Hii (hapo chini) ni video mpya ya wasanii kutokea Nigeria,Bracket iitwayo Alive waliyowashirikisha Tiwa Savage pamoja na Diamond Platnumz ukishamaliza kuitazama mtu wangu usiache kuniandikia lako la moyoni ili Bracket na Diamond & Tiwa Savage wakipita waone watu wao mmesema nini kuhusu video hiyo.karibuni sana wasomaji wa blog hii usikubali kupitwa na habari tanzania na hata nje ya tanzania.
Tuesday, December 23, 2014
Mabibi na Mabwana,Bracket wametuletea hii video mpya waliyomshirikisha Diamond
Hii (hapo chini) ni video mpya ya wasanii kutokea Nigeria,Bracket iitwayo Alive waliyowashirikisha Tiwa Savage pamoja na Diamond Platnumz ukishamaliza kuitazama mtu wangu usiache kuniandikia lako la moyoni ili Bracket na Diamond & Tiwa Savage wakipita waone watu wao mmesema nini kuhusu video hiyo.
Hatua hiyo imechukuliwa na Rais Kikwete mbele ya wazee wa Dar Es Salaam aliokuwa akiongea nao na matangazo kurushwa moja kwa moja kupitia televisheni ya taifa na vyombo vingine.
Uchunguzi uliofanywa na kamati ya hesabu za umma ya Tanzania (PAC), ilidai kuwa Profesa Tibaijuka ni mmoja wa watu walionufaika kinyume cha sheria kwa kupata fedha zilizotoka katika akauti hiyo iliyofunguliwa kutunza fedha kusubiri ufumbuzi wa mgogoro wa kibiashara kati ya kampuni ya kusambaza umeme TANESCO na kampuni binafsi ya kuzalisha umeme ya IPTL.
Siku chache zilizopita Profesa Tibaijuja aliitisha mkutano na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam kubainisha kuwa hakuwa akikusudia kujiuzulu kutokana na tuhuma zilizokuwa zikimkabili.
Hata hivyo Rais Kikwete hakutangaza kuwachukulia hatua watumishi wengine waliodaiwa kuhusika na tuhuma hiyo kwa maelezo kuwa uchunguzi zaidi unatakiwa kwa kila mtuhumiwa.
Kumekuwa na ubishi mkubwa kujadili endapo fedha ambazo ni mabilioni zilizochukuliwa zilikuwa za umma au la. Na hata Rais Kikwete amesema maelezo aliyopewa na wataalam yanaonyesha hazikuwa mali ya TANESCO.
Monday, December 22, 2014
Essebsi ajitangaza kushinda Tunisia
Mgombea Urais, akitangaza ushindi nchini Tunisia
Matokeo ya awali ya uchaguzi wa Rais nchini Tunisia yanaonesha kuwa Beji Caid Essebsi anaongoza kwa zaidi ya asilimia 55 ya kura
Licha ya Kujitangaza mshindi, mpinzani wake ambaye ameshika nafasi ya pili Moncef Marzouki amesema matokeo hayo yanakaribiana mno.
Wakati wafuasi wa Beji Caid Essebsi wakishangilia ushindi, kiongozi wa kampeni ya uchaguzi wa Bwana Essebsi, Mohsen Marzouk, amedai ushindi.
‘’…Kulingana na matokeo ya awali kutoka katika vituo vya kupigia kura tunaweza kusema kuwa Beji Caid Essebsi ameshinda katika duru ya pili...'' Anasema Marzouk.
Hata hivyo wakosoaji wake wanasema, ushindi wa bwana Essebsi ni ishara kurudi tena uongozi usioaminika.
Lakini mwenyewe anasema ni mtendaji ambaye ataimarisha nchi hiyo.
Uchaguzi huo unaonekana kama kilele cha mageuzi ya kisiasa ambayo nchi hiyo imepitia kufuatia machafuko ya kisiasa yaliyotokea takriban miaka minne iliyopita.
Subscribe to:
Posts (Atom)













































































