Showing posts with label princeroberthamisi. Show all posts
Showing posts with label princeroberthamisi. Show all posts

Wednesday, January 7, 2015

Utata wajitokeza kifo cha Meshack Yebei

robert
William Ruto
hali tata imezidi kujitokeza juu ya kifo cha Meshack Yebei, anayetajwa kuwa shahidi katika kesi inayomkabili Naibu Rais wa Kenya William Ruto.Shahidi huyo alitarajiwa kutoa ushahidi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC dhidi ya naibu Rais wa Kenya.Lakini mwishoni mwa wiki mwili wa Yebei ambao ulionekana kuunguzwa kiasi ,ulikutwa umetupwa kando ya mto huko Eldoret Magharibi mwa nchi hiyo.Familia ya Yebei wanashuku kwamba chanzo cha mauaji hayo ilikuwa ni kumzuia ndugu yao asiweze kutoa ushahidi wake katika mahakama ya ICC huko The Hague.Hata hivyo msemaji wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita, ICC Fadi El Abdallah ameiambia BBC kuwa Bwana Yebei hakuwa katika orodha ya mashahidi rasmi wa upande wa mashitaka katika mahakama ya ICC.Amesema, kuna makundi tofauti ya watu wanaoweza kupewa ulinzi na mahakama ya ICC, ambao ni pamoja na makundi tofauti ya mashahidi wawe ni wale wa upande wa mashitaka, utetezi na majaji au wawakilishi wa waathirika na zaidi ya hapo ICC inaweza kutoa ulinzi kwa watu wengine binafsi au kwa sababu ya kuwa na uhusiano na ICC lakini bila kuwa mashahidi rasmi. "Na katika hatua hii kile tunachoweza kueleza ni kuwa Bwana Yebei hakuwa katika orodha ya mashahidi wa ICC upande wa mashitaka kinyume na kilichoripotiwa katika badhi ya vyombo vya habari.Lakini kwa minajiri ya uchunguzi hatuwezi kueleza yeye yuko katika kundi gani la watu wanaolindwa na ICC" amesema Bwana Fadi.Mwendesha mashitaka mkuu wa ICC, Fatou Bensouda amewahi kunukuliwa akisema kuwa mashahidi kadha mpaka sasa wamekuwa wakitishiwa maisha na matokeo yake wengi wamejitoa katika ushahidi wa kesi hiyo iliyokuwa ikiwakabili viongozi kadha wa taifa la Kenya akiwemo Rais Uhuru Kenyatta ambaye hivi karibuni amefutiwa mashitaka na mwendesha mashitaka mkuu huyo wa ICC,kwa kile alichoeleza kuwa ni kukosekana kwa ushahidi ambao ungetosheleza kuendelea na kesi hiyo, baada ya mashahidi wengi kujitoa au kudaiwa kuuawa na hata kukosa vielelezo vingine ambavyo angevitumia kama ushahidi katika kesi hiyo.Awali aliyekuwa mwendesha mashitaka mkuu wa ICC, Louis Ocampo aliwafungulia kesi watu sita, ambao alisema ni wahusika wakuu katika kesi ya ghasia za baada ya uchaguzi mkuu nchini Kenya 2007.Watuhumiwa hao walikuwa ni pamoja na Uhuru Kenyatta, ambaye wakati huo alikuwa naibu waziri mkuu na waziri wa fedha, Francis Kirimi Muthaura, aliyekuwa katibu wa baraza la mawaziri,na Mohammed Hussein Ali, mkuu wa polisi wa zamani. Wengine ni Henry Kosgey, aliyekuwa waziri wa viwanda,William Ruto, aliyekuwa waziri wa elimu na baadaye kusimamishwa na Joshua Arap Sang, mtangazaji wa redio moja nchini Kenya.Naibu Rais William Ruto na mtangazaji wa redio Joshua Arap Sang ndio waliobakia katika kesi hiyo ya ghasia za baada ya uchaguzi mkuu nchini Kenya ambapo watu wapatao 1,200 waliuawa na wengine 500, 000 kukosa

