Saturday, January 24, 2015

Freeman Mbowe atoa gari ya wagonjwa Hai


 Mbunge wa Jimbo la HAI,,na Kiongozi wa kambi RAsmi bungeni MH FREEMAN MBOWE ameendeleza juhudi zake katika kuokoa maisha wa watu wa jimbo lake ambapo wiki hii ametoa gari la wagonjwa kwa ajili ya watu wa jimbo lake.
Kutolewa kwa gari hilo itakuwa ni ukombozi mkubwa kwa wakazi wa Hai jimbo ambalo lina   mito na mabonde  ambayo huleta adha  kwa wakazi wa maeneo hayo na kushindwa kuwawaisha wagonjwa hospitali za teule ya Machame na ile ya Wilaya.
Kufuatia kutolewa kwa gari hilo la wagonjwa  mkazi mmoja wa kata ya Lyamungo Kati amesema itakuwa ni msaada mkubwa sana kwao maana itarahisisha kupeleka wagonjwa kutoka Kituo cha afya Lyamungo Hadi hospitali teule ya Machame. 

Mabibi na Mabwana,Yamoto Band wanakualika kutazama video yao mpya #Nitakupwelepweta



Ntakupelepetwa





Style
ya muziki wanaoufanya imewafanya kupanda mashabiki wa umri
tofauti,Yamoto Band wametuletea video yao mpya hii inaitwa
Nitakupwelepweta,imeongozwa na Adam Juma.


Bonyeza play kutazama


















Kuhusu mabadiliko ndani ya Baraza la Mawaziri TANZANIA, hapa kuna ya wote walioteuliwa


Leo huenda ikawa moja ya siku ambayo itaingia kuwa siku yenye headlines kubwa kwenye siasa TANZANIA, wakati wa mchana kulikuwa na taarifa kutoka Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini, Dar es Salaam ambapo aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo alifanya kikao na waandishi wa Habari na kutangaza kujiuzulu.
Kubwa nyingine kwenye upande huo huo ni ishu ya Rais Kikwete kutangaza mabadiliko madogo ndani ya Baraza la Mawaziri, ambapo mabadiliko hayo nimekuwekea hapa, wapo waliohamishwa na wapo waliokuwa Manaibu Mawaziri sasa ni Mawaziri, list yote ni hii hapa;
Mawaziri
George Simbachawene – Waziri wa Nishati na Madini
Mary Nagu- Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais- Mahusiano na Uratibu
Christopher Chiza- Waziri Uwezeshaji na Uwekezaji
Harrison Mwakyembe- Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
William Lukuvi- Waziri wa Ardhu, Nyumba na Makazi
Steven Wasira- Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
Samuel Sitta- Waziri wa Uchukuzi
Jenista Muhagama- Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge
Manaibu Waziri
Stephen Masele- Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu Rais- Muungano
Angela Kairuki- Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi
Ummy Mwalimu- Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
Anna Kilango- Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Charles Mwaijage- Naibu Waziri wa Nishati na Madini

Rais Kikwete awateua mawaziri 8 Tanzania

Rais Jakaya Kikwete

Rais Jakaya kikwete wa Tanzania ametangaza mabadiliko katika baraza lake la mawaziri.
Rais amewateua mawaziri wanane wapya pamoja na manaibu watano.
Tangazo hilo lilifanywa na katibu katika ikulu ya rais balozi Ombeni Sefue.
Mabadiliko hayo yanajumuisha wadhfa wa waziri wa nishati na kawi wa Profesa Muhongo ambaye amejiuzulu mapema leo pamoja na wadhfa wa waziri wa ardhi ambao uliwachwa wazi baada ya kupigwa kalamu kwa Anna Tibaijuka.
Mawaziri hao wawili wanahusishwa na kashfa ya ufisadi ambayo ilimshinikiza mwanasheria mkuu pia kujiuzulu.Nafasi ya Profesa Muhongo imechukuliwa na aliyekuwa naibu wa waziri wa ardhi, George Simbachawene
Rais Kikwete amewaapisha mawaziri hao wapya hii leo katika tangazo lililorushwa hewani na runinga ya taifa moja kwa moja.

MSF:Sudan ilishambulia hospitali

Jeshi la Omar el Bashir ladaiwa kushambulia hospitali kusini mwa Kordofan

Jeshi la Omar el Bashir ladaiwa kushambulia hospitali kusini mwa Kordofan Shirika la madaktari wasio na mipaka Medecine Sans Frontieres limeilaumu Sudan kwa kushambulia moja ya hospitali katika jimbo la Kordofan Kusini ambapo wanajeshi wa serikali wanapigana na waasi. Shirila hilo linasema kuwa jeshi la wanahewa la Sudan lilidondosha mabomu 13 ndani na nje ya hospitali hiyo kwenye milima ya Nuban ambapo watu wawili walijeruhiwa. Serikali ya Sudan awali imekana kuwalenga raia katika kampeni yake dhidi ya waasi

Friday, January 23, 2015

Ukweli kuhusu ishu ya Wema Sepetu kumshitaki Diamond Polisi

Wema 1January 21 na 22 2015 zilitoka stori kwenye mitandao na kwenye gazeti kwamba mwigizaji Wema Sepetu kamshitaki Polisi mpenzi wake wa zamani Diamond Platnumz akitaka alipwe pesa zake alizomkopesha.


Upande wa Wema Sepetu umeongea ukweli wa kila kitu kwenye hii video hapa chini.