Friday, January 2, 2015

Mkusanyiko wa zile Stori muhimu zilizoandikwa kwenye Magazeti ya leo Jan 2, 2015 Nimekuwekea hapa

HABARILEO
Mahakama ya Mkoa wa Tabora imemuhukumu Mwinjilisti wa kanisa la Menonite Ipuli kifungo cha miaka 30 kwa tuhuma za kumbaka msichana wa miaka 16.
Hakimu mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Tabora  Joctan Rushelwa alisema kifungo hicho kiwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo.
Alisema kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo hakukuwa na shaka yoyote ndio maana wameamua kutoa adhabu hiyo kwa mshtakiwa huyo.
Licha ya kutoa hukumu hiyo mshtakiwa hakuonyesha kuumizwa na adhabu hiyo hata baada ya kutakiwa kusema lolote na kusema atakata rufaa tu mara baada ya hukumu yake kutoka.
TANZANIA DAIMA
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema yeye ni mtu mwadilifu ambaye hajawahi kutoa wala kupokea rushwa kwa mtu katika maisha yake yote.
Pinda amesisitiza kwamba ana hakika kuwa hata siku moja hawezi kukamatwa kwa kosa la kupokea rushwa,isipokua kuna watu wanamchafua mara baada ya kutangaza nia yake ya kuvaa viatu vya Rais Kikwete.
Alisema kuwa wako baadhi ya watu walipanga kumchafua kwa kutaka kumsingizia wakati wa mkutano wa 16 na 17 Bungeni kwamba anahusika na uchotwaji wa fedha za Escrow.
“Nilishangaa sana watu ambao walitaka kunichafua kwa kunihusisha na fedha za Escrow,mimi sihusiki na wala sitahusika hata siku moja katika kupokea na kutoa rushwa mahali popote pale”alisisitiza Pinda.
NIPASHE
Mwanafunzi wa Darasa la pili katika shule ya msingi Ungindoni kata ya Mji mwema Dar es salaam anadaiwa kuchomwa moto na mama yake mkubwa sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kutumia jalo.
Mtoto huyo alifanyiwa ukatili huo siku ya krismasi akidaiwa kula vipande viwili vya nyama na hivyo kupewa adhabu na mama yake huyo kwa kuchomwa moto kwenye paja,mikono,magoti na miguu.
Mmoja wa shuhuda wa tukio hilo alisema  majirani walibaini kujeruhiwa kwa mtoto huyo mara baada ya kutoka nje na kuonekana akichechemea na alipoulizwa alisema amechomwa na na mama yake huku akionyesha maeneo alikofanyiwa ukatili huo.
Mama mkubwa Rachel alipoulizwa sababu ya kufanya hivyo alisema alichukua uamuzi huo baada ya kubaini alikula mboga na alipoulizwa alikana.
“Nakiri nimekosea kumpiga lakini mara kwa mara nimekua nikimuonya aache tabia ya wizi lakini amekua hasikii”alisema Rachel.
NIPASHE
Askofu msaidizi wa kanisa jimbo kuu Dar es salaam Eusebius Nzigilwa amevunja ukimya kuhusu mgao wa sh.milioni 40.4 alioupata kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya VIP Engineering& Marketing limited James Rugemalira.
Ukimya wa askofu Nzigilwa unatokana na sakata la uchotwaji wa zaidi ya bilioni 300 kutoka katika akaunti ya Tegeta Escrow iliyokua katika benki kuu ya Tanzania BoT.
Alisema kiutaratibu siyo vibaya waumini kutoa michango na matoleo kwa kanisa na watumishi wake.