Tuesday, January 6, 2015

Binti wa miaka 12 kutoka Nigeria kwenye rekodi kubwa za Kimataifa…

ZuUnapokuwa karibu na mtoto wako na kumfuatilia ni rahisi kujua kipaji chake na kukiendeleza ingawa ni wazazi wachache wanaoweza kufanya hivyo, msichana kutoka Nigeria ambaye anasoma Marekani anakuwa msichana mdogo aliyeweza kuvunja rekodi kadhaa kubwa duniani.
Zuriel Oduwole, umri wake ni miaka 12, ameweka historia nyingine baada ya documentary yake ya ‘A Promising Africa’ kuwa documentary ya binti mdogo zaidi duniani kuonyeshwa katika majumba makubwa ya cinema.
Jarida la Forbes lilimtaja kuwa msichana mdogo mwenye asili ya Afrika ambaye ni miongoni mwa watu 100 mashuhuri wenye ushawishi zaidi Afrika waliotajwa kwa mwaka 2013 wakiwemo Marais watatu, pia akawa na rekodi ya kuwa mtu mdogo zaidi dunia kuandikwa historia yake katika Jarida la Forbes.
Documentary hiyo itaonyeshwa London, Januari mwaka huu na baadaye itaanza kuuzwa.
zuriel-and-kunle-afolayan-450x600

Dar es Salaam jiji ghali kuishi

Wakazi wa Dar es Salaam hutumia gharama kubwa kufanya manunuzi
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam hutumia gharama kubwa zaidi, kulipia mahitaji yao ya muhimu kuliko wenzao wengine wa Afrika mashariki, jijini Nairobi na Kampala,utafiti uliofanywa na Shirika linalotathimini gharama za maisha,Numbeo umeeleza. Utafiti huu ulifanywa ukihusisha miji mikubwa 22 ukiangalia uwezo wa kununua bidhaa,biashara za migahawani, hali kadhalika utafiti huu ulijikita kwenye gharama za juu na urahisi wa maisha ya mijini Kwa mujibu wa Ripoti ya Numbeo , takwimu za gharama za watumiaji kwa wakazi wa Dar es Salaam kwenye bidhaa na huduma mbalimbali ni asilimia 62.83 ambayo imezidi Kampala na Nairobi zenye asilimia 54.34. Kwa sasa Kenya ni nchi inayoongoza kwa kuwa na uchumi mkubwa Afrika Mashariki na iko nafasi ya sita barani Afrika, hata hivyo kwa mujibu wa matazamio ya Benki ya Standard Charterd , Tanzania inaelekea kuipiku Kenya na kuwa nchi yenye uchumi mkubwa ifikapo mwaka 2030 iwapo pato la taifa halitabadilika.

Sitti Mtemvu na Wema Sepetu

wema sepetu 2006
Wema Sepetu alipovalishwa Taji la Miss Tanzania 2006.
Soudy Brown leo katuletea U Heard inayowahusu Wema Sepetu na Sitti Mtemvu ambao waliwahi kuvaa Taji la Miss Tanzania kwa nyakati tofauti.
Soudy amewalinganisha Wema na Sitti kwamba, wakati ambao Wema alishinda Taji hilo kulikuwa na story kwamba ameongopa umri kwa kujiongeza miaka miwili huku Sittikukiwa na story ya kupunguza umri miaka miwili pia story ya kwamba wote walikuwa wanene.
IMG_6871
Sitti Mtemvu baada ya kuvishwa Taji la Miss Tanzania 2014.
Kuhusiana na Sitti kujivua Taji, Wema amesema kama ingekuwa ni yeye asingevua taji kutokana na mambo ambayo yalikuwa yakizungumzwa mitandaoni baada ya kuvishwa Taji hilo.

MAFUNZO YA UFUGAJI KUKU WA ASILI YAFANYIKA MJINI PANGANI

Mkuu wa Wilaya ya Pangani,MkoaniTanga Bi. Hafsa Mtasiwa akifungua mafunzo ya ufugaji kuku wa asili yaliyofanyika mjini Pangani. Mafunzo hayo yaliendeshwa na Taasisi ya Twende Pamoja Foundation ikishirikiana na Radio ya Pangani FM.

Microsoft na ujio wa #Nokia215… Hii inakaa na chaji mwezi mmoja!

