Saturday, January 3, 2015

Idara ya polisi yaongoza kwa ufisadi TZ

Jeshi la polisi nchini tanzania ndio taasisi fisadi zaidi chini humo
Idara ya polisi ndio taasisi inayochukua hongo zaidi nchini Tanzania kulingana na ripoti ya ufisadi katika jumuiya ya Afrika mashariki.
Ripoti hiyo inasema kuwa maafisa wa polisi walipokea asilimia 25 ya hongo zote zilizotolewa kwa wafanyikazi wa taasisi za uma mwaka uliopita.
Ya pili ni idara ya mahakama,ambayo wafanyikazi wake walitia mfukoni asilimia 18 ya hongo,huku mashirika yalio na majukumu ya usajili na utoaji wa leseni yakiwa katika nafasi ya tatu kwa asilimia 10.
kwa mujibu wa gazeti la The Citizen, Idara ya Polisi nchini Tanzania imetajwa kuwa ya tatu kwa ufisadi katika jumuiya ya Afrika mashariki.
Polisi wa Uganda wanaongoza wakifuatiwa na wale wa Kenya katika nafasi ya pili na wale wa Burundi wakiwa katika nafasi ya nne.
Kulingana na ripoti hiyo maafisa wa polisi wa Rwanda ndio wasiochukua hongo ya juu Afrika mashariki.
Utafiti huo ulifanywa mwezi Julai na Agosti mwaka uliopita na shirika la lenye na maslahi ya kimaendeleo barani afrika ForDIA likishirikiana na Jukwaa la uwazi nchini tanzania Trafo.

mmiliki wa VIP enginering(james lugamalila) afungua kesi mahakamani

Mmiliki wa VIP Enginering, aliyekuwa anamiliki hisa IPTL Ndugu Rugemalira amefungua kesi mahakama kuu akiidai serikali jumla ya Sh. 398 bilion zilizokuwemo/ zinazotakiwa kuwemo katika Escrow Account ya Tegete na zilizolipwa kwa kampuni ya PAP na kuleta mjafala mkubwa bungeni.

Katika madai yake, mwenye hisa hatambui malipo yote yaliyolipwa na serikali kwa kampuni ya PAP kwani kampuni hiyo haikuwa na nyaraka halali kutoka kwa msajili wa makampuni BRELA, Taxe Clearance Certificate kutoka TRA, kuandikishwa Tanzania Investment Center na wala mmliki wake kuwa na vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini kutoka idara ya Uamiaji.

Katika hoja yake mdai anasema kuwa ni jukumu la serikali kuwahakiki wawekezaji wa nje ili kuwalinda wawekezaji wa ndani pindi tu wanapoingia ubia na wawekezaji wa nje. Ameendelea kudai kuwa, kwa uzembe huo wa serika kwa kutotimiza uhakiki wake wa kigeni ulisabibisha kampuni yake ya VIP Engineering kuingia ubia na Kampuni Feki na kumsababishia hasara ya sh. Bilion 56 kwani alizimika kuvunja ubia wao na kumfungulia mashitaka mbia mwenza PAP baada ya kugundua ubabahishaji wa uhalali wa kampuni hiyo. 

Hivyo ameitaka tena serikali kulipa gharama zote alizotumia kuendesha kesi sh.36.8 bilion.
Aidha amedai kuwa aliwafahamisha serikali kutolipa malipo yoyote yaliyokuwemo kwenye account ya Escrow na endapo serikal ingeona kuna haja ya kufanya hivyo basi ilipe kwa VIP au IPTL account ambayo yeye alikuwa signatory. 

Katika uwasilishaji wake mahakamani hapo anadai kutofahamu au kutambua kulipwa kwa PAP. Hivyo serikali inatakiwa kulipa tena madai yote kwa VIP au IPTL. Amewapa serikali siku 14 tu toka 1 Januari,2015 kuwa wamelipa malipo yote.

Katika madai hayo, ili kuyadhitisha ameambatinisha:
1. Report ya Mkaguzi mkuu wa hesabu za serika inayodhibitisha baadhi ya pesa kulipwa kwa PAP

2. Mkaguzi mkuu kudhibitisha kuwa mlipwaji hajawahi kusajiliwa kama mlipa kodi wala kupewa Taxe clearance certificate.

3. Report ya mdhibi mkuu wa Rushwa kuthibitisha kuwa kampuni iliyolipwa haikusajiliwa BRELLA na wala haikuwa na sifa au uhalali kufanya kazi yoyote ya ugavi dhidi ya Shirika lolote la Uma.

