Saturday, January 31, 2015

Msanii Wa Injili Rose Muhando Akimsifia Msanii H.Baba Kwa Shows zake.

Neymar awa tatizo ligi ya Hispania.

neymar-barcelona-2013-hd-wallpapers-jpg

Kiungo mshambuliaji wa Barcelona Neymar Da Silva Jr vamekuwa kwenye kiwango cha juu msimu huu ambapo amekuwa sehemu muhimu sana ya timu yake katika michezo ya hivi karibuni .
Neymar amedhihirisha ubora wake kwa jinsi ambavyo amekuwa akifunga mabao mfululizo huku akisaidia kwa kutoa pasi za mwisho kwa wenzie na amekuwa akifanya hivyo kwa mwendelezo mzuri ,
Tatizo limekuwa moja tu , jinsi amabvyo mchezaji huyu amekuwa akilaumiwa hasa na wapinzani kwa kuwa mtovu wa nidhamu na mkosefu wa heshima ambapo amekuwa akiwadhihaki wachezaji wa timu pinzani kwenye nyakati tofauti hali ambayo imeonekana kuwakera wengi .
Wapinzani wa Barcelona wamemlalamikia Neymar kwa kitendo chake cha kuwadhihaki anapokuwa uwanjani .
Wapinzani wa Barcelona wamemlalamikia Neymar kwa kitendo chake cha kuwadhihaki anapokuwa uwanjani .
Neymar amekuwa na tabia ya kuwatukana wachezaji wa timu pinzani na wakati mwingine hata kwa vitendo na ndio maana amekuwa kwenye vurugu nyingi ambazo zimekuwa zikitokea kwenye michezo ya Fc Barcelona .
Majuzi wakati wa mchezo war obo fainali ya michuano ya Kombe la Mfalme ambapo Barcelona ilishinda kwa 3-2 Neymar alikuwa kwenye fujo zilizoibuka kati yake na wachezaji wa Atletico ambao ni Gabi , Juan Fran na Raul Garcia.
Ilifikia mpaka kocha Luis Enrique alilazimika kumtoa uwnajani ambapo baadae alikir kufanya hivyo kwa lengo la kumlinda .
Neymar amekuwa akihusika kwneye vurugu zinazotokea uwanjani kutokana na tabia yake ya kuwatukana wachezaji wa timu pinzani .
Neymar amekuwa akihusika kwneye vurugu zinazotokea uwanjani kutokana na tabia yake ya kuwatukana wachezaji wa timu pinzani .
Hivi karibuni Luis Enirque alisikika akisema kuwa Neymar anapaswa kujiheshimu na kuwaheshimu wapinzani na kama asipofanya hivyo huenda akafanywa ‘chambo’ na kuumizwa na wachezaji wa timu pinzani ambao wamejawa na hasira juu yake .
Tabia hii ya Neymar itawakumbusha wengi juu ya kile kilichokuwa kinafanywa na Ronaldinho Gaucho wakati akiwa na klabu hii ya Barcelona ambapo aliripotiwa kuwadhihaki na kuwatusi wapinzani huku akiendelea kuwakera kwa chenga zake za maudhi .

Baba yao P Square alifariki Nov 2014, kazikwa hivi jana, Jan 30 2015. #RIP

Psq VIIMzee Moses Okoye, baba mzazi wa mastaa wa muziki kutoka Nigeria, Peter na Paul Okoye wa kundia laP Square’ alifariki November 25 2014 baada ya kuanguka kwenye ngazi ndani ya nyumba.
Taarifa za wanafamilia zilisema mzee huyo alifanyiwa upasuaji wa goti siku za nyuma na hali yake ilianza kuwa sawa kabla ya kufariki ambapo leo January 30, 2015 ndio mzee huyu amezikwa ikiwa ni miaka miwili imepita toka kufariki kwa mama yao.
Hizi ni picha za safari ya mwisho ya Mzee Moses Okoye, baba wa mastaa mzazi wa P Square na Jude ‘Engees’ Okoye.
Ps
Psq II
PSq Iv
Psq IX
.
Peter na Paul Okoye.
Psq VI
PSQ vkas
.
Peter na kaka yake Jude Okoye.
pSQ
P S 1
PS 2
PS 3
Kulikua na ulinzi pia
Kulikua na ulinzi pia
ps 5
ps 6