Nokia-215
Simu za Nokia ni moja ya simu ambazo zimekuwa na umaarufu mkubwa Duniani, mbali na hiyo hii ni moja ya Kampuni kongwe zaidi kwenye soko la bidhaa hizo.
Kuna wakati ambao umaarufu wa bidhaa za Nokia ulishuka, lakini unaambiwa kwa sasa wanakuja hivi; Nokia wametengeneza simu za Nokia 215, zitakuwa za line moja na line mbili.
Nokia
Simu aina hii ina uwezo mkubwa wa kukaa na chaji mpaka mwezi mmoja kwa ile ya line moja, ya line mbili ina uwezo wa kukaa na chaji kwa siku 21, zina internet na mtumiaji ataweza kutumia FacebookTwitter ambazo zimeungwa moja kwa moja tofauti na ilivyo kwa smartphone.
Wanakadilia kwamba zikiingia sokoni bei yake itakuwa ni dola 29, ambayo ni sawa na sh. elfu 50 kwa T’zania.
Microsoft wamepanga kuiuza simu hii Afrika, Asia, Ulaya, na Mashariki ya Kati japo hawajasema lini itakuwa sokoni.
Hii ni moja ya hatua kubwa ambazo Nokia imezipiga sokoni tangu Kampuni hiyo inunuliwe na Microsoft.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AFANYA ZIARA KATIKA MKOA WA SIMIYU

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akipokelewa na baadhi ya watendaji kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Kanda ya Ziwa na Nishati na Madini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza. Profesa Muhongo anafanya ziara katika mikoa ya Simiyu, Tabora na Shinyanga lengo likiwa ni kukagua miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Taneesco.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega kabla ya kuanza ziara katika wilaya hiyo ili kujionea utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini pamoja na kuzungumza na wananchi.
Mkazi wa kijiji cha Ihale kilichopo wilayani Busega mkoani Simiyu ambaye jina lake halikupatikana mara moja akiuliza maswali mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na wananchi (hawapo pichani) mara Waziri alipofanya mazungumzo na wananchi wa kijiji hicho ili kusikiliza kero zao.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo kwenye mkutano na wananchi wa kata ya Ijitu iliyopo wilayani Busega.(P

MAGAZETI LEO JUMANNE TAR 6 JAN 2015




















Monday, January 5, 2015

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AKIHUTUBIA WAKAZI WA MPONDE

SERIKALI YAWAREJESHEA KIWANDA CHA CHAI WANANCHI WA MPONDE

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akiwasili mkoani Tanga ambapo alipokelewa Segera kijiji cha Mchungwani.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Tanga Aisha Kigoda mara baada ya kuwasili mkoani Tanga.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Tanga Mjini Omary Nundu wakati wa mapokezi yaliofanyika Segera kijiji cha Mchungwani.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Mchungwani kata ya Segera waliojitokeza kumpokea akiwa njiani kuelekea Mponde jimbo la Bumbuli.
 Gari iliyombeba Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye uwanja wa mkutano kijiji cha Mponde jimbo la Bumbuli.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mwenyekiti wa Wakulima Halmashauri ya Bumbuli Almasi Kassim wakati akiwasili kwenye uwanja wa mikutano wa kijiji cha Mponde.
 Sehemu ya Umati wa wakazi wa kijiji cha Mponde waliojitokeza kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu  Abdulrahman Kinana ambaye amerudi Mponde kutimiza ahadi yake ya kurudi na kulizungumzia suluhisho la mgogoro wa kiwanda cha Chai cha Mponde.
 Wananchi wakinyoosha mikono juu kama ishara ya kumsalimia Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
 Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mhe. Majid Hemed Mwanga akisalimia wananchi wa Mponde waliojitokeza kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aliyerejea kijijini hapo kutimiza ahadi yake ya kurejea .

 Msanii aliyevaa kinyago usoni akiigiza kama muwekezaji wa chai Mponde.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Mponde ambapo aliwaambia Serikali imerudisha kiwanda cha chai cha Mponde kwa wananchi hao.
 Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Chai Tanzania Mathias Assenga Benedict akisalimia wananchi wa Mponde mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,
 Mkurugenzi Mkuu wa Maendeleo ya wakulima wadogo wa chai Tanzania Ndugu Mustafa  Umande akisalimia wananchi wa Mponde.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Mponde.
 Mbunge wa Jimbo la Bumbuli ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh.January Makamba akiwasalimia wananchi wa Mponde ambapo alimshukuru Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwa kazi nzuri ya kujenga na kuimarisha chama.
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mponde na kuwataka kuwa na umoja na ushirikiano na kuepuka watu watakaotaka kutumia fursa hiyo ya umiliki wa kiwanda .