Sunday, January 11, 2015

Mkusanyiko wa Stori kubwa muhimu zilizoandikwa kwenye Magazeti ya leo January 11, 2015

NIPASHE
Rais Jakaya Kikwete ametangaza habari njema kwa Watanzania kwamba kuanzia mwaka kesho elimu ya Sekondari na msingi itatolewa bure.
Alisema hatua hiyo inakuja baada ya kukamilisha sera mpya ya elimu na ufundi  ili kuboresha sekta hiyo ambayo imepitishwa na Baraza la Mawaziri.
Hatua hiyo inachukuliwa katika kuhakikisha kila Mtanzania anapata kiwango hicho cha Elimu kwa gharama inayobebwa na Serikali.
Kwenye sera mpya,imeanisha jinsi ya utoaji wa elimu bora na viwango vinavyokubalika katika ufundi,hii itawezesha elimu hizi mbili kukidhi matakwa katika soko la ajira pamoja na kujiajiri“alisema.
Hatua ya Rais kutangaza azma ya kutoa elimu bure imekuja miaka 10 baada ya wapinzani hasa Chadema kueleza kuwa moja ya mikakati yao ni kutoa elimu bure kwa kila Mtanzania iwapo watachaguliwa kuongoza nchi.
NIPASHE
Zoezi la kuwaapisha watu 500 wakiwemo wenyeviti na wajumbe wa Serikali za Mitaa na wa Vitongoji katika Halmashauri ya mji wa Tarime limekwama kwa mara ya pili.
Hatua hiyo imesababishwa na kutokea vurugu zinazodaiwa kuwa zinafanywa na wafuasi wa Chadema wanaokataa kuwapa ushindi wagombea wa CCM wakati kura zilikua na utata.
Wafuasi wa Chadema wapinga kuapishwa kwa aliyekua mgombea wa CCM Kitongoji cha Highway,baada ya kumnyan’ganya na kuchana fomu za kiapo na kutaka aapishwe mgombea wa Chadema hali iliyozusha vurugu.
Katika vurugu hizo watu walirushiana viti,kukabana,kuvutana mashati hai iliyosababisha ukumbi kuzizima kwa fujo na kumlazimu hakimu aliyekua afanye kazi hiyo kutowaapisha wenyeviti hao ambao walipanga kuapishwa juzi baada ya zoezi hilo kushindikana Desemba 30.
NIPASHE
Polisi aliyetimuliwa kazi,Godfrey Mashumbusi amewakata mapanga na kuwajeruhi vibaya mama na mwanaye kisa wanadaiwa chupa mbili tupu za bia.
Mama huyo na mwanaye ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam walikatwa mapanga na kupigwa virungu wakiwa maeneo tofauti katika baa inayojulikana kwa jina la Itawa inayomilikiwa na askari huyo.
Mkasa huyo ulitokea Tabata Kisukuru,ulithibitishwa na kamanda wa Polisi Mkoa wa IlalaMarietha Minangi ambaye alisema chanzo ni familia hiyo kushindwa kupeleka chupa hizo kwa wakatib na kulipa deni la shilingi 10,000.
Akielezea tukio hilo mama huyo Sekela Mwiniwasa alisema alimwagiza mdogo wake bia mbili kwenye baa hiyo na siku iliyofuata alipita kwenye baa hiyo na kuulizwa kwanini hajarudisha chupa na alijibu amezisahau nyumbani ndipo akaanza kumshambulia kwa mapanga kabla ya kumfuata mtoto wake na kumfanyia hivyo hivyo.
NIPASHE
Manispaa ya Kinondoni inakusudia kufanya msako wa kufuatilia shule za awali maarufu kama chekechea ambazo hazijasajiliwa na zinazoendeshwa katika mazingira mabovu.
Ofisa Elimu wa Manispaa hiyo Kikove Takwimu alisema kuna utitiri wa shule za awali zisizofuata utaratibu wa elimu hali inayochangia kushusha viwango vya elimu kutokana na elimu hiyo kutolewa katika mazingira yasiyoridhisha.
“Ukizunguka katika jiji la Dar es salaam hasa Kinondoni utakuta shule za awali nyingi ambazo haziko kwenye mazingira ya kuridhisha ikiwa ni pamoja na kuwa karibu na barabara,gereji,baa na wakati mwingine katikati ya nyumba za watu,”alisema Takwimu.
Alisema kuwa Wizara ya Elimu na mafunzo ilitoa utaratibu wa kuanzisha shule za awali kuwa mwananchi anayetaka kuanzisha kituo hicho awe na heka tatu au zaidi ili kujenga madarasa,vyoo na viwanja vya michezo pamoja na uwepo wa hewa safi.
MWANANCHI
Rais Jakaya Kikwete ametuma ujumbe mzito dhidi ya watakaofanya vurugu ama kuvuruga uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka huu,akisema watachukuliwa hatua kali.
Kikwete ambaye anamalizia muda wake wa miaka 10 tangu akabidhiwe nchi mwaka 2005 ametoa kauli hiyo ikiwa ni wiki chache baada ya uchaguzi wa viongozi wa Serikali za mitaa kutawaliwa na vurugu na ukiukwaji wa sheria na taratibu na kusababisha Wakurugenzi sita kutenguliwaajira zao huku wengine watano wakisimamishwa kupisha uchunguzi.