Alisema aliombwa akaunti yake na Rugemarila mwanzoni mwa mwezi Februari na kwamba hakuwahi kufahamu kiasi cha fedha kilichowekwa kwenye akaunti yake hadi alipoangalia taarifa ya benki Februari 27 iliyoonyesha aliingiziwa milioni 40.4.
“Niliwasiliana na Rugemarila na kumwambia nimeona kiasi kikubwa cha fedha katika akaunti yangu,naye akaniambia hayo ni matoleo yake ambayo anaamini yatasaidia katika shughuli za kitume na kiuchungaji,,nikamshukuru kwa ukarimu huo mkubwa”alisema askofu huyo.
MTANZANIA
Siku chache baada ya kutangaza nia ya kugombea Urais katika uchaguzi mkuu,Waziri wa Nishati na Madini Lazaro Nyalandu ameadhimisha sherehe za kuuaga mwaka katika kanisa la Efatha huku mchungaji wa kanisa hilo Josephat Mwingira,akimtabiria ushindi wa safari aliyoianza.
Mwingira alisema neno hilo ni la kinabii na kusisitiza hakuna wa kumzuia kwa kuwa ukuu umeariwa juu yake.
Mwingira ambaye alisema neno hilo linatoka kwa bwana,alisisitiza kuwa vikwazo juu ya Nyalandu havitakuwepo tena.
“Hakuna atakayekuzuia tena,ni wakati wa wana wa Mungu kuinuka,hakuna atakayekukandamiza tena,mimi baba yako nitatangulia mbele yako niseme kitu,neno hili la kinabii litasababisha yale yaliyokua mbali yawe karibu na yaliyokua hayawezekani yatawezekana”alisema Nabii huyo.
MWANANCHI
Simba wanne waliotoka nje ya hifadhi ya Taifa ya Tarangire na kuingia eneo la kijiji cha Kibaoni, Manyara wameuawa kwa kuchomwa mikuki na wananchi.
Kijiji hicho kipo hatua chache kutoka ndani ya hifadhi hiyo ambayo ni mojawapo ya vivutio vya utalii wa Tanzania na mara nyingi wayamapori huzagaa mitaani hasa kipindi cha masika kuepuka majani marefu hifadhini.
Tukio hilo ambalo lilielezwa kuwa ni janga kubwa katika sekta ya utalii nchini,lilitokea jana alfajiri hadi saa 6 mchana na mizoga saba ya Simba ilipatikana  huku mmoja akiaminika kufia kwenye vichaka baada ya kukimbia alipojeruhiwa.
Waziri wa Maliasili Lazaro Nyalandu ameziagiza mamlaka zinazohusika kuwasaka na kuwatia mbaroni wahusika kuwaongoza wanakijiji hao kuua Simba hao kinyume na utaratibu.
MWANANCHI
Wakati Watanzania wengi wakiwa na matumaini ya utawala bora kwa mwaka 2015,ripoti mpya ya utafiti wa hali ya rushwa inaonyesha vitendo vya rushwa vitaendelea au kupungua ikilinganishwa na mwaka jana.
Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa na asasi ya ConcernFor Development Initiatives in Afrika ForDIA kwa kushirikiana na mtandao wa Uwazi TRAFO wananchi wanane kati ya kumi wanaamini hali ya rushwa iliongezeka mwaka jana.
Pamoja na vitendo hivyo kuendelea kuathiri maisha na upatikanaji wa huduma za jamii nchini,Watanzania tisa kati ya 100 waliripoti Takururu au Polisi hali ambayo ilitokana na wengi kutokua na imani na mamlaka hizo.
Vitendo hivyo vimeifanya Tanzania kushika nafasi ya pili katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya Burundi huku viashiria vya uwezekano wa kutokea rushwa navyo vikipanda.