3. Report ya Bunge kama muhimili mwingine wa nchi kupitia kamati yake ya hesabu za serikali na mashirika ya uma kutodhibitisha/kudhibitisha juu uhalali wa PAP, mmiliki wa kampuni ya PAP na utendaji wake wa kazi.

4. Mapendekezo ya kamati ya bunge kwa serikali dhid ya PAP, mali zake na mmiliki wake.

5. Mapendekezo ya bunge kwa serikali yanayodhibitisha kuwa PAP haikuwa halali.

6. Mapendezo ya bunge kwa serikali juu ya watendaji wote walioshilikiana kwa pamoja ya kuilipa kampuni isiyo halali.

7. Baadhi ya magazeti likiwemo gazeti la serikal kudhibitisha mkuu wa nchi kupokea na kuridhia mapendezo hayo.

8. Magazeti pamoja na la serikali kudhibitisha serikali kwa kuwaadhibu watendaji wote waluofanya udhembe wa kulipa kampuni isiyo halali.

9. Mkanda wa video ya Rais wa nchi katika hotuba yake kukili watendaji wake kuilipa kampuni isiyo halali na kawasimamisha kazi kwa uzembe huo.

10. Barua ya Mwanasheria mkuu wa serikali kwa Rais ya kuomba kujiuzuru kwa kufanya uzembe huo wa kulipa kampuni isiyo halali.

11. Barua ya Rais kwa Mwanasheria mkuu kukubali kujiuzuru kwake kwa kutoa ushahuri wa kulipa kampuni isiyo halali.

Kesi hiyo uenda ikaamsha tena hasia za wanachi juu ya malipo ya Escrow account. Ni mtihani mwingine kwa serikali kwani Bunge na wanachi hawako tiyari kuona pesa kama hiyo ikilipwa tena.

askofu aeleza namna alivyoingiziwa mamilioni

Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa(pichani), amevunja ukimya kuhusu mgao wa Sh. milioni 40 alioupata kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya VIP Engineering & Marketing Limited, James Rugemalira.

Ukimya wa Askofu Nzigilwa unatokana na sakata la uchotwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 kutoka akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT). 

Akaunti hiyo ilifunguliwa baada ya waliokuwa wanahisa wa Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ikiwamo VIP kuingia katika mgogoro na Shirika la Umeme nchini (Tanesco).

Taarifa kwa vyombo vya habari jana ilisema fedha alizopewa Askofu Nzigilwa na Rugemalira, zilikuwa za matoleo kwa ajili ya maendeleo ya Kanisa.

Alisema kiutaratibu siyo vibaya kwa waumini kutoa michango na matoleo kwa Kanisa na watumishi wake.

Katika taarifa hiyo ambayo Askofu Nzingilwa alipotafutwa alithibitisha kwamba ni yake, alifafanua kuwa alifahamiana na familia ya Rugemalira tangu akiwa Paroko Msaidizi wa Parokia ya Makongo Juu, Dar es Salaam na hata baada ya kuteuliwa kuwa Askofu Msaidizi wameendelea kushirikiana na kuwasiliana katika masuala mbalimbali ya kikanisa na kijamii.

“Samahani nipo kwenye kazi fulani hatuwezi kuongea kwa sasa. Ni kweli kuna taarifa nimeitoa leo kwa Tumaini Media na nimewaambia waitume pia kwa vyombo vingine vya habari,” alisema Askofu Nzingilwa alipowasiliana na NIPASHE kwa kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno (sms).

Askofu Nzingilwa katika taarifa hiyo aliyoisaini juzi, alisema mwanzoni mwa Februari 2014, Rugemalira alimuomba namba ya akaunti yake ya benki ya Mkombozi ili aweke matoleo yake.

Alisema aliombwa akaunti yake na Rugemalira mapema Februari, mwaka jana na kwamba hakuwahi kufahamu kiasi cha fedha kilichowekwa kwenye akaunti yake hadi alipoangalia taarifa ya benki Februari 27, mwaka jana iliyoonyesha aliingiziwa Sh. milioni 40.4.

