Saturday, January 10, 2015

Dr. kelvin mandopi aapishwa kuwa kamishna wa tume ya haki za binaamdamu

Dr.mandopi akiapa mbele ya raisi


nimekuwekea video hapo namna tume hii ilivyoapa mbele ya raisi,mungu awatie nguvu hasa mwalimu wangu Dr.mandopi

Msichana wa miaka kumi ajilipua Nigeria

Mlipuaji wa kujitolea muhanga ajilipua katika soko moja Nigeria
Mlipuaji wa kujitolea muhanga amejilipua katika soko moja katika mji wa kazkazini mashariki wa Maiduguri nchini Nigeria.Baadhi ya ripoti zinasema kuwa mlipuaji huyo ni msichana wa miaka kumi.Duru kutoka hospitali zimeambia BBC kwamba takriban watu 15 wameuawa.Hakuna mtu aliyekiri kutekeleza shambulizi hilo kufikia sasa.Hatahivyo watu wanalishuku kundi la Boko Haram kutokana na misururu yake ya mashambulizi katika mji huo na maeneo mengine ya Nigeria Kazkazini.Takriban watu elfu ishirini wamelazimika kutoroka na inahofiwa kuwa mamia waliuawa wakati Boko Haram lilipochukua udhibiti wa mji wa Baga na viungani mwake wiki iliopita.

Hujasoma Magazeti leo Jan 10? Nimekuchambulia story kubwa tano kutoka Magazetini, zisome hapa

NewspaperMTANZANIA
Wabunge wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wanakusudia kupeleka hoja binafsi Bungeni ili kumng’oa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia kwa kusababisha vurugu katika uchaguzi na siku ya kuapishwa wenyeviti Serikali za Mitaa.
Akizungumza na waandishi wa Habari jana, Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chama cha CUF,Magdalena Sakaya alisema wameamua hayo baada ya Ghasia mwenyewe kukataa kung’atuka na Rais Kikwete kushindwa kumuwajibisha kwa kushindwa kusimamia uchaguzi.
Sakaya amesema kuna baadhi ya maeneo ambayo uchaguzi haukufanyika lakini CCM ilitangazwa kushinda, huku maeneo mengine ambako vilishinda vyama vya upinzani lakini wakaitwa Wenyeviti waliokuwa wakigombea kupitia CCM kwa ajili ya kuapishwa hali iliyopelekea vurugu.
MWANANCHI
Jeshi la Polisi Dar wametangaza kumsaka mtu mmoja raia wa Marekani ambaye anatuhumiwa kumuua rafiki yake, Nadine Aburadas ambaye waliyefahamiana miaka mitatu iliyopita kupitia mtandao wa Facebook.
Mtu huyo anatuhumiwa kufanya mauaji hayo katika hoteli Uingereza na kukimbilia Tanzania ambapo vyombo vya habari vya Uingereza viliripoti kuhusu mauaji hayo.
Kaimu Mkurugenzi wa makosa ya jinai, Diwani Athumani amesema kuwa upelelezi kuhusu mtuhumiwa huyo bado unaendelea wakishirikiana na Interpol japo hana uhakika kama mtuhumiwa huyo bado nchini.
Taarifa zinasema mtuhumiwa huyo aliingia hotelini hapo na marehemu siku ya Desemba 30, siku ya January 1 alionekana akitoka peke yake hotelini hapo, akapanda ndege kwenda Bahrain na baadaye kuja Tanzania.
HABARI LEO
Mfanyabiashara Seleman Manoti amepandishwa Mahakama ya Wilaya Ilala kujibu mashtaka ya kujifanya Ofisa wa Usalama wa Taifa kwa lengo la kudanganya kufanya utapeli maeneo ya Kariakoo, Dar.
Mshtakiwa alikana mashtaka hayo na kurudishwa rumande kutokana na kushindwa kwa masharti ya dhamana yaliyomtaka kuwa na wadhamini wawili ambao walitakiwa kulipa sh. mil. 1.
HABARI LEO
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka amesema Jeshi la Polisi Mkoani humo wanamshikilia mwanamke mmoja anayetuhumiwa kusababisha kifo cha mtoto wa mwaka mmoja na mama wa mtoto huyo kulazwa baada ya kunywa pombe ya ‘mturuku’nyumbani kwa mtuhumiwa huyo.
Kamanda huyo amesema mwanamke huyo mtuhumiwa, Anastazia Kadama aliandaa pombe hiyo ya kienyeji na kuwaalika majirani kumsaidia kulima shamba lake, lakini ikashindikana kwenda kulima kutokana na mvua kubwa kunyesha.
Kutokana na kuhofu pombe hiyo kuharibika aliamua kuigawa kwa watu ili wainywe bure ikiwemo mama ambaye mtoto wake alifariki, Magdalena Muna.
Magdalena aliionja pombe hiyo na kumuonjesha mtoto wake, alianza kutapika na kuharisha, wakiwa njiani kuelekea Hospitali mtoto huyo alifariki.
JAMBO LEO
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Majengo Moshi, Peter Lyimo amelalamikia kuwepo utitiri wa vitabu vingi kwamba vinachangia wanafunzi kufeli katika mitihani yao na kuiomba Serikali kuhakikisha inaweka mitaala inayoendana na maisha ya Watanzania.
Mkuu huyo wa shule amesema kuwa utitiri huo wa vitabu unawachanganya wanafunzi ambao wanashindwa kuchagua vitabu vipi muhimu wasome na vipi wasivisome, huku kukiwa na msululu mkubwa wa vitabu kuingia sokoni bila kuhakikiwa hivyo wanafunzi kusoma vitabu vyenye makosa.
Mwalimu huyo amesema kumekuwa siasa imekuwa ikichangia kwa asilimia kubwa kuvuruga mfumo wa elimu ikiwemo mitaala kubadilishwa mara kwa mara hivyo kuwachanganya walimu na wanafunzi.

