Leo huenda ikawa moja ya siku ambayo itaingia kuwa siku yenye headlines kubwa kwenye siasa TANZANIA, wakati wa mchana kulikuwa na taarifa kutoka Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini, Dar es Salaam ambapo aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo alifanya kikao na waandishi wa Habari na kutangaza kujiuzulu.
Kubwa nyingine kwenye upande huo huo ni ishu ya Rais Kikwete
kutangaza mabadiliko madogo ndani ya Baraza la Mawaziri, ambapo
mabadiliko hayo nimekuwekea hapa, wapo waliohamishwa na wapo waliokuwa
Manaibu Mawaziri sasa ni Mawaziri, list yote ni hii hapa;
Mawaziri
George Simbachawene – Waziri wa Nishati na Madini
Mary Nagu- Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais- Mahusiano na Uratibu
Christopher Chiza- Waziri Uwezeshaji na Uwekezaji
Harrison Mwakyembe- Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
William Lukuvi- Waziri wa Ardhu, Nyumba na Makazi
Steven Wasira- Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
Samuel Sitta- Waziri wa Uchukuzi
Jenista Muhagama- Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge
Manaibu Waziri
Stephen Masele- Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu Rais- Muungano
Angela Kairuki- Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi
Ummy Mwalimu- Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
Anna Kilango- Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Charles Mwaijage- Naibu Waziri wa Nishati na Madini
No comments:
Post a Comment