“Niliwasiliana na Rugemalira na kumwambia nimeona kiasi kikubwa cha fedha katika akaunti yangu, naye akaniambia hayo ni matoleo yake ambayo anaamini yatasaidia katika shughuli zetu za kitume na kichungaji. Nikamshukuru kwa ukarimu huo mkubwa,” alibainisha Askofu huyo.

Alisema matoleo hayo yalipokelewa kwa moyo mnyofu kutoka kwa mtu anayefahamika kwa ukarimu wake katika kusaidia Kanisa na watumishi wake.

“Kampuni anazomiliki na biashara anazofanya Rugemalira kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, haviwezi kumpa shaka mtu anayemfahamu kuhusu uwezo wake au kampuni yake kutoa mchango mkubwa kama huo,” alisema.

Alisema ni desturi ya kawaida katika Kanisa kwa waamini kutoa michango na matoleo mbalimbali kila mmoja kwa kadri ya uwezo na ukarimu wa moyo wake na kwamba matoleo ya waamini hutumika katika shughuli za uinjilishaji na uendeshaji wa Jimbo, Parokia na taaisi zake.

Askofu huyo aliongeza kuwa hutumika katika miradi maalum iliyokusudiwa na matoleo hayo na kwa kadri ya matakwa na lengo la mtoaji.

“Nilipokea matoleo hayo kwa roho safi na moyo mweupe na wa shukrani kama tunavyofanya siku zote tunapopokea ukarimu wa michango na matoleo ya waamini wetu. Na tangu matoleo hayo yalipotolewa Februari, mwaka jana, hakuna mamlaka yoyote iliyowahi kuniuliza ,” alifafanua na kuongeza:

“Nawaomba waamini tuendelee kujitoa kwa hali na mali katika kulijenga Kanisa la Mungu; kila aliyepewa talanta na Mungu aitumie kwa kuzalisha matunda mema ili kulijenga kanisa letu na hatimaye kuurithi ufalme wa mbinguni.”

Hata hivyo, alisema Kanisa hilo litaendelea kuwa mstari wa mbele katika kutetea haki, ukweli na uadilifu, na halitarudi nyuma wala kukaa kimya katika kukemea maovu katika jamii.

UHUSIANO NA FAMILIA YA RUGEMALIRA
Alisema familia ya Rugemalira ni waumini wakatoliki wanaosali katika Parokia ya Bikira Maria Malkia wa Rozari Takatifu, Makongo juu katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam na kwamba ni washiriki wazuri katika shughuli za ibada na wamekuwa na moyo mkubwa wa ukarimu katika kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo ya Kanisa ndani na nje ya jimbo.

“Binafsi, nimeifahamu familia hii muda mrefu kutokana na majitoleo yao katika shughuli za Kanisa na uhusiano baina yangu na familia hiyo ulizidi kuimarika pale alipopangwa kufanya huduma za kichungaji katika Parokia ya Makongo Juu nikiwa Paroko Msaidizi, mwaka 2008,” alibainisha na kuongeza:

“Kipindi hicho ilikuwa katika harakati za ukamilishaji wa ujenzi wa nyumba ya mapadre na mikakati ya ujenzi wa Kanisa jipya la Parokia na walikuwa wachangiaji wazuri katika kufanikisha.”

Hata hivyo, aliwaomba waumini wa kanisa hilo kuendelea kujitoa kwa hali na mali katika kulijenga Kanisa la Mungu. 

Aidha, Askofu huyo alisema utume wa kanisa siku zote umekuwa ukiwezeshwa na kutegemezwa kwa nguvu ya Mungu Roho Mtakatifu anayeliongoza kanisa katika ukweli wote, na kwa sadaka, matoleo na michango mbalimbali ya hali na mali kutoka kwa waamini na watu wengine wenye mapenzi mema waliopo ndani na nje ya nchi.

“Kwa waumini kutoa michango na matoleo kwa kanisa na watumishi wake ni jambo la kawaida katika desturi za imani yetu tangu nyakati za mitume,” alisema Askofu Nzigilwa.

KASHFA YA ESCROW
Mei, mwaka jana, Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, aliibua kashfa ya kuchotwa kwa zaidi ya Sh bilioni 306 katika akaunti ya Tegeta Escrow, ambayo ilipingwa vikali na baadhi ya wabunge na viongozi wa serikali na Mbunge huyo kutakiwa kufuta kauli kwa kulidanganya Bunge.

Mbunge huyo aliendelea na msimamo wake na kutaka Bunge kuunda kamati ya kuchunguza sakata hilo.Juni mwaka jana, Bunge liliagiza Ofisi ya CAG kufanya ukaguzi wa fedha hizo na ripoti yake kuwasilishwa Bungeni.

Baada ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kukamilisha kazi yake, ripoti hiyo ilikabidhiwa kwa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), chini ya uenyekiti wa Zitto Kabwe.

Kamati hiyo ilifanya uchunguzi na kuweka wazi ripoti na mapendekezo yake ya awali ambayo yalizua mjadala mkali bungeni kiasi cha kutishia Bunge kushindwa kufikia maamuzi ya pamoja na baadaye Spika Anne Makinda, aliunda kamati ya maridhiano ambayo ilikubaliana katika maazimio yaliyowasilishwa Bungeni na Zitto.

Novemba 26, mwaka jana, Zitto, aliwasilisha ripoti iliyowataja viongozi wa dini, serikali na watu wengine waliopokea fedha za Tegeta Escow.

Viongozi wa dini waliotajwa na Zitto kiasi cha fedha walichopokea kwenye mabano ni Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini (Sh. milioni 80)  Askofu Eusebius Nzigirwa na Padri Alphonce Twimanye Simon (Sh. milioni 40.4), ambao walipewa fedha hizo kupitia Benki ya Mkombozi.

VIONGOZI WA SERIKALI WALIOWAJIBIKA 
Desemba 16, mwaka jana, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, alijiuzulu nafasi kutokana na ushauri alioutoa.

Desemba 22, mwaka jana, Rais Jakaya Kikwete, alimfukuza kazi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, ambaye katika kashfa hiyo alipokea kiasi cha Sh. bilioni 1.6, huku akimuweka kiporo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

Desemba 23, mwaka jana, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alimsimamisha kazi Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake.

VIONGOZI WENGINE WALIOPATA MGAWO
Viongozi waliopata mgawo wa Rugemalira Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (bilion 1.6); Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (milioni 40.4); Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Daniel Yona (milioni 40.4); Mbunge mstaafu Paul Kimiti (milioni 40.4); Msajili wa zamani wa Hazina na Mjumbe wa Bodi ya Tanesco, Dk. Enos Bukuku (milioni 161.7).

Wamo pia Jaji Profesa Eudes John Ruhangisa (milioni 404.25) na Jaji Aloysius Mujulizi (milioni 40.4).

Watumishi wa umma ni aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa wa Rita, Philip Saliboko (milioni 40.4); aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Emmanuel Ole Naiko (milioni 40.4) na Mtumishi wa TRA, Lucy Appolo (milioni 80.8).

Baada ya Nikki Mbishi kutangaza kuacha muziki, haya ndio maneno ya Chid Benz

.
.
Baada ya msanii wa Hip Hop Nikki Mbishi aka Baba Malcom kutangaza kuwa ameacha kufanya kazi ya muziki sasa Chid Benz amekanusha taarifa hizo na kusema kuwa ameshafanya mazungumzo na msanii huyo  na kumtaka asichukue uamuzi huo mapema kwani hata yeye amepitia katika changamoto hizo.
Chid Benz alichukua nafasi hiyo kuwataarifu mashabiki wa muziki kupitia ukurasa wafacebook na kuandika ‘Nakanusha habari za Nikki mbishi kuacha mziki,nimeongea nae kama kaka na kumgusia mengi,najua amenielewa na nimemwambia asikubali wale wanaomkubali waanze kukubali wengine.mimi nimekumbana na vingi na watu weengi waliaminishwa kama nimeshushwa kimziki,jimefanyiwa mengi ambayo kwa muda ule nsingeweza kuelezea kila mtu nini kinaendelea,so if kikitokea kibaya kinatangazwa mpk kwenye taarifa za habari mbona mziki hauchezwi?ningekua sina nguvu hio nisingesumbua watu kuniweka front page..but bado nipo na nimekomaa.na naishi na naona wanaopewa kipaumbele na najua bado mimi ni mimi.Iron
.