Barcelona kumfukuza kazi kocha wao kesho?

luis

Rais wa Fc Barcelona Joseph Bartomeu anatarajiwa kumfukuza kazi kocha wa klabu hiyo Luis Enrique baada ya mchezo wa ligi ya Hispania utakaopigwa jumapili dhidi ya mabingwa watetezi Atletico Madrid baada ya uhusiano wake na Lionel Messi kuendelea kuwa mbaya .
Taarifa zaidi zinadai kuwa rais huyo wa Barcelona alikutana na Messi hapo jana (ijumaa) na kumuarifu kuhusu mpango wake na inaaminika kuwa Messi aliunga mkono mpango huo huku akitoa maoni ya nani anapswa kuwa mrithi wa Enrique mara atakapofukuzwa.
Messi amependekeza kuteuliwa kwa kocha wa zamani Frank Rijkaard.
Messi amependekeza kuteuliwa kwa kocha wa zamani Frank Rijkaard.
Messi ameomba kurejeshwa kwa kocha wake wa zamani Mdachi Frank Rijkaard ambaye ndiye alikuwa kocha wa kwanza kumtoa Messi wakati akiwa kwenye kikosi cha timu za vijana na kumpa mchezo wake wa kwanza kwenye timu ya wakubwa kabla ya kuingia na kufikia mahali aliko leo hii.
Uhusiano wa Messi na kocha wake umeendelea kuripotiwa kuwa hauko vizuri pamoja na ushindi ilioupata Barcelona katika mchezo wake dhidi ya Elche ambako ilishinda kwa mabao matano huku Messi akishangiliwa na mashabiki wa Barcelona na wengine wakimzomea kocha .
Rais wa Barcelona Jose Maria Bartomeu amekanusha tetesi za kuwepo na mpango wa kumfukuza kazi Luis Enrique.
Rais wa Barcelona Jose Maria Bartomeu amekanusha tetesi za kuwepo na mpango wa kumfukuza kazi Luis Enrique.

zainabu Kawawa apigwa mawe


Mwaandishi wetu Liwale…. Wananchi wa  kata ya Kipule  kijiji cha  Makinda wilaya  Liwale  mkoani Lindi wamemtimua mbunge wa viti maalum,zainabu  Kawawa  kwa  madai  kufanya mkutano wa kutangaza nia ya kuomba ubunge katika jimbo hilo kabla ya  muda wa kufanya hivyo haujafika. Tukio hilo limetokea juzi(alhamisi)  majira ya saa nane  mchana baada ya mbunge huyo kufika kijijini hapo kwa lengo la kukutana na  mwenyekiti wa kijiji Salum Kachwele ili kumtaka  aitishe  mkutano wa wajumbe wa serikali ya kijiji na baadhi ya wananchi hasa wazee maarufu ikiwa ni kuwashaawishi ili wamwuunge mkono katika harakati zake za kuwania ubunge wa jimbo hilo. Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Salum Kachwele alisema mbunge huyo alifika kijiji hapo akiwa na mpambe wake Mkopora Mkopara  na   kumuomba awaite  wajumbe wa serikali  ya kijiji  pamoja na wazee maarufu ili azungumze nao jambo ambalo alidai hakulikubali kwani kabla ya harakati hizo za ubunge Kawawa hajawahi kufanya kikao chochote wala kutembelea katika kijiji hicho. Kachwela alisema  kabla zoezi la kukutana na wanachi hao  halijafanikiwa lilikuja kundi  kubwa la wananchi likiongozwa na vijana wakizomea wakiwa na mawe na magongo waliotokea kwenye mkutano wa chama cha wananchi cuf waliokuwa kwenye mkutano wakuwashukuru wananchi kwa kukichangua cha hicho kwenye uchagunzi wa serikali uliopita  na kumtaka mbunge huyo kuondoka katika eneo  mara moja.  Kwa upande wake mbunge  Zainabu kawawa alikiri kutembelea kijiji hapo ila alikataa kufanya kikao na wananchi hao  na kutokea tukio la kufukuzwa na kueleza kuwa yeye alikwenda kufanya ziara ya kikazi ya kuwatembelea wapiga kura kuhamasisha maendeleo.  ‘Ndugu  yangu hayo maneno sio kweli mimi nilikwenda kijiji hapo kufanya kazi za kibunge sio kufanya kampeni kama ilivyoelezwa na hao watu wasionitakia mema’ukweli ni kwamba  mti wenye matunda matamu ndiyo unapigwa mawe alisema Kawawa.SAUTI YA KUSINI