Radamel Falcao kusajiliwa moja kwa moja na Man United.

Radamel Falcao celebrates scoring against Everton, his first goal for Manchester United.

Kla
bu ya Manchester United inatarajiwa kumsajili moja kwa moja mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia Radamel Falcao mara baada ya usajili wake wa mkopo kumalizika .
Falcao ambaye hadi sasa amekuwa na mabingwa hao wa zamani wa ligi ya England kwa karibu miezi mine tangu aliposajiliwa kwa mkopo akitokea klabu ya Monaco amenaza kucheza mechi mfululizo hali inayoashiria kuwa fiti kiasi cha kumshawishi kocha wa United Louis Van Gaal kuridhia kusajiliwa kwake .
Awali United walikuwa na dhamira ya kumsajili Falcao tangu awali wakati walipomchukua kwa mkopo lakini walikuwa na hofu na afya yake hasa baada ya mchezaji huyo kupata jeraha baya la goti lililomfanya akose michuano ya kombe la dunia nchini Brazil.
Hofu hiyo ilizidi pale ambapo Falcao alipata majeraha kadhaa akiwa na United hali iliyomfanya akose karibu mwezi mzima wa michezo ya ligi ya England huku kocha Louis Van Gaal akiendelea kusisitiza kuwa mchezaji huyo anahitaji kudhihirisha utimamu wake wa mwili kabla ya kupata nafasi ya uhakika kwenye kikosi cha kwanza .

Falcao anatarajiwa kusajiliwa na United kwa muda mrefu mara baada ya kumalizika kwa mkataba wake wa mkopo.
Falcao anatarajiwa kusajiliwa na United kwa muda mrefu mara baada ya kumalizika kwa mkataba wake wa mkopo.
Vipimo ambavyo Falcao amefanyiwa na wataalamu wa afya wa United vimeonyesha kuwa mchezaji huyo amerudi kwenye hali yake ya kawaida na anaweza kumudu kasi ya ligi ya England na kwa sababu hiyo kocha LVG ameridhia usajili wake .
Hivi karibuni habari toka nchini Ufaransa zinasema kuwa wakala wa Falcao Jorge Mendez amekutana na viongozi wa Monaco na viongozi wa United na tayari mipango ya kukamilisha usajili wa moja kwa moja imekamilika na United italipa Euro Milioni 40 kwa ajili ya mchezaji huyo .
Radamel_Falcao
Hadi sasa Falcao amefunga mabao mawili akiwa na United huku akianza kucheza mechi karibu zote tangu mwezi wa 12 .

unaikumbuka hii ya wariona na komba

Obama na familia yake wamesherehekea hivi kuupokea Mwaka mpya (Pichaz)

Barack Obama
Sherehe kubwa za mwaka kwa mwaka 2014 ni kama zimeisha juzi baada ya kuupokea mwaka mpya 2015, kila mmoja kasherekea kwa aina yake, Rais wa Marekani Barack Obama pamoja na familia yake nao walipata nafasi ya kutoka nje ya Ikulu ya White House na kwenda kuenjoy kama watu wengine.
Vacation ya Obama na familia yake imeendelea katika visiwa vya Hawaii, alikutana na watu mtaani akawapa salamu za mwaka mpya; “Happy New Year, everybody!“, akasalimiana nao halafu wakaendelea kula zao ice cream.
Picha zake na familia yake wakijienjoy hizi hapa.
Barack Obama
BO II
Rais Obama na mtoto wake Malia wakila Ice cream.
Rais Obama na mtoto wake Malia wakila Ice cream.
BO IV
Hawa ni watu waliopata  nafasi kuwa karibu na familia ya Obama wakienjoy Beach, Hawaii.
Hawa ni watu waliopata nafasi kuwa karibu na familia ya Obamawakienjoy Beach, Hawaii.
Meli ya watu wa usalama haikuwa mbali na familia ya Obama.
Meli ya watu wa usalama haikuwa mbali na familia ya Obama

Umesoma makubwa yaliyoandikwa na Magazeti ya Tanzania leo Jan 2?Yako hapa

princerobert
 Kama kawaida ya princeroberthamisi.blogspot inakupa vichwa vya habari vya magazeti yote ya kila siku. Leo pia kuna headlines mpya kwenye magazeti mbalimbali. Chukua muda wako kupitia kila kilichoandikwa kwenye kurasa za mbele za magazeti ya leo.