Friday, January 2, 2015

Mayweather aringishia utajiri wake kwenye instagram.

floyd
Bondia Mmarekani mwenye mbwembwe nyingi Floyd ‘Money’ Mayweather siku zote amekuwa na tabia ya kuonyesha au kuringishia utajiri wake mbele za watu na amekuwa hana aibu katika hilo .
Akitumia ukurasa wake wa Instagram Floyd ijumaa hii alipost picha zinazoonyesha kabati ambalo limejaa viatu ambapo aliandika Caption ya kuwataka watu wanamfuata kumshauri ni viatu gani avivae kwa siku hiyo .
Mayweather alifichua kuwa ana pea zaidi ya 80 za viatu aina ya sneekers viatu ambavyo vinauzwa kwa bei ya juu ambavyo kwa utajiri wake ni vitu vidogo sana .
Pea 80  za viatu za Bondia Flloyd Mayweather .
Pea 80 za viatu za Bondia Flloyd Mayweather .
Kama hiyo haitoshi Mayweather alitumia ukurasa huo huo wa Instagram kuwauliza mashabiki ni miwani gani ambayo itampendeza akiivaa .
Mayweather aliwauliza mashabiki wamshauri avae miwani ipi kati ya hii inayoonekana kwenye picha .
Mayweather aliwauliza mashabiki wamshauri avae miwani ipi kati ya hii inayoonekana kwenye picha .
Siku za nyuma Mayweather alishawahi kupost picha inayoonyesha saa zake za mkononi ambazo thamani yake kwa pamoja na dola milioni 2 .
Hivi karibuni Bondia huyo mwenye rekodi ya kuopoteza pambano lolote tangu alipoanza kucheza masumbwi ya kulipwa alithibitisha kuwa atapanda ulingoni mwaka mwezi mei tarehe 2 kupambana na mpinzani wake wa muda mrefu Manny Pacquiao.
Saa za kifahahri za Mayweather ambazo jumla zina thamani ya dola milioni 2.
Saa za kifahahri za Mayweather ambazo jumla zina thamani ya dola milioni 2.

Sheria ya usalama yakatwa makali Kenya

prince rpbert
mahakama ya kenya
Mahakama kuu nchini Kenya imesimamisha kwa muda matumizi ya baadhi ya vipengee vya sheria ya usalama yenye utata iliopitishwa na bunge na kuidhinishwa na Rais Uhuru Kenyatta.
Wanasiasa wa upinzani waliwasilisha kesi mahakamani kupinga uhalali wa sheria hiyo kikatiba, huku wakisema inahujumu haki ya raia wa Kenya.
Sheria hiyo iliidhinishwa majuma mawili yaliyopita bungeni huku wabunge wa upinzani na serikali wakikabiliana kwa makonde na mateke.
Bunge la Kenya