Hatua za kinidhamu zilizochukuliwa na Serikali dhidi ya watu waliovuruga uchaguzi wa Serikali za mitaa mwishoni mwa mwaka jana ni ujumbe mzito kuelekea uchaguzi mkuu unaokuja“alisema Kikwete.
“Tunatuma ujumbe kuwa matukio kama haya hayatavumilika kwenye uchaguzi mkuu ujao”alisema.
MWANANCHI
Mamlaka ya hali ya Hewa Tanzania TMA imetahadharisha uwezekano wa kutokea kwa mafuriko kufuatia mvua kubwa inayotarajiwa kunyesha kwa kiwango cha zaidi ya milimita 50 katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Mkurugenzi wa TMA Agnes Kijaza alisema Mikoa inayotarajiwa kupata mvua hizo ni pamoja na Dar es salaam,Mwanza,Mtwara,Lindi,Mbeya,Iringa,Njombe,Dodoma,Singida,Ruvuma,Pwani na Morogoro.
Aliwataka wakazi wa maeneo hayo na Mamlaka zinzohusika na maafa kuchukua tahadhari stahiki ili kupunguza madhara yanayoweza kutokea.
“Mvua hizo zinatokana na kuimarika kwa mgandamizo mdogo wa hewa katika eneo la Bahari ya Hindi lililokaribu na Pwani ya Msumbuji”alisema Agnes.
MTANZANIA
Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa amesema Tanzania ni mali ya Watanzania wote na hakuna mtu mwenye hatimiliki.
Lowassa alitoa kauli hiyo kwenye ibada ya kuapishwa kwa mchungaji Solomon Misangwa wa kanisa la KKKT Dayosis ya  Kaskazini na kati kuwa askofu.
Bila kufafanua kauli hiyo Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli kupitia CCM aliliomba kanisa kuendelea kuombea amani na utulivu kwa sababu wana wajibu huo na wafanye hivyo wakitambua Tanzania ni ya Watanzania wote.
Alisema kanisa lina wajibu wa kuendelea kusaidia miradi mbalimbali linayoiendesha,lakini pia halipaswi kuacha kuiombea nchi amani huku akikumbusha msuguano uliotokea kati ya wajumbewa Bunge la Katiba wakati lilipokua likiketi kuandika katiba inayopendekezwa.
MTANZANIA
Naibu Waziri wa viwanda na Biashara Janeth Mbene, amejitosa katika sakata la sukari za magendo na kulitaka Jeshi la Polisi kufanya doria maeneo ya mipakani ili kulinda viwanda vya ndani.
Mbena alisema suala hilo ni dogo katika kulinda viwanda vya ndani na kaahidi kushirikiana na Mamlaka husika ili kuhakikisha wanaoingiza sukari hiyo wanadhibitiwa.
Ni jambo la aibu kwa baadhi ya Watanzania kuendelea kuingiza sukari kwa njia ya magendo nchini huku viwanda vya ndani vikipoteza soko,pia ajira nyingi za Watanzania zipo shakani katika viwanda vya sukari vya ndani kwa kiwango kikubwa“alisema Mbene.
Alisema uingizwaji wa sukari ya magendo kutoka nje ya nchi unakera kwa kuwa tunasaidia kutengeneza ajira za watu wa nchi za nje huku Watanzania wenzetu wakikosa ajira na kupunguzwa kazini kutokana na kile wanachokizalisha kutofika kwa mlaji moja kwa moja.
Alitaja miongoni mwa njia watakazotumia kukamata sukari inayoonekana imeingizwa nchini kinyume na utaratibu ni kuwatumia askari,TRA kupitia doria endelevu na kufanya ukaguzi katika maduka makubwa.
JAMBOLEO
Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ litaendelea kutumika endapo litahitajika sehemu yoyote duniani kwa ajili ya kusaidia kulinda amani ya watu ambao wamekua wakipoteza  maisha bila hatia kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Aidha Jeshi hilo litaendeleza mapambano dhidi ya waasi wanaopigana na majeshi ya Serikali ya Congo,Mashariki mwa nchi hiyo ili kuyatokomeza kabisa na kutoendelea kuleta madhara kwa nchi jirani.
Rais Jakaya Kikwete alisema hadi sasa Tanzania imetoa wanajeshi 3,000 kwenda UN ili kuendelea kulinda amani Congo,Durfur na Lebanon na Tanzania imekua nchi ya sita kuchagia jeshi kwa lengo la kulinda amani Afrika.
Kwa upande wa duniani JK alisema inashika nafasi ya 12 na kuheshimika barani Afrika na duniani kote hivyo sera ya mambo ya nje ni kuendeleza yale yote mazuri yaliyofanywa kwa ajili ya kutaka bara la Afrika na duniani watu waishi kwa amani.

No comments:

Post a Comment