Siku chache zilizopita kulikuwa na taarifa kwamba kuna ugeni wa kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani ambapo atakuwa anatembelea Ufilipino.
Ambacho sikuwa nimejua ni hii kuhusu taarifa ya agizo rasmi kwa matrafiki na maofisa usalama wa Ufilipino kutakiwa kuvaa pampers muda wote wakati wa ziara ya Papa ambayo itakuwa kati ya tarehe 15-19 January, hilo lilikuwa agizo la Mwenyekiti wa Mamlaka ya Maendeleo ya Metropolitan Manila, Francis Tolentino.
Lengo la agizo hili ni kuwafanya Askari na maafisa hao kuwa kazini muda wote wakati wa ziara ya Kiongozi huyo.
Ziadi ya trafiki 2,000 ambao watakua kazini katika ziara hiyo itakayoanza Januari 15 hadi 19 watatakiwa kuvaa nepi hizo zitakazowawezesha kukaa katika maeneo yao ya kazi bila kuondoka kwenda kujisaidia wakati wa ziara ya Papa.
Ofisa wa Mamlaka ya Maendeleo ya Metropolitan Manila, Emerson Carlos alisema nepi hizo zitafanyiwa majaribio wakati wa maandamano maalum ya Black Nazarene.
“Tutawapa nepi hizi kwa sababu hatufahamu ni wakati gani mkusanyiko wa watu utaongezeka zaidi, tunataka amani itawale wakati wote wa ziara“– Carlos.
Nchi hiyo inatarajia ugeni mkubwa wa mamilioni ya watu kutoka Asia kujitokeza kumuona Papa na pia kushiriki ibada maalum atakayoiongoza tarehe 18 huko Manila.
Unadhani bongo ingekuwa vipi story ya matrafiki kuvalishwa pampers?
No comments:
Post a Comment