Red Carpet, utoaji wa Tuzo

Diamondz
Usiku wa January 8, ilikuwa ni siku ambayo  Shirikisho la Soka  Afrika, CAF walitoa Tuzo  kwa Wachezaji  Bora wa Afrika waliofanya vizuri kwa mwaka 2014.
Hapa nimekuwekea Pichaz za Redcarpet  za baadhi ya mastar waliohudhuria sherehe hizo pamoja na matukio mbalimbali ikiwemo show ya P  Square, Diamond Platnumz, Flavourna Fally Ipupa.
Msanii Lynxxx wa Nigeria

.
Muigizaji wa Nolywood, Van Vicker.

Glo-CAF-Awards-January-2015-BellaNaija0003-400x600
.
Muigizaji wa Noloywood, Richard Mofe-Damijo

Mchekeshaji Bovi (huyu alitokea kwenye video ya Yemi Alade ya 'Johnny')
Mchekeshaji Bovi (huyu alitokea kwenye video ya Yemi Alade ya‘Johnny’)
.
Mchezaji Jay Jay Okocha.

Glo-CAF-Awards-January-2015-BellaNaija0006-400x600 - Copy
Golikipa Vincent Enyeama, huyu alikuwa akiwania pia tuzo hiyo.
Glo-CAF-Awards-January-2015-BellaNaija0060-400x600
Msanii 2 Face Idibia.
Glo-CAF-Awards-January-2015-BellaNaija0067-400x600
.
Asisat Oshoala, mchezaji wa mpira wa miguu kutoka Nigeria.

.
Mchezaji Yaya Toure akiongea baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo hiyo.

Glo-CAF-Awards-January-2015-BellaNaija0055-600x400
Glo-CAF-Awards-January-2015-BellaNaija0056-600x400
Diamondz
Diamond Platnumz akifanya show.
.
Msanii Flavour akifanya show.
Glo-CAF-Awards-January-2015-BellaNaija0026-600x400 - Copy
Glo-CAF-Awards-January-2015-BellaNaija0044-600x400
.
Msanii Fally Ipupa.
.
P Square.
Glo-CAF-Awards-January-2015-BellaNaija0081-600x400

Friday, January 9, 2015

nikiwa chuo cha uongozi wa mahakama lushoto kabla ya mitihani ya timrd test













Mastaa wa movie waliopata pesa nyingi zaidi Holywood 2014

Filamu inalipa sana hasa kwa nchi za wenzetu, wamekuwa na mfumo mzuri ambao inakuwa rahisi hata kupata takwimu za kipato ambacho kupitia kazi hiyo wamekuwa wakikusanya kwa mwaka.
Jarida la Forbes limetoa orodha ya mastaa 10 walioongoza kwa kukusanya pesa nyingi kwa mwaka 2014, list yote iko hapa.
j lawrance
No.1Jennifer Lawrence, amekusanya kiasi cha dola za Marekani bilioni 1.40 kupitia kucheza movie peke yake ikiwemo movie ya The Hunger Games: Mockingjay na X-Men: Days of the Future Past.
chris prant
No. 2: Chris Pratt, dola bil 1.20 ndizo alizopata kupitia movie alizocheza, the Lego Movie na Guardians of the Galaxy.
scarlett
No. 3Scarlett Johansson, amepata dola bilioni 1.18 kupitia movie, moja ambayo ameonekana 2014 ni movie ya Captain America: the First Avenger.
mark
No. 4Mark Wahlberg, kipato chake ni dola bilioni 1 kupitia kucheza movie ya Transformer: Age of Extinction.
evance
No. 5Chris Evance, amepata dola milioni 801 kupitia movie zaSnow Piercer na Captain America: Winter Soldier.
emma stone
No. 6Emma Stone, amejikusanyia dola milioni 764 kupitia movie kama Magic in the Moonlightthe Amazing Spiderman na Birdmanmwaka 2014.
jolie
No.7Angelina Jolie mwaka 2014 haukuwa mzuri sana kwake, kiasi alichoingiza ni dola milioni 758 kupitia movie ya Maleficent.
james
No. 8James McAvoy, amekusanya dola milioni 747 kupitia filamu ya X-Men: Days of the Future Past na the Disappearance of Eleanor Rigby.
michael
No. 9: Michael Fassbender, amepata dola milioni 747 kupitia movie ikiwemo Shame na 12 years a Slave.
wolverine-jackman-_3150891k
No. 10Hugh JackmanDays of the Future Past imesaidia kumuingizia kiasi cha dola mil. 746 kwa mwaka 2014.