Thursday, December 11, 2014

Jopokazi moja nchini Afrika Kusini limesema kua mwanawe Jacob Zuma hakua makini alipokuwa anaendesha gari hadi kusababisha ajali ya barabarani ambapo mwanamke mmoja alifariki.
Awali kiongozi wa mashitaka hakuwa tayari kumchukulia hatua zozote za kisheria mwanawe Zuma. Sasa atakabiliwa na shinikizo za kumfungulia mashitaka.
Gari la Duduzane Zuma aina ya Porsche iligonga gari dogo la abiria mjini Johannesburg mwezi Februari, na kumuua mwanamke huyo papo hapo.
Mwandishi wa BBC Pumza Fihlani mjini Johannesburg anasema uamuzi huo unaonyesha uhuru wa vyombo vya sheria nchini humo.
Katika nchi ambapo swala la usawa bado ni tete, mahakama ndio mojawpao ya sehemu chache ambapo usawa unapatikana kwa wananchi na mwanawe Rais hajasazwa kwa hilo.
Rais Zuma ana watoto 21 na ameoa mara sita.
Duduzane mwenye umri wa miaka 30 aliambia jopokazi hilo kwa alipoteza mwelekeo wa barabaraalipokuwa anaendesha gari na kuingia ndani ya maji taka.
Hata hivyo hakimu alimwambia kwamba hakua na tabia njema hasa baada ya tukio hilo.
Mwezi Julai mamlaka ya mashitaka ilikataa kufungulia mashitaka kijana huyo ambaye pia ni mfanyabiashara na kosa la mauaji bila ya kukusudia ikisema hakuna ushahidi wa kutosha.
Watu watatu walijeruhiwa katika ajali hio.

No comments:

Post a Comment