Thursday, January 1, 2015

Radamel Falcao kusajiliwa moja kwa moja na Man United

Radamel Falcao celebrates scoring against Everton, his first goal for Manchester United.
Klabu ya Manchester United inatarajiwa kumsajili moja kwa moja mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia Radamel Falcao mara baada ya usajili wake wa mkopo kumalizika .
Falcao ambaye hadi sasa amekuwa na mabingwa hao wa zamani wa ligi ya England kwa karibu miezi mine tangu aliposajiliwa kwa mkopo akitokea klabu ya Monaco amenaza kucheza mechi mfululizo hali inayoashiria kuwa fiti kiasi cha kumshawishi kocha wa United Louis Van Gaal kuridhia kusajiliwa kwake .
Awali United walikuwa na dhamira ya kumsajili Falcao tangu awali wakati walipomchukua kwa mkopo lakini walikuwa na hofu na afya yake hasa baada ya mchezaji huyo kupata jeraha baya la goti lililomfanya akose michuano ya kombe la dunia nchini Brazil.
Hofu hiyo ilizidi pale ambapo Falcao alipata majeraha kadhaa akiwa na United hali iliyomfanya akose karibu mwezi mzima wa michezo ya ligi ya England huku kocha Louis Van Gaal akiendelea kusisitiza kuwa mchezaji huyo anahitaji kudhihirisha utimamu wake wa mwili kabla ya kupata nafasi ya uhakika kwenye kikosi cha kwanza .

Falcao anatarajiwa kusajiliwa na United kwa muda mrefu mara baada ya kumalizika kwa mkataba wake wa mkopo.
Falcao anatarajiwa kusajiliwa na United kwa muda mrefu mara baada ya kumalizika kwa mkataba wake wa mkopo.
Vipimo ambavyo Falcao amefanyiwa na wataalamu wa afya wa United vimeonyesha kuwa mchezaji huyo amerudi kwenye hali yake ya kawaida na anaweza kumudu kasi ya ligi ya England na kwa sababu hiyo kocha LVG ameridhia usajili wake .
Hivi karibuni habari toka nchini Ufaransa zinasema kuwa wakala wa Falcao Jorge Mendez amekutana na viongozi wa Monaco na viongozi wa United na tayari mipango ya kukamilisha usajili wa moja kwa moja imekamilika na United italipa Euro Milioni 40 kwa ajili ya mchezaji huyo .
Radamel_Falcao
Hadi sasa Falcao amefunga mabao mawili akiwa na United huku akianza kucheza mechi karibu zote tangu mwezi wa 12 .

Simba kumtambulisha mrithi wa Phiri.

Klabu ya Simba ya jijini Dar-es-salaam iko mbioni kuingia mkataba ba kocha mpya kutoka Serbia baada ya kumalizana na kocha Mzambia Patrick Phiri ambaye alifukuzwa kazi siku chache zilizopita .
Kocha huyo Goran Kapunovic aliingia nchini Tanzania akitua kwenye uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere hapo jana saa 1 asubuhi na alikuja kupokewa na viongozi wa Simba akiwemo mjumbe wa timu hiyo Colin Firsch .
Simba ilimfukuza Phiri mapema wiki hii baada ya klabu hiyo kutoridhika na kiwango cha timu hiyo kufuatia mfululizo wa matokeo mabaya hasa kwenye mchezo wake wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar ambapo wekundu wa msimbazi walifungwa 1-0 .
Moja ya vichwa vya habari vya magazeti ya michezo hapa nchini ambavyo vimebeba 'story' kuhusu kocha mpya wa Simba.
Moja ya vichwa vya habari vya magazeti ya michezo hapa nchini ambavyo vimebeba story kuhusu kocha mpya wa Simba.
Simba kwa sasa iko visiwani Zanzibar ambako inashiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi huku ikiwa chini ya kocha msaidizi wa timu hiyo Suleiman Matola ambaye ataiongoza timu hiyo hadi hapo kocha mpya atakapoungana rasmi na kikosi chao.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kilichomo ndani ya klabu hiyo ambacho hakikuwa tayari kunukuliwa Phiri tayari ameagana na wachezaji wa timu hiyo baada ya maamuzