo ya taifa ya Mwaka 2025.
Awamu ya kwanza ya BRN iliziangazia sekta sita ambazo ni Kilimo, Elimu, Maji, Uchukuzi, Nishati na ukusanyaji wa mapato ambapo sekta za Afya na Uboreshaji wa mazingira ya Biashara zimeanza rasmi Mwaka huu. Sekta sita za mwanzo zimedhihirisha mafanikio anuwai ambayo yaliwavutia jopo la wataalamu wa maendeleo wakiongozwa na Rais Mstaafu wa Botswana Bw Mogae. Ripoti kamili ya utekelezaji wa BRN kwa Mwaka wa kwanza itazinduliwa rasmi mapema mwezi Machi Mwaka huu.
Sekta ya afya inakusudia kutekeleza vipaumbele vine ambavyo ni mosi; ugawanyaji sawia wa wahudumu wa afya wenye ujuzi takikana kuanzia ngazi ya chini ya afya ya msingi, pili; utoaji huduma wenye ubora wa nyota tatu katika ngazi zote, tatu; upatikanaji wa dawa na bidhaa muhimu za afya katika ngazi zote, nne; kuimarisha afya ya uzazi na usalama wa mama na mtoto ili kupunguza vifo vya kundi hili muhimu kwa angalau asilimia 60 ifikapo Mwaka 2018.
Jumuiya ya wahisani wamepongeza uamuzi wa kuiingiza sekta ya afya katika BRN na wakithibisha utayari wao wa kufanikisha mkakati huu, wametoa wito kwa wizara ya afya, PDB, Sekta binafsi na jamii ya kitanzania kwa ujumla kuhakikisha kuwa mkakati huu utafanikiwa.
Malengo haya yote yanahitaji juhudi kubwa na ya pamoja kutoka kwa jamii, wizara na taasisi zake zote hadi ngazi ya kijiji, wahisani wa maendeleo na sekta binafsi. "tusingoje nani aanze, sote tuwajibike, kila mmoja ajitazame kama anawajibika ipasavyo. Dira ya maendeleo ya Taifa tunayotaka itupeleke kuwa nchi yenye uchumi wa kati haiwezi kufikiwa tusipofanya kazi kwa pamoja bila kunyoosheana vidole. BRN ni treni iliyoanza safari tayari, kila mmoja anawajibika kuingia kwa wakati na kwa nia Chanya, ukichelewa ukakuta imeondoka bado una fursa ya kuikimbilia kituo kinachofuata ili twende pamoja" Bw Omari Issa ametoa wito huo kwa wahisani wa maendeleo na jamii kwa ujumla.

BALOZI WA RWANDA AONANA NA DR.K SHEIN ZANZIBAR

BALO1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania Eugene S.Kayihura alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo Picha na Ikulu.]
BALO2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akibadilishana mawazo na Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania Eugene S.Kayihura (katikati) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar (kushoto) Mshauri wa Rais Uhusiano wa Kimataifa, Uchumi na Uwekezaji Balozi wa Mohamed Ramia Abdiwawa. Picha na Ikulu.]

SEMINA YA UBORESHAJI YA DAFTARI LA WAPIGA KURA MKOANI LINDI

Wasimamizi wa uchaguzi manispaa ya Lindi wakiwa kwenye semina ya maboresho ya daftari la wapiga kura yaliyokuwa yanaendeshwa na tume ya uchaguz
Afisa tume ya uchaguzi akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa uchaguzi na mafisa uchaguzi wilaya za mkoa wa Lindi kuhusu marekebisho ya tafutari la wapigakura 
Wasimamizi wa uchaguzi manispaa ya Lindi wakiwa kwenye semina ya maboresho ya daftari la wapiga kura yaliyokuwa yanaendeshwa na tume ya uchaguz

Mwaandishi wetuLindi

Vyama siasa mkoani Lindi vimeshauriwa kuteuwa mawakala
wa adilifu na 
waaminifu katika uchaguzi mkuu ujao ili kuepusha malalamiko
na migogoro 
isiyo na tija.
Wito huo ulitolewa   na katibu tawala wa mkoa huo Abdallah
Chikota wakati 
anafungua mafunzo ya uboreshaji daftarila wapiga kura kwa
 wasimamizi na Maafisa wa uchaguzi mkoani humo. 
Chikota alisema baadhi ya malalamiko na migogoro
 inayotokea mara kwa mara
 baada ya chaguzi inatokana na vyama kuwateua na
 kuwapeleka watu wasio 
makini,waaadifu na waaminifu kwenye vituo vya kupigia na
 kuhesabia kura. 
Alisema hali hiyo inasababisha malalamiko na migogoro
ambayo kama 
mawakala watakuwa makini inaweza kuepukwa.Alibanisha
 kwamba baadhi ya
 mawakala wanasahu wajibu wao na kujipa majukumu ya siyo
 wahusu ikiwamo kutoa maelekezo kwa wasimamizi.
Kitendo ambacho hakikubaliki kwa mujibu wa kanuni,taratibu
 na sheria.
"wakala hapaswi nasiowajibu wake kutoa maelekezo kwa
msimamizi wa 
uchaguzi kwani kufanya hivyo nikuingilia majukumu na utendaji
 ma tume,
" alisema Chikota.
Aliongeza kusema mawakala ambao sio makini,waadili na
waaminifu mara 
nyingi hupeleka takwimu za uongo kwa vyama vyao kutokana
 na kushindwa 
kujua na kutekeleza majukumu yao.
Aidha katibu tawala huyo aliwataka wasimamizi hao kuepuka
 upendeleo kwa
 chama chochote cha siasi kwani wanaweza pia kuwa chanzo
 cha malalamiko 
na migogoro." ninyi mnatakiwa kutenda haki kwani kama
waamuzi wa mchezo,
sasa kama mwamuzi anaipendelea timu mojawapo kwenye
mchezo nilazima 
yataibuka malalamiko na fujo ikitokea hivyo ni mwamuzi
 atakuwa
 amesababisha," aliongeza kusema Chikota.

ADVERTISEMENT

0 COMMENTS:

Post a Comment


:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-#=p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer 
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.