MAJARIBIO BVR YAKUMBWA NA CHANGAMOTO LUKUKI


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akizunguza na waandishi wa habari  Makao makuu ya tume ya uchaguzi jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akizunguza na waandishi wa habari Makao makuu ya tume ya uchaguzi jijini Dar es salaam.
Mashine ya kuandikisha wapiga kura maarufu kama Biometric Voters Registration (BVR).
Mashine ya kuandikisha wapiga kura maarufu kama Biometric Voters Registration (BVR).
Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania imetoa ripoti ya tathmini ya majaribio ya matumizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura (Pilot Registration) kwa mfumo wa Biometric Voters Registration (BVR) uliofanyika wiki moja iliyopita.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva  amesema kwamba  zoezi la Majaribio la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lilifanyika kwa siku saba (7) katika Kata za Bunju na Mbweni katika Jimbo la Kawe, Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam; Kata za Ifakara, Kakingiuka, Ipangala, Mlabani na Viwanja Sitini katika Jimbo la Kilombero Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro; na Kata za Ikuba, Usevya na Kibaoni katika Jimbo la Katavi, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi.
Katika zoezi hilo la majaribio  Jumla ya BVR Kits 250 zilitumika katika Uboreshaji huo kwa mgawanyo ufuatao:- Halmashauri ya Kilombero BVR Kits 80, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele BVR Kits 80 na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni BVR Kits 90. Vituo katika Kata zote vilikuwa vinafunguliwa saa 2.00 asubuhi na kufungwa saa 12.00 jioni.
“Katika majaribibio hayo idadi kubwa ya watu ilijiokeza kujiandikisha  Mkoa wa Dar es salaam, Kata za Bunju Wapiga Kura 15,123 waliandikishwa kati ya 27,148 na Kata ya Mbweni Wapiga Kura 6,200 waliandikishwa kati ya 8,278. Takwimu hizi za waliondikishwa inatokana na makisio ya watu tuliyokuwa tumejiwekea kutokana na matokeo ya sensa mwaka 2012″.Alisema Luuva
Mkoa wa Morogoro Kata za Ifakara, Kakingiuka, Ipangala, Mlabani na Viwanja Sitini Wapiga Kura walioandikishwa ni 19,188 wakati makisio yalikuwa watu 17,790 na Mkoa wa Katavi Halmashauri ya Mlele kata za Ikuba, Usevya na Kibaoni Wapiga Kura 11,210 waliandikishwa wakati makisio yalikuwa watu 11,394. Matokeo haya yanadhihirisha kuwa vifaa vya uandikishaji vilifanya kazi vizuri
Kwa upande mwingine Jaji Lubuva amesema majaribio ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika majimbo matatu yaliyotajwa yameonesha mafanikio pamoja na changamoto mbalimbali.
Akizungumzia Changamoto amesema , changamoto kadhaa wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo zimoenekana ambazo ni Matatizo yaliyotokana na ’Settings’ za BVR Kits,baadhi ya ”BVR Kits” zilitumia camera iliyo katika Laptop badala ya camera iliyowekwa kwa ajili ya kupiga picha. Uchukuaji wa alama za vidole (Automatic Process settings) ilisababisha Mfumokusimama(Crash).
Changamoto nyingine ni tatizo la kuchukua picha iwapo viwango vya ICAO vya ubora wa Picha havijafikiwaMatatizo yaliyosababishwa na Software. Fingeprint Scanner kusababisha Mfumo wa Uandikishaji  kusimama (Crash) kutokana na SDK na za vifaa finger print scanner.

picha za diamond nchini rwanda

Tarehe December 30, 2014
Diamond, Zari na timu yake wakiwasili uwanja wa ndege nchini Rwanda
Diamond, Zari na timu yake wakiwasili uwanja wa ndege nchini Rwanda
Diamond na Zari walipowasili nchini Rwanda jana
Diamond na Zari walipowasili nchini Rwanda jana
Zari  na Diamond wakitoka nje ya uwanja wa ndege nchini Rwanda
Zari na Diamond wakitoka nje ya uwanja wa ndege nchini Rwanda
Diamond na Zari wakipokelewa kayika uwanja wa ndege nchini Rwanda
Diamond na Zari wakipokelewa kayika uwanja wa ndege nchini Rwanda
mon6
Waandishi wa habari nchini Rwanda wakiendelea na majukumu yao
Waandishi wa habari nchini Rwanda wakiendelea na majukumu yao
Diamond akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili nchini Rwanda jana
Diamond akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili nchini Rwanda jana
Waandishi wa habari nchini Rwanda wakifanya kazi yao wakati msafara wa Diamond ukiondoka katika uwanja wa ndege kuelekea hotelini
Waandishi wa habari nchini Rwanda wakifanya kazi yao wakati msafara wa Diamond ukiondoka katika uwanja wa ndege kuelekea hotelini
Diamond baada ya kuwasili katika Serena Hotel Rwanda alipofikia
Diamond baada ya kuwasili katika Serena Hotel Rwanda alipofikia
Diamond akiwa Serena Hotel baada ya kuwasili kutoka uwanja wa ndege
Diamond akiwa Serena Hotel baada ya kuwasili kutoka uwanja wa ndege
Mfalme wa muziki wa bongo flava nchini Tanzania aliyepo jijini Kigali Rwanda katika ziara yake ya Burudani, Diamond Platinumz amepokelewa kama mfalme alipowasili jijini humo akitokea nchini Burundi katika ziara yake iliyokamilika juzi kwa kufanya makamuzi ya nguvu kwa mashabiki wa nchini hapo.
Diamond anategemea kuuwasha moto kesho Desemba 31, 2014 katika mkesha wa kuukaribisha mwaka 2015 jijini Kigali, Rwanda katika ukumbi wa PSF/ EXPO Ground kwa kiingilio cha 10,000RWF ambapo onesho lake hilo maalumu limepewa jina la ‘The Vibe Party’.
Katika ziara hiyo Diamond ameongozana na kipenzi chake Zarinnah Hassan pamoja na timu yake nzima ya Wasafi Classic Baby (WCB) kwa ajili ya makamuzi.

Hiki ndicho alichokiandika msanii wa Hip Hop baada ya kutangaza kuacha muziki

Rapper aliyekua akiwakilisha kundi la Lunduno Nikki Mbishi ‘Baba Malcom’ leo ameingia kwenye headline baada ya kutangaza kuwa ameacha kazi ya muziki.
Taarifa hizo aliwahabarisha mashabiki wake kupitia ukurasa wa twitter na kuandika ‘I’m glad to say I’ve officially decided to quit music….Wishing all the best to the slaves and victims of Music industry. #2015
Hizi ni baadhi ya tweets za rapper huyo baada ya kutangaza kuacha kazi ya muziki 2015

Mkusanyiko wa zile Stori muhimu zilizoandikwa kwenye Magazeti ya leo Jan 2, 2015 Nimekuwekea hapa


HABARILEO
Mahakama ya Mkoa wa Tabora imemuhukumu Mwinjilisti wa kanisa la Menonite Ipuli kifungo cha miaka 30 kwa tuhuma za kumbaka msichana wa miaka 16.
Hakimu mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Tabora  Joctan Rushelwa alisema kifungo hicho kiwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo.
Alisema kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo hakukuwa na shaka yoyote ndio maana wameamua kutoa adhabu hiyo kwa mshtakiwa huyo.
Licha ya kutoa hukumu hiyo mshtakiwa hakuonyesha kuumizwa na adhabu hiyo hata baada ya kutakiwa kusema lolote na kusema atakata rufaa tu mara baada ya hukumu yake kutoka.
TANZANIA DAIMA
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema yeye ni mtu mwadilifu ambaye hajawahi kutoa wala kupokea rushwa kwa mtu katika maisha yake yote.
Pinda amesisitiza kwamba ana hakika kuwa hata siku moja hawezi kukamatwa kwa kosa la kupokea rushwa,isipokua kuna watu wanamchafua mara baada ya kutangaza nia yake ya kuvaa viatu vya Rais Kikwete.
Alisema kuwa wako baadhi ya watu walipanga kumchafua kwa kutaka kumsingizia wakati wa mkutano wa 16 na 17 Bungeni kwamba anahusika na uchotwaji wa fedha za Escrow.
“Nilishangaa sana watu ambao walitaka kunichafua kwa kunihusisha na fedha za Escrow,mimi sihusiki na wala sitahusika hata siku moja katika kupokea na kutoa rushwa mahali popote pale”alisisitiza Pinda.
NIPASHE
Mwanafunzi wa Darasa la pili katika shule ya msingi Ungindoni kata ya Mji mwema Dar es salaam anadaiwa kuchomwa moto na mama yake mkubwa sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kutumia jalo.
Mtoto huyo alifanyiwa ukatili huo siku ya krismasi akidaiwa kula vipande viwili vya nyama na hivyo kupewa adhabu na mama yake huyo kwa kuchomwa moto kwenye paja,mikono,magoti na miguu.
Mmoja wa shuhuda wa tukio hilo alisema  majirani walibaini kujeruhiwa kwa mtoto huyo mara baada ya kutoka nje na kuonekana akichechemea na alipoulizwa alisema amechomwa na na mama yake huku akionyesha maeneo alikofanyiwa ukatili huo.
Mama mkubwa Rachel alipoulizwa sababu ya kufanya hivyo alisema alichukua uamuzi huo baada ya kubaini alikula mboga na alipoulizwa alikana.
“Nakiri nimekosea kumpiga lakini mara kwa mara nimekua nikimuonya aache tabia ya wizi lakini amekua hasikii”alisema Rachel.
NIPASHE
Askofu msaidizi wa kanisa jimbo kuu Dar es salaam Eusebius Nzigilwa amevunja ukimya kuhusu mgao wa sh.milioni 40.4 alioupata kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya VIP Engineering& Marketing limited James Rugemalira.
Ukimya wa askofu Nzigilwa unatokana na sakata la uchotwaji wa zaidi ya bilioni 300 kutoka katika akaunti ya Tegeta Escrow iliyokua katika benki kuu ya Tanzania BoT.
Alisema kiutaratibu siyo vibaya waumini kutoa michango na matoleo kwa kanisa na watumishi wake.
Alisema aliombwa akaunti yake na Rugemarila mwanzoni mwa mwezi Februari na kwamba hakuwahi kufahamu kiasi cha fedha kilichowekwa kwenye akaunti yake hadi alipoangalia taarifa ya benki Februari 27 iliyoonyesha aliingiziwa milioni 40.4.
“Niliwasiliana na Rugemarila na kumwambia nimeona kiasi kikubwa cha fedha katika akaunti yangu,naye akaniambia hayo ni matoleo yake ambayo anaamini yatasaidia katika shughuli za kitume na kiuchungaji,,nikamshukuru kwa ukarimu huo mkubwa”alisema askofu huyo.
MTANZANIA
Siku chache baada ya kutangaza nia ya kugombea Urais katika uchaguzi mkuu,Waziri wa Nishati na Madini Lazaro Nyalandu ameadhimisha sherehe za kuuaga mwaka katika kanisa la Efatha huku mchungaji wa kanisa hilo Josephat Mwingira,akimtabiria ushindi wa safari aliyoianza.
Mwingira alisema neno hilo ni la kinabii na kusisitiza hakuna wa kumzuia kwa kuwa ukuu umeariwa juu yake.
Mwingira ambaye alisema neno hilo linatoka kwa bwana,alisisitiza kuwa vikwazo juu ya Nyalandu havitakuwepo tena.
“Hakuna atakayekuzuia tena,ni wakati wa wana wa Mungu kuinuka,hakuna atakayekukandamiza tena,mimi baba yako nitatangulia mbele yako niseme kitu,neno hili la kinabii litasababisha yale yaliyokua mbali yawe karibu na yaliyokua hayawezekani yatawezekana”alisema Nabii huyo.
MWANANCHI
Simba wanne waliotoka nje ya hifadhi ya Taifa ya Tarangire na kuingia eneo la kijiji cha Kibaoni, Manyara wameuawa kwa kuchomwa mikuki na wananchi.
Kijiji hicho kipo hatua chache kutoka ndani ya hifadhi hiyo ambayo ni mojawapo ya vivutio vya utalii wa Tanzania na mara nyingi wayamapori huzagaa mitaani hasa kipindi cha masika kuepuka majani marefu hifadhini.
Tukio hilo ambalo lilielezwa kuwa ni janga kubwa katika sekta ya utalii nchini,lilitokea jana alfajiri hadi saa 6 mchana na mizoga saba ya Simba ilipatikana  huku mmoja akiaminika kufia kwenye vichaka baada ya kukimbia alipojeruhiwa.
Waziri wa Maliasili Lazaro Nyalandu ameziagiza mamlaka zinazohusika kuwasaka na kuwatia mbaroni wahusika kuwaongoza wanakijiji hao kuua Simba hao kinyume na utaratibu.
MWANANCHI
Wakati Watanzania wengi wakiwa na matumaini ya utawala bora kwa mwaka 2015,ripoti mpya ya utafiti wa hali ya rushwa inaonyesha vitendo vya rushwa vitaendelea au kupungua ikilinganishwa na mwaka jana.
Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa na asasi ya ConcernFor Development Initiatives in Afrika ForDIA kwa kushirikiana na mtandao wa Uwazi TRAFO wananchi wanane kati ya kumi wanaamini hali ya rushwa iliongezeka mwaka jana.
Pamoja na vitendo hivyo kuendelea kuathiri maisha na upatikanaji wa huduma za jamii nchini,Watanzania tisa kati ya 100 waliripoti Takururu au Polisi hali ambayo ilitokana na wengi kutokua na imani na mamlaka hizo.
Vitendo hivyo vimeifanya Tanzania kushika nafasi ya pili katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya Burundi huku viashiria vya uwezekano wa kutokea rushwa navyo vikipanda.