Thursday, December 18, 2014

Kenya ya vioja… Pale ambapo wanawake wanaojiuza wanahitaji kutambuliwa na Serikali(Video & story)


Kundi la wanawake wanaofanya biashara ya kujiuza nchini Kenya limefanya maandamano kuadhimisha siku ya makahaba duniani jana December 17, lengo lake ni kukomesha dhuluma dhidi yao.
Wanawake hao waliandamana ofisi ya Jaji Mkuu Willy Mutunga wakitaka Serikali kuwapa nafasi ya kuwatambua rasmi na wawe walipa kodi halali kama ilivyo kwa wafanyabishara wengine.

Waandamanaji hao wameishutumu Serikali kwa kuruhusu ukiukwaji wa haki zao za kibinadamu kwa kutokana na kesi ambazo huwa zinawahusu kutochukuliwa hatua za kisheria.

Kura za Wabunge zimefanya mabadiliko haya ndani ya Bunge la Afrika Mashariki…

Bunge la Afrika Mashariki limemfuta kazi aliyekuwa Spika wake Margaret Nantongo Zziwa ambapo uamuzi huo umetokana na malalamiko ya kutumia vibaya ofisi yake kama Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).
Maamuzi hayo yamefikiwa leo (17-12-2014) katika makao makuu ya Bunge hilo  Arusha, ambapo Zziwa aliwahi kulalamikiwa na baadhi ya Wabunge kwamba anatumia vibaya ofisi yake, amekuwa kitoa huduma isiyokidhi pamoja na ukosefu wa heshima kwa Wabunge hivyo wawakilishi 45 kukubaliana kuhusu kufukuzwa kwake kwa kupiga kura, ambapo jumla ya Wabunge waliokuwepo walikuwa 39, kura za ndiyo zilikuwa 36 huku mbili zikisema hapana na nyingine moja kuharibika.

Umesoma makubwa yaliyoandikwa na Magazeti ya Tanzania leo December 18? Yako hapa

prince blog inakupa vichwa vya habari vya magazeti yote ya kila siku. Leo pia kuna headlines mpya kwenye magazeti mbalimbali. Chukua muda wako kupitia kila kilichoandikwa kwenye kurasa za mbele za magazeti ya leo.






































Wednesday, December 17, 2014

Ile ahadi ya Waziri Hawa Ghasia ameanza kuitekeleza, Wakurugenzi hawa wamesimamisha kazi

Siku chache baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Hawa Ghasia kuahidi kumuwajibisha yoyote aliyehusika na kuvuruga uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika tarehe 14, leo Waziri huyo ametangaza majina ya Wakurugenzi watano waliosimamishwa kazi na wengine sita waliopewa onyo kutokana na uchunguzi kuonyesha wameshindwa kutekeleza wajibu wao.
Majina ya Wakurugenzi waliotajwa kusimamishwa ni haya; Felix Mabula (Halmashauri ya Hanang), Fortunatus Fwema (Halmashauri ya Mbulu),  Isabella Chilumba(Halmashauri ya Ulanga),  Pendo Malabeja (Halmashauri ya Kwimba) na William Shimwela (Halmashauri yaSumbawanga).
…Ni dhahiri kuwa Wakurugenzi wa kwenye zile Halmashauri zenye dosari wameonyesha udhaifu mkubwa sana wa kutekeleza majukumu yao ikiwemo jukumu la msingi la kusimamia uchaguzi ambao ni moja ya majukumu ya Wakurugenzi. Kasoro hizo zilisababisha kurudiwa kwa uchaguzi katika baadhi ya maeneo yao… Wakurugenzi hao wametenda makosa yafuatayo ambayo yanawaondolea sifa ya kuwa wakurugenzi katika halmashauri…“– Hawa Ghasia.
… Kwanza ni kuchelewa kuandaa vifaa vya kupigia kura, kukosa, umakini katika kuandaa vifaa vya kupigia kura na hivyo kuchanganya majina pamoja na vyama, kuchelewa kupeleka vifaa kwenye maeneo ya kupigia kura, uzembe katika kutekeleza majukumu yao na kutoa taarifa za kupotosha kuhusu maandalizi ya uchaguzi.. kwa sababu walituhakikishia kwamba maandalizi yamekamilika huku wakifahamu kwamba suala hilo sio kweli…“– Hawa Ghasia.