Mugabe ateuliwa kuwa mwenyekiti wa AU



Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ndio mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika -Au
Rais mkongwe wa Zimbabwe Robert Mugabe, mwenye umri wa miaka tisini, sasa ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa muungano wa Afrika-AU.
Wajumbe walimteuwa Mugabe kwa kauli moja katika mkutano wa AU unaoendelea mjini Addis Ababa-Ethiopia.
Sasa Mugabe amechukua mahala pak mwenyekiti anayeondoka wa muungano huo, Nkosazana Dlamini-Zuma.
Uteuzi wa Mugabe kuongoza muungano huo mkubwa ulio na wanachama zaidi ya arubaini, sasa umeingiza doa ndani ya AU, kwani Mugabe hana uhusiano mzuri na mataifa ya Magharibi, hasa baada ya kukaa uongozini tangu Zimbabwe ilipojipatia uhuru mnamo mwaka wa 80.BBC

Monday, January 26, 2015

JK atema mawaziri 60


Dar es Salaam. Panga pangua ya saba ya Baraza la Mawaziri iliyofanyika juzi imefikisha mawaziri 61 waliotemwa, kujiuzulu au kufariki dunia tangu Rais Jakaya Kikwete aingie madarakani mwaka 2005, huku mawaziri 16 wakihimili mawimbi hayo hadi sasa.
Katika mabadiliko hayo saba yaliyofanywa katika kipindi cha miaka tisa, wako waliobadilishwa wizara, kupandishwa kutoka naibu waziri kuwa waziri kamili, huku sura mpya zikiingizwa.
Mabadiliko hayo yalitokana na mawaziri kutakiwa kuwajibika kutokana na kashfa mbalimbali, huku mengine yakitokana mawaziri kufariki na moja likitokana na Waziri Asha-Rose Migiro kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Katika panga pangua hiyo, mawaziri 16 wamefanikiwa kudumu katika baraza hilo tangu Rais Kikwete aingie madarakani ambao ni Sofia Simba, Profesa Mark Mwandosya, Stephen Wasira, Dk Hussein Mwinyi na Dk John Magufuli.
Wengine ni Profesa Jumanne Maghembe, Dk Shukuru Kawambwa, Hawa Ghasia, Dk Mary Nagu na Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye kabla ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo, alikuwa naibu waziri na baadaye waziri wa Tamisemi.
Mawaziri wengine waliopo sasa ambao mwaka 2005 walikuwa manaibu mawaziri ni Gaudencia Kabaka, Bernard Membe, Celina Kombani, Christopher Chiza na Mathias Chikawe.
Naibu waziri pekee ambaye alikuwamo katika baraza la mawaziri la kwanza la Rais Kikwete akiwa na wadhifa huohuo ni Dk Makongoro Mahanga ambaye sasa ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira.CHANZO:MWANANCHI
Waliotemwa
Mawaziri waliotemwa au kujiuzulu tangu Rais Kikwete aingie madarakani, wakiwamo wale walioshindwa katika kinyang'anyiro cha ubunge ni Edward Lowassa, ambaye alijiuzulu, Antony Diallo, Dk Ibrahim Msabaha, Basil Mramba, John Chiligati, Andrew Chenge, Joseph Mungai, Dk Emmanuel Nchimbi, Lawrence Masha, Mustafa Mkulo, William Ngeleja, Dk Cyril Chami, Omary Nundu, Bakari Mwapachu na Kingunge Ngoimbale-Mwiru.
Wengine ni Ezekiel Maige, Dk Hadji Mponda, Teresa Huvisa, Shamsi Vuai Nahodha, Nazir Karamagi, Dk Mathayo David, Khamis Kagasheki, Profesa Anna Tibaijuka, Profesa Sospeter Muhongo, Dk Batilda Buriani, Joseph Mungai, Diodorus Kamala, Mohamed Seif Khatib, Mwantumu Mahiza, Profesa Peter Msola na Profesa David Mwakyusa, Philip Marmo na Juma Ngasongwa.
Naibu mawaziri ni Dk Luca Siyame, Balozi Seif Ally Idd, Hezekiah Chibulunje, Shamsa Mwangunga, Daniel Nsanzugwanko, Hezekiah Chibulunje, Rita Mlaki, Dk Charles Mlingwa, Zabein Mhita, Athuman Mfutakamba, Dk Lucy Nkya, Goodluck Ole Medeye, Benedict Ole Nangoro, Gregory Teu, Philipo Mulugo, Mohamed Abood, Dk Aisha Kigoda, Omari Yusuf Mzee, Jeremiah Sumari, Dk Maua Daftari, Zakia Meghji, Joel Bendera, Abdisalaam Issa Khatib na James Wanyancha.Pia, wapo ambao walifariki dunia ambao ni Salome Mbatia, Juma Akukweti, Jeremiah Sumari na William Mgimwa.
Badiliko la Kwanza
Katika baraza lake la kwanza Rais Kikwete aliteua mawaziri na naibu mawaziri 60 Januari 2006 na ilipofika Oktoba 2006, Rais Kikwete alifanya mabadiliko ya kwanza makubwa ya baraza lake la mawaziri kwa kuwahamisha vituo vya kazi mawaziri 10 na naibu mawaziri wanane.