aisha madinda amefariki dunia

Taarifa ambayo imetolewa kupitia Clouds FM December 17 2014 mchana ni kuhusu kifo cha aliyekua Mmnenguaji maarufu kwenye familia ya muziki wa dansi Tanzania Aisha Mohamed Mbegu maarufu kama ‘Aisha Madinda’.Chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika lakini taarifa za mwanzo zinasema alipelekwa hospitali ya Mwananyamala akiwa tayari amefarik ambapo taarifa zaidi zitazidi kukufikia kupitia princeroberthamisi.blogspot.com baadae.

Zile Stori zilizopewa nafasi kwenye Magazeti ya leo Tanzania December 17 nimekuwekea hapa mtu wangu



MTANZANIA
Matumizi ya shirika la Maendeleo ya Mafuta Tanzaniua TPDC ambayo pamoja na mambo mengine yameinisha mishahara inayotaka iidhinishiwe na Mamlaka ya udhibiti wa huduma za maji na nishati EWURA ili ianze kutumika Januari mwakani,imebainika ni kufuru.
Kwa mujibu wa Baraza la Uashauri la Watumiaji wa  wa huduma zinazodhibitiwa na EWURA,mishara ambayo TPDC inataka EWURA iipitishe  ili iweze kutumika mwakani ni shilingi milioni 36 kwa Mkurugenzi wa Shirika hilo.
Maofisa wengine walioombewa mishahara ni mkurugenzi na makamu wa vitengo milioni 28,maofisa waandamizi milioni 16.2,wahasibu,maofosa rasilimali watu,ofisa masoko,ugavi milioni 12.6,wahudumu,madereva na makatibu Muhtasi milioni 5.4.
“Mishahara inayopendekezwa ni mikubwa,utetezi wa TPDC kuwa viwango vya mishahara ni kwa mujibu wa soko la ajira katika sekta za mafuta mna gesi haujitoshelezi kwa sababu hauelezei soko hilo ni kwa nchi zipi”inasema sehemu ya nyaraka hiyo.
Msemaji wa Ewura Stella Lupimo alikiri nyaraka hiyo ni ya Baraza hilo na alisema mapendekezo hayo yaliwasilishwa kwenye mkutano wa taftishi wa kujadili mapendekezo ya TPDC uliofanyika November 27 mwaka huu.
MTANZANIA
Klabu ya Yanga imemsainisha Mshambuliaji wa kimataifa Hamis Tambwe mkataba wa mwaka mmoja kwa dau la kiasi cha dola 20,000 za kimarekani sawa na milioni 34.3 za kitanzania.
Imeelezwa kuwa Yanga iliahidi kumlipa mshahara wa dola 2,000 kwa mwezi pamoja na kumpa nyumba ya kuishi maeneo ya Sinza jijini Dar es salaam,mshahara ambao ni mara mbili wa ule aliokua akilipwa Simba wa milioni 1.3.
Usajili wa Tambwe ambao ni raia wa Burundi aliachwa na Simba kwa madai ya kushuka kiwango chake amewashanga wengi kutokana na mashabiki wengi wa Simba kumkubali baada ya kuibuka mfungaji bora wa ligi kuu Tanzania bara msimu uliopita.
Chanzo cha uhakika kilisema Simba imekubali kumlipa mshambuliaji huyo dola 6,000 kama stahiki zake baada ya kuvunja mkataba wake kama ilivyofanya kwa kiungo Pierre Kwizera ambaye nae ni raia wa Burundi ambaye hakupata mafanikio yoyote tangu asajiliwe kwenye timu hiyo.
NIPASHE
Baada ya kufanya vibaya katika uchaguzi wa Serikali za mitaa,vitongoji na vijiji Mkoani Shinyanga baadhi ya wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM wamefikia hatua ya kurushiana matusi na kuvuana nguo hadharani.
Katibu wa siasa na uenezi wa Chama hicho Wilayani Shinyanga Charles Shigino alisema baada ya CCM kufanya vibaya katika kata ya Ngokolo na Chadema kuchukua mitaa sita kati ya saba,wanachama wameanza kumtuhumu kwa kusababisha matokeo mabaya.
Wakati akiingia ofisini alikutana na Katibu wa jumuiya ya vijana UVCCM Zawadi Nyambo na kumzuia kuingia ofisini huku akimrushia maneno ya matusi hali iliyosababisha mtafaruku mkubwa na kujaza watu.
Alisema baada ya kushindwa kuvumilia matusi hayo aliamua kukabiliana nae huku watu wakiingia hali iliyosababisjha nguo kumvuka na kubaki mtupu.
MWANANCHI
Mwenyekiti mwenza wa Umoja wa katiba ya wananchi Ukawa Freeman Mbowe amesema Umoja huo utafanya tathimni ya maeneo ambayo wangeweza kushinda na kusimamisha mgombea mmoja kila eneo ili kuwachukulia hatua wale wote waliokiuka makubaliano yao.
Wenyeviti wa Umoja huo walisaini makubaliano kadhaa yakiwemo ya kusimamisha mgombea mmoja atakayeungwa mkono na Ukawa katika chaguzi zote kuanzia Serikali za mitaa hadi uchaguzi mkuu ujao.
Hata hivyo katika uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika jumapili,baadhi ya maeneo kila chama kilisimamisha mgombea wake na matokeo yake kuipa CCM kushinda kwa urahisi.
Mbowe alisema viongozi wote kutoka vyama hivyo walihusika kukiuka makubaliano hayo na watawachukulia hatua za kinidhamu na tathmini itakayofanyika ndani ya umoja huo itakua nafasi muhimu ya kujipanga kufanikiwa katika uchaguzi mkuu ujao.
MWANANCHI
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imewataka wamiliki wa vyombo vya moto visivyotumika kufuta usajili wake ili kuiwezesha Serikali kuwa na kumbukumbu sahihi ya vyombo vya moto vinavyofanya kazi.
Akizungumza jana na Gazeti hili Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipakodi Richard Kayombo alisema lengo la agizo hilo ni kuondoa kumbukumbu za malipo kwa vyombo wasivyotumia.
“Uamuazi huu tunaufanya ili kuwasaidia wamiliki wa vyombo hivyo kuondokana na usumbufu kwani tusipofanya hivyo TRA itaendelea kuweka kumbukumbu ya kodi zake”alisema Kayombo.
Alisema mmliki anayetaka kufuta usajili wa chombo chake atalazimika kwenda Polisi na kupewa cheti kutoka polisi makao makuu ya Usalama Barabarani.
MWANANCHI
Watoto wa Watanzania waliokua wameungana kifua ambao walikua wakitumia maini na mapafu yaliyounganika,mvungu mmoja wa moyo na mmeng’enyo wa chakula wamefanyiwa upasuaji na kutenganishwa huko India.
Pacha hao wa kile Abriana na Adriana wenye umri wa miezi minne walifanyiwa upasuaji huo November 17 katika Hospitali ya Apollo.
Daktari aliyesimamia upasuaji huo Ks Sivakumar alisema upasuaji huo ulichukua zaidi ya saa 20 na walilazimika kutumia muda huo kutokana na jinsi pacha hao walivyokua wameungana na haikua kazi ndogo kuwarudisha kwenye hali yao ya kawaida.
“Huu ni upasuaji wa kwanza na wa aina hii kufanikiwa kwani wengi tuliokua tukiwafanyia walikua wakipoteza maisha,hivyo tunajivunia kwa hili,jumla ya madaktari 50 waliobobea katika taaluma mbalimbali tulifanikiwa kufanya upasuaji huu kutokana na kuwa ni mkubwa”alisema SivaKumar.
TANZANIA DAIMA
Mwananchi wa Chama cha Mapinduzi CUF Ibrahim Lipumba amesema Waziri mkuu Mizengo Pinda ni mzigo usiobebeka  katika Serikali ya Rais Kikwete na hafai kuwa rais kwani ameshindwa katika kila jambo analosimamia.
Kutokana na hali hiyo amemtaka Rais Kikwete aachane na Pinda kwani atamsababisha kumaliza muda wake wa urais vibaya.
Alisema uchaguzi wa Serikali za mitaa uliokua katika  chini ya ofisi ya Waziri mkuu umekua sehemu nyingine ya matumizi mabaya ya fedha za Serikali huku wakijua kuwa Serikali haipo tayari kuona mabadiliko kupitia masanduku ya kura.
“Pinda na Ghasia waachia madaraka,wameshindwa kusimamia uchaguzi huu,wameruhusu Wakurugenzi kuwa sehemu ya watatufa mafanikio ya CCM badala ya kusimamia majukumu ya wananchi,kuchagua viongozi wanaowataka,hili linamuharibia rais Kikwete zaidi na anaweza asimalize muda wake akiwa na chembe ya usafi”alisema Lipumba.
Alisema waziri Mkuu amekua na mambo mengi yasiyoeleweka na ameshindwa kusimamia misingi ya kiuongozi na kwamba hali hiyo inatoa unafuu kwa wapinzani kushinda chama tawala iwapo CCM itampitisha kuwa mgombea wao.

Nitagombea Urais Marekani:Jeb Bush

                                            Jeb Bush
  
Gavana wa zamani wa jimbo la Florida nchini Marekani Jeb Bush amesema anataka kujitosa katika kinyang’anyiro cha Uraia wa Marekani uchaguzi mkuu wa 2016.
Jeb mwenye umri wa miaka 61 ambaye pia ni mtoto wa rais wa zamani,lakini pia ni mdogo wa rais George W Bush.
Akizungumza kupitia mitandao ya kijamii Jeb amesema kuwa anaangalia uwezekano ili kujitosa katika mtifuano wa kusaka urais 2016.
Msemaji wake amesema kuwa maamuzi yoyote ni hapo mwaka kesho ambapo anatarajiwa kuweka peupe nia yake
Jeb Bush alikuwa Gavana wa jimbo la Florida kuaniza miaka 1999.
Baadhi ya wachunguzi wa mamabo wanasema Urais kwa Jeb inaweza kuwa ni nia njema ama ikawa mgogoro kwake.              

Haiti waandamana kumng'oa Rais wao

Mamia ya raia wa nchini Haiti wameandamana katika mitaa ya Port-au-Prince wakishinikiza Rais Michel Martelly kuondoka madarakani.
Rais wa Hait mICHAEL Martelly
Hata hivyo maandamano hayo yamegeuka vurugu baada polisi kutumia mabomu ya mchozi kuwatawanya waandamanaji hao. polisi wamepambana na waaandamanaji hao ambao wamekuwa wakirusha mawe na kuchoma moto matairi mitaani.
Madai ya raia hao ni kumtaka Rais Martelly kuitisha uchaguzi na kuunda serikali,ambapo uchaguzi ulitakiwa kuitishwa miaka mitatu iliyopita.
Waziri mkuu wa Haiti Laurent Lamothe, siku ya jumapili aliamua kuachia ngazi baada ya shinikizo la siku mbili.Maoni kutoka vyama vya upinzani ni kwamba wanamtaka rais Martelly kujiuzulu. Awali Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry ameitaka Hait kuitisha uchaguzi mara moja