Mawaziri waliohusika na mabadiliko hayo ni Diallo (Maliasili na Utalii) ambaye alihamishiwa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Profesa Maghembe (Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana) kupelekwa Wizara ya Maliasili na Utalii.
Dk Msabaha (Nishati na Madini) alihamishiwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Karamagi (Viwanda na Biashara) alihamishiwa Wizara ya Nishati na Madini, Mramba (Miundombinu) alihamishiwa Viwanda na Biashara na Chiligati (Mambo ya Ndani) alihamishiwa Wizara Kazi, Ajira na Vijana.
Mawaziri wengine ni Chenge (Ushirikiano Afrika Mashariki) alihamishiwa Wizara ya Miundombinu, Dk Kawambwa (Maendeleo ya Mifugo) alihamishiwa Wizara ya Maji, Wasira (Maji) alihamishiwa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika na Mungai (Kilimo, Chakula na Ushirika) alihamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani.
Naibu Mawaziri waliohamishwa wizara zao na kupelekwa wizara nyingine ni Dk Nchimbi (Habari, Vijana, Michezo na Utamaduni) kwenda Wizara ya Kazi, Nsanzugwanko (Kazi na Ajira) kwenda Wizara ya Habari, Michezo na Utamaduni, Dk Mathayo (Biashara na Viwanda) kwenda Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika na Chibulunje (Kilimo, Chakula na Ushirika) kwenda Wizara ya Viwanda na Biashara.
Wengine ni Dk Buriani (Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto) kuhamishiwa Wizara ya Mipango, Uchumi na Uwezeshaji, Mbatia (Mipango, Uchumi na Uwezeshaji) kwenda Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Masha (Nishati na Madini) kwenda Mambo ya Ndani na Membe (Mambo ya Ndani) kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini.
Badiliko la Pili
Februari 2007, Rais Kikwete alifanya uteuzi wa mawaziri wawili na naibu waziri wawili baada ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk Asha-Rose Migiro kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Nafasi ya Migiro ilichukuliwa na Membe.Dk Buriani aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Uratibu) kujaza nafasi iliyoachwa wazi baada ya kifo cha Akukweti. Kabla ya uteuzi huo Buriani alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mipango, Uchumi na Uwekezaji.
William Ngeleja aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini na Gaudence Kayombo aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mipango, Uchumi na Uwekezaji.
Badiliko la tatu
Februari 12, 2008 baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu kutokana na kashfa ya Richmond, Kikwete alivunja Baraza la Mawaziri na kuliunda upya.
Lowassa alijiuzulu sambamba na waliokuwa mawaziri wawili Dk Msabaha na Karamagi ambao wote walikuwa wameiongoza Wizara ya Nishati na Madini kwa nyakati tofauti. Nafasi zao zilizibwa na William Ngeleja (Nishati na Madini), Dk Kamala (Afrika Mashariki), huku Pinda akiteuliwa kuchukua nafasi ya Lowassa.
Badiliko la nne
Rais Kikwete alifanya mabadiliko mara ya nne katika baraza lake Mei, 2008 baada ya Chenge, ambaye ni mbunge wa Bariadi, kujiuzulu kutokana na kashfa ya ununuzi wa rada na nafasi yake kujazwa na mbunge wa Bagamoyo, Dk Kawambwa huku Rais Kikwete pia akibadilisha mawaziri kadhaa.
Badiliko la tano
Mei 2012, Rais Kikwete alifanya mabadiliko ya tano katika baraza lake baada ya kuwaondoa mawaziri sita baada ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kubaini kuwa walikiuka maadili ya utumishi wa umma na kushindwa kuwajibika kisiasa kusimamia mali za umma.Katika mabadiliko hayo waliondolewa walikuwa ni Mkulo (Fedha), Ngeleja (Nishati na Madini), Dk Mponda (Afya na Ustawi wa Jamii), Maige (Maliasili na Utalii), Nundu (Uchukuzi) na Dk Chami (Viwanda na Biashara). Wengine waliotemwa ni Mfutakamba (Naibu, Uchukuzi) na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Nkya.
Mawaziri walioziba nafasi hizo ni William Mgimwa (Fedha), Kagasheki (Utalii), Dk Harrison Mwakyembe (Uchukuzi), Dk Abdallah Kigoda (Viwanda na Biashara), Dk Mwinyi (Afya), Profesa Muhongo (Nishati na Madini), Dk Seif Rashid (Naibu, Afya) na George Simbachawene (Naibu, Nishati na Madini).
Manaibu wapya walioingia ni January Makamba (Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia), Dk Charles Tizeba (Uchukuzi) na Amos Makala (Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo). Wengine ni Dk Binilith Mahenge (Maji), Stephen Masele (Nishati na Madini), Angela Kairuki (Katiba na Sheria), Janet Mbene na Saada Mkuya Salum (Fedha).
Badiliko la sita
Januari 19, 2014, Rais Kikwete alifanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri kwa kuteua mawaziri wapya wawili na manaibu mawaziri wapya wanane, huku akiwapandisha vyeo manaibu mawaziri wanne kuwa mawaziri kamili.
Katika mabadiliko hayo, Rais Kikwete aliwapumzisha Dk Terezya Huvisa, ambaye alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Gregory Teu, aliyekuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara na Philipo Mulugo aliyekuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Wengine waliopumzishwa ni Benedict Ole-Nangoro aliyekuwa naibu waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Goodluck Ole-Medeye aliyekuwa naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Mabadiliko hayo yalikuwa yanalenga kujaza nafasi zilizoachwa na Balozi Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii, Dk Nchimbi (Mambo ya Ndani ya Nchi), Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) na Dk Mathayo (Maendeleo ya Mifugo) waliotemwa Desemba 2013 kutokana na kashfa ya Operesheni Tokomeza na nafasi ya Dk Mgimwa, aliyefariki dunia kutokana na maradhi.
Mawaziri wapya walioteuliwa wakati huo ni Dk Asha-Rose Migiro (Katiba na Sheria), Dk Titus Kamani kuwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.
Wengine aliowateua kuwa naibu mawaziri ni Mwigulu Nchemba, Naibu Waziri wa Fedha, Dk Kebwe Stephen, Naibu Waziri, Afya na Ustawi wa Jamii na Jenista Mhagama, naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Pia, Dk Pindi Chana aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na Kaika Telele, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi. Wengine ni Godfrey Zambi, naibu Waziri Kilimo, Chakula na Ushirika, Juma Nkamia, Naibu Waziri Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Mahmoud Mgimwa, Naibu Waziri, Maliasili na Utalii.Naibu mawaziri waliopandishwa kuwa mawaziri ni Saada Mkuya (Waziri wa Fedha), Lazaro Nyalandu (Maliasili na Utalii) na Dk Seif Seleman Rashidi ( Afya na Ustawi wa Jamii), Dk Binilith Mahenge alipandishwa kutoka Naibu Waziri wa Maji na kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira).
Dk Hussein Ali Mwinyi alihamishwa kutoka Afya na Ustawi wa Jamii kwenda Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na wengine kadhaa walihamishwa.
Badiliko la saba
Juzi, Rais Kikwete alifanya mabadiliko ya saba ambayo yanawezekana kuwa yatakuwa ya mwisho kutokana na kusalia miezi sita kabla ya kuvunjwa kwa Bunge kupisha Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba.
Mabadiliko hayo baada ya mawaziri wawili, Profesa Tibaijuka (kufutwa kazi) na Profesa Sospeter kujiuzulu kutokana na kuhusishwa na kashfa ya Tegeta Escrow.
Walioingia ni manaibu waziri wawili, Charles Mwijage (Nishati na Madini) na Anna Malecela (Elimu na Ufundi). Wengine walihamishwa ambao ni Wasira kutoka Ofisi ya Rais kwenye Kilimo na Ushirika, Lukuvi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kwenda Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Wengine ni Dk Nagu kwenda Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu) na Jenister Mhagama (Waziri Mkuu, Uhusiano, Uratibu na Bunge).
Dk Harrison Mwakyembe anahamia Afrika Mashariki (kutoka Uchukuzi) na nafasi yake inachukuliwa na Sitta akitokea Wizara ya Afrika Mashariki.
                                                                        

SHERIA NGOWI AMVALISHA RAIS MPYA WA ZAMBIA



Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential suit) iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini TanzaniaSheria Ngowi akikagua gwaride rasmi kabla ya kuapishwa katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia. Guy Scott, of Scottish

Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential suit)iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini TanzaniaSheria Ngowi akila kiapo cha kuwa Rais Mpya wa Zambia katika sherehe za zilizofanyika jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia. Guy Scott, of Scottish.

Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential suit) iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini TanzaniaSheria Ngowi akipokea salaam Maalum Kutoka kwa Rais wa Mpito wa ZambiaGuy Scotts Muda mfupi baada ya kuapishwa katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia.

Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential suit)iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini Tanzania Sheria Ngowi akiwa na Mkewe Eshter Lungu Muda mfupi baada ya kuapishwa katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia.
-----
Mbunifu wa mavazi wa kimataifa, Sheria Ngowi ameendelea kuipeperusha bendera ya Tanzania kupitia kipaji chake cha ubunifu wa mavazi baada ya kumvalisha Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia.
Rais Lungu 58, aling'arisha sherehe hizo baada ya kuvaa suti rasmi (Presidential suit) rangi ya bluu, shati jeupe na tai nyekundu zilizobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa kimataifa, Sheria Ngowi. Lungu aliambatana na mke wake, Eshter Lungu walipokuwa wanaingia viwanjani hapo huku wakisindikizwa na ulinzi mkali.
Akizungumza baada ya hafla hiyo, Sheria Ngowi alisema amefurahi kupata nafasi ya kipekee ya kumvalisha Rais Lungu katika sherehe za kuapishwa kwake na kusema ni hatua kubwa katika kazi yake kama mbunifu wa mavazi wa kimataifa.
"Hii ni hatua kubwa katika kazi yangu ya ubunifu wa mavazi, namshukuru Mungu kwa kipaji alichonipa kinachoweza kunitambulisha na kunifanya niaminike hata kufikia hatua ya kuvuka mipaka ya Tanzania na kumvalisha Rais mpya wa Zambia, Mheshimiwa Edgar Lungu", alisema Ngowi.
Mbunifu Ngowi alisisitiza kuwa juhudi, nidhamu, bidii na kumweka Mungu mbele ndio chachu ya mafanikio katika kila utendaji wa kazi zake akiwa na malengo ya kuipeleka kazi yake katika nyanja za kimataifa hata kutambulika katika sekta ya ubunifu wa mavazi duniani kote.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na aliyekuwa Rais wa muda wa Zambia, Guy Scott na mke wake Charlotte, Mwenyekiti wa jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini(SADC), Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, baadhi ya viongozi wa juu wa Zambaia na nchi mbalimbali pamoja na wananchi wake.
Mbunifu huyo ameendelea kuonyesha na kudhihirisha kuwa Tanzania ni nchi yenye vipaji vinavyoweza kuiletea nchi ya Tanzania sifa na kuinua uchumi wake katika sekta mbalimbali. Hii si mara ya kwanza kwa mbunifu huyo kukata mawingu kuitangaza nchi yetu, kwani ni miongoni mwa wabunifu mashuhuri kutoka Afrika wanaopata fursa kuonyesha ubunifu wa mavazi yao katika maonyesho ya kimataifa kama vile New York Fashion Week nchini Marekani na Mercedes Benz fashion Week nchini Afrika Kusini.
Hii ni changamoto pia kwa wabunifu wa Tanzania kuziwania fursa zilizopo na pia kuongeza juhudi ili kutangaza na kupeleka kazi zao katika soko la kimataifa kama vile Sheria Ngowi alivyofungua mlango

Magazeti Leo Jumatatu






















TIGO MUSIC YAZINDULIWA RASMI TANZANIA.

unnamed1
Mwanamuziki Profesa J akiimba katika uzinduzi huo.
unnamed3
Mwanamuziki Vanessa Mdee akiimba katika uzinduzi huo.
Tigo Tanzania leo imetangaza rasmi uzinduzi wa Muziki wa Tigo ujulikanao kama "Tigo Music" kwa kushirikiana na Deezer, ambayo ni huduma ya kimataifa inayorusha muziki itakayowapa Watanzania muziki usiokuwa na kikomo.
Kutakuwa na hafla ya uzinduzi kwa ajili ya Tigo Music katika viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam Tarehe 24 Januari ambapo wananchi watatumbuizwa na nyimbo tofauti tofauti kutoka kwa wasaniii 18 wa hapa nchini kama Diamond Platinum, Ali Kiba, Professor J, Weusi, Msondo, Ben Paul, Shillole Linah, Christian Bella, AY hao ni kati ya 18.
Kuanzia Januari 24, wateja wa Tigo wenye vifurushi vya malipo ya kabla ya intaneti wana uwezo wa kupata nyimbo milioni 36 za wasanii wa Kitanzania na Afrika kwa ujumla katika simu zao za mkononi za smartphone. Vilevile, Tigo itatafuta miziki mipya ya kusisimua ya wasanii wa ndani kupitia ushirikiano mpya na kampuni ya Africa Music Rights, ambayo inawezesha, kutafuta na kusimamia haki za muziki katika bara la Afrika,
Meneja Mkuu wa Tigo Bi, Cecile Tiano alisema, 'Tuna furaha kuwa kampuni ya kwanza ya mawasiliano Tanzania kuwapa wateja wetu muziki usiokuwa na kikomo". Muziki unajukumu kubwa katika Tanzania yetu tajiri na tamaduni tofauti kama starehe katika matukio ya kijamii na hata wakati binafsi. Haya ni mafanikio makubwa kwetu tukitarajia watu zaidi na zaidi kutumia smartphones katika sehemu hii ya dunia'.
"Kama bidhaa yenye maisha ya kidijitali, lengo letu ni kuiwezesha tasnia ya muziki kwa kujenga jukwaa ambalo si tu linaruhusu kupata nyimbo za wasanii wa ndani kwa urahisi, lakini pia linawapa mafunzo wanamuziki wetu kwenye masuala muhimu kama vile haki miliki na masoko. Hii ni njia yetu ya kusaidia vipaji vya wasanii na kukuza tasnia ya muziki wa ndani, "aliongeza.
Kuanzishwa kwa Muziki wa Tigo (Tigo Music) nchini Tanzania kumetokana na mafanikio ya uzinduzi nchini Amerika ya Kusini mwaka 2012 pamoja na Ghana mwaka 2014, na. Tangu kuanzishwa kwake imekuwa ni sehemu muhimu kwa maisha ya kidijitali ya watu ya kila siku na hii inaendana na matukio ya muziki wa ana kwa ana yaliyowahi kufanywa na wanamuziki mashuhuri duniani, pamoja na yale yaliyorekodiwa ndani ya studio.
Kama bidhaa, Tigo music imeongezeka kwa kiasi kikubwa huko Colombia kama nchi inayoongoza kwa huduma ya urushwaji wa muziki, wakiwa na watumiaji 600,000 wakisikiliza kwa wastani nyimbo zaidi ya 400 na masaa 40 ya muziki kila mwezi.
Urushwaji wa muziki ni eneo linalokua kwa haraka sana katika tasnia ya muziki kimataifa, na bidhaa ya muziki tayari imekuwa ya pili kimaarufu kwenye vipengele vya simu za mkononi katika Afrika.

Sunday, January 25, 2015

Mnyika awasilisha hoja kupinga kura ya maoni

Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika, amewasilisha taarifa kwa Katibu wa Bunge akitaka Bunge lijadili udhaifu wa katiba inayopendekezwa na kupitisha azimio la kuahirishwa kufanyika kwa kura ya maoni ya wananchi kuamua ama kuikubali au kuikataa katiba hiyo.

Pia amemtaka Rais Jakaya Kikwete kutangaza kufuta tangazo la serikali la kufanyika kwa kura hiyo mwishoni mwa Aprili, mwaka huu, hadi uchaguzi mkuu utakapofanyika.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mnyika alisema kama ambavyo Rais Kikwete alitumia sheria kutangaza upigaji kura hiyo, ni vema pia akafanya hivyo kuutengua kwa kuwa kuna udhaifu katika mchakato mzima.

Alisema zimebaki siku chache kufanyika mchakato huo, lakini hadi sasa elimu kuhusiana na suala hilo haijatolewa kwa wananchi.

“Kwa kuheshimu sheria, Rais ajitokeze atoe tangazo la kulifuta tangazo la serikali la kufanyika kwa kura ya maoni hadi baada ya uchaguzi mkuu. La sivyo, tutakwenda kubanana na udhaifu wa utendaji wake utaanikwa bungeni,” alisema Mnyika.

Alisema kabla ya mchakato huo, serikali ilipaswa kutoa elimu kwa umma miezi miwili na kutenga siku 30 kwa ajili ya kampeni, lakini vitu hivyo havijafanyika.

“Sheria inataka kuwe na uandikishaji, utoaji elimu, kampeni na uhakiki wa walioandikishwa katika daftari kama ni sahihi au umechakachuliwa, vitu ambavyo havijafanyika mpaka sasa,” alisema Mnyika.

Aliongeza: “Rais anakiuka sheria ya nchi kwa kulazimisha kura ya maoni kufanyika Aprili wakati bado kuna udhaifu mkubwa katika mchakato mzima wa zoezi hilo.”

Aliunga mkono kauli ya aliyekuwa Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, aliyoitoa wakati akifanya mahojiano na NIPASHE juzi.

Jaji Warioba alisema kura ya maoni haiwezi kufanikiwa kutokana na maandalizi hafifu.

Alisema kwa mujibu wa sheria namba tatu ya mwaka 2014, ambayo inahusu kura ya maoni, jambo la kwanza linalotakiwa kufanyika ni uboreshaji wa daftari la wapigakura, elimu kwa umma kwa kipindi cha miezi miwili kisha kampeni za mwezi mmoja.

Aliitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kutangaza ratiba kamili ya kila eneo au uboreshaji wa daftari la wapigakura ndani ya wiki hii.

Alisema uboreshaji wa daftari hilo, ambao ulitakiwa kuwahi kwa ajili ya kufanikisha zoezi la upigaji kura ya maoni, lakini nalo limecheleweshwa kwa kuishia kuahirishwa mara kwa mara.

Wengine, ambao Mnyika alisema wataenda kubanwa bungeni kutokana na udhaifu wa utendaji wao katika kuchelewesha zoezi hilo, ni Ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Wizara ya Fedha na Wizara ya Katiba na Sheria.

Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, alipotafuta kuzungumzia kama amepokea taarifa ya Mnyika, alisema alikuwa katika kamati za Bunge zinazoendelea jijini Dar es Salaam, hivyo hakuwapo ofisini.

Alisema kama taarifa hiyo imepelekwa ofisini kwake anaamini imepokelewa na itafanyiwa kazi.

Rais Kikwete alitangaza zoezi la kura ya maoni Novemba 4, mwaka jana wakati akizungumza na wazee mjini Dodoma.

Alisema sheria ya kura ya maoni imeainisha muda wa wadau wa katiba kutoa elimu na kufanya kampeni, hivyo akataka sheria hiyo izingatiwe na kuheshimiwa ili kuepuka ugomvi.

Rais Kikwete alisema upigaji wa kura ya maoni kuhusu katiba hiyo utafanyika Aprili 30, baada ya elimu na kampeni juu ya kura hiyo kuanza rasmi Machi 30 na kuhitimishwa Aprili 29, mwaka huu kama sheria ya kura ya maoni inavyoelekeza.

Alisema imezoeleka kampeni ni siku 60, lakini baada ya kushauriana na wanasheria ilionekana siyo lazima isipokuwa inaamuliwa na rais kwa mujibu wa sheria.

MBATIA KUTIMULIWA UKAWA?


HALI inazidi kuwa mbaya ndani ya Kambi ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kufuatia taarifa za mgogoro mkubwa uliopo kati ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilbroad Slaa na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia.

Chanzo cha mgogoro huo ambao unafukuta, ni madai ya Slaa ya kutomwamini Mbatia anayedai ni pandikizi anayetumiwa na serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) kuvuruga umoja huo.

Inaelezwa, Slaa anamshutumu Mbatia kuwa ni Afisa wa Idara ya Usalama wa Taifa, hivyo ni hatari kwa ustawi wa umoja huo, na kuna uwezekano akasababisha kusambaratika kwake iwapo ataendelea kuwepo.

"Ukiwa nje huwezi kuona hali halisi ya mambo, kwa tulio ndani ndio tunaona kila kitu, huu umoja hauwezi kufika popote maana watu hawaamiani hata kidogo na kuna migogoro kila kukicha"

"Sasahivi Slaa anashinikiza Mbatia aondolewe UKAWA, anadai akiachwa atavuruga mpango wa kwenda ikulu" kilisema chanzo chetu kilichopo ndani ya kambi ya UKAWA.

Chanzo hicho kilisema, msimamo huo wa Slaa umewapa wakati mgumu vongozi wengine wa kambi hiyo na wanaona wakimtosa Mbatia watasababisha mgawanyiko wa wanachama, hivyo kuna uwezekano mkubwa wakampuuza Katibu Mkuu huyo.

"Slaa hapendi kumuona Mbatia akiwa UKAWA, ila Mbatia ni muhimu zaidi kuliko Slaa kwenye umoja huu maana anawakilisha chama na iwapo chama chake kitatoka kutasababisha mpasuko, kwahiyo kuna uwezekano mkubwa wakampuuza katibu mkuu, ila wakimpuuza unamjua mambo yake, ataanza vurugu ndani ya chama" kilisema chanzo chetu.

Aidha, mbunge mmoja wa CUF akizungumza na mwandishi wa habari hizi alisema, baadhi ya wanachama wa UKAWA wanamshutumu Mbatia kuwa mmoja wa walioshinikiza kambi hiyo kususia mchakato wa Katiba mpya na kushawishi wasirudi bungeni.

"Kuna mambo yanatia mashaka sana na leo viongozi wetu wanajuta, uamuzi wa kususia bunge la Katiba haukuwa sahihi, vongozi wetu walipotoshwa kususia bunge. Naamini kama tungebakia bungeni na kushindana kwa hoja, kingeeleweka"

"Mbatia alikuwa kinara wa kusisitiza tusirudi na kuna taarifa feki zilikuwa zinakuja ambazo zilionekana wazi mchakato ungekwama, lakini tumeona kilichotokea, CCM na baadhi ya wabunge wa UKAWA wakaendelea na wameandika walichotaka, na kwa hali ilivyo katiba wanayotaka wao itapita" alisema mbunge huyo kutoka Zanzibar (jina tunalihifadhi).  

Mbunge huyo alisema, hali hiyo inaonyesha wazi kuna watu ndani ya kambi hiyo wanatumika na CCM, na mbinu ya kushawishi UKAWA wasirudi bungeni ilikuwa ni maagizo maalum yenye lengo la kuwapa nafasi CCM kupitisha mambo waliyotaka kwenye Katiba mpya.

Taarifa zaidi zinasema, jambo jingine ambalo linampotezea imani Mbatia kwa baadhi ya viongozi wenzake, ni uhusiano wake na kigogo mmoja mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), ingawa mwenyewe mara kadhaa amekuwa akikana madai hayo na kushusha lawama kwa CCM kuhusika kusambaza madai hayo.

Inaelezwa, Mbatia amekuwa karibu na kigogo huyo na wamekuwa wakikutana mara kwa mara nyumbani kwake maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam kwa lengo la kupeana maelekezo ambayo hawana shaka yanalenga kufanya hujuma kwa kambi hiyo.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa waliozungumza na mwandishi wa habari hizi wamesema, kambi ya UKAWA ipo kwenye wakati mgumu ukiachilia mbali mgawanyiko uliopo katika suala la kuteua mgombea Urais kwenye uchaguzi mkuu ujao, kuna hali ya kutoaminiana na kila mmoja anamuona mwenzake ni msaliti.

"Kabla hawajaungana Chadema waliwahi kukishutumu CUF kuwa ni tawi la CCM (CCM B), Wenje (Ezekiel Wenje) aliwahi kuwashutumu CUF kuwa ni chama cha mashoga, Chadema hao hao walishamuita Mbatia ni mbunge wa Rais Kikwete kwa kuwa aliteuliwa na Rais hivyo ni mbunge anayefuata maagizo ya CCM" alisema John Malingumu mchambuzi wa masuala ya kisiasa.

Mchambuzi huyo aliongeza kuwa, kila mmoja ndani ya kambi hiyo ameungana na mwenzake kwa malengo binafsi, ila hakuna mwenye imani na mwenzake.

"Pale kuna unafki mkubwa, kila mmoja amebaki na historia yake kichwani ya mambo ambayo walifanyiana kabla hawajaungana, utakumbuka pia Chadema waligoma kuunda Kambi ya Upinzani na CUF, haya yote hayajafutika"

HII NAYO KALI KUTOKA MTWARA: ETI WAZUNGU WAFANYIWA TAMBIKO!



Bosi wa kampuni ya mafuta ya Maurel et Prom (T) Ltd akinywa dawa ya tambiko

Bosi wa kampuni ya mafuta ya Maurel et Prom (T) Ltd akipakwa dawa ya tambiko kwenye kipaji cha uso

Mabosi na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwa katika tambiko hilo linalodaiwa kufanyika mapema wiki hii.Za kitaa kutoka Mtwara zinadai kuwa bibi mmoja aliyeitisha Serikali kuwa ikifanya mchezo na haki za watu wa mkoa huo atabadili gesi kuwa maji, amewapigia tambiko Wafaransa wazungu wa Kampuni ya uchimbaji wa visima vya mafuta ya Maurel et Prom (T) Ltd yenye ofisi zake Chole Road, Msasani Peninsular, Dar es Salaam, baada ya kile kilichodaiwa drill yao ya kuchimbia mafuta kukatika mara tatu wakati wakichimba kisima cha urefu wa mita 3,000 chini ya bahari. Inadaiwa baada ya kuanza kuona maajabu katika kazi yao hiyo, fasta walijisalimisha kwa bibi huyo huko Mtwara na kukubali kufanyiwa tambiko ili mambo yanyooke, kama wanavyoonekana pichani hapo juu! Kama ni kweli, basi bibi anatisha! L