MWANANSHERIA MKUU AMEJIUZULU



aliyekua mwanasheria mkuu wa serikali jaji werema.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia jana, Jumanne, kufuatia sakata la uchotaji wa fedha kutoka akaunti ya ESCROW ambapo zaidi ya dola milioni 120 zilihamishwa.
Mwanasheria mkuu, pamoja na baadhi ya wanasiasa na maafisa waandamizi wa serikali walituhumiwa kuhusika kwa namna moja au nyingine kufanikisha kufanyika kwa miamala haramu ya fedha za Akaunti ya Escrow ya Tegeta.
Leonard Mubali ameandaa taarifa ifuatayo:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Dar es Salaam, imesema Rais Jakaya Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu kwa Mwanasheria Mkuu huyo wa Serikali.
Katika barua yake kwa Rais Kikwete, Jaji Werema amesema ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow haukueleweka na umechafua hali ya hewa. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.Sakata la Akaunti ya Escrow liliibuliwa bungeni na mmoja wa wabunge wa bunge la Tanzania, David Kafulila na kusababisha mjadala mkali na kuamua Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kupewa jukumu la kuchunguza kashfa hiyo.Baada ya uchunguzi kuwasilishwa katika mkutano wa bunge uliomalizika mwishoni mwa mwezi Novemba, kamati hiyo ilikuja na maazimio manane kuhusu taarifa ya ukaguzi maalum kuhusiana na miamala iliyofanyika katika akaunti ya Escrow ya Tegeta pamoja na umiliki wa kampuni ya IPTL.
Miongoni mwa maazimio ya bunge yaliwataja baadhi ya wanasiasa, mwanasheria mkuu, maafisa waandamizi wa serikali, majaji, wakuu wa taasisi za umma, viongozi wa dini, mawakili wa kujitegemea na watu binafsi kuhusika katika kashfa hii na hivyo kuagiza mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua za kisheria wahusika na wengine kuondolewa katika nyadhifa zao za kuteuliwa.Kamati hiyo ya Bunge pia ilipendekeza kuwa waziri wa Nishati na Madini, waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, mwanasheria mkuu, katibu mkuu wa wizara ya Nishati na Madini na wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa Tanesco wawajibishwe kwa kuishauri mamlaka ya uteuzi kutengua uteuzi wao.
Pia maazimio ya Kamati ya kudumu ya bunge ilipendekeza kuwa, kwa miaka mingi mikataba mibovu ya kuzalisha umeme kati ya Tanesco na makampuni binafsi imeisababishia Tanesco hasara ya mabilioni ya fedha na kutishia uhai wake wa kifedha, serikali iwasilishe mikataba husika bungeni au kwenye kamati zake kwa lengo la kutekeleza vema wajibu wake wa kuimamia na kuishauri serikali.
Akaunti ya Escrow ilianzishwa katika Benki Kuu ya Tanzania ili kuhifadhi fedha, baada ya kuibuka kwa mvutano kati ya Shirika la Umeme la Tanzania, Tanesco na kampuni ya kufua umeme ya IPTL kuhusu ongezeko la mtaji wa uwekezaji, huku TANESCO ikilalamika kuwa gharama za kununua umeme kutoka kampuni ya IPTL zilikuwa za juu mno. Fedha hizo zingeendelea kutunzwa katika Akaunti hayo hadi wakati ambapo suluhisho la mvutano wa wabia hao wawili lingepatikana.

BARUA AMBAYO INADAIWA KATIBU MKUU WA NISHATI NA MADINI ALILAZIMISHWA KUANDIKA NA MWANASHERIA MKUU WEREMA ILI KUCHOTA PESA HUKO ESCROW



chanzo;
http://www.theguardian.com/global-development/2014/oct/13/uk-and-international-donors-suspend-tanzania-aid-after-corruption-claims

Kurasa za mwanzo na mwisho Magazetini leo December 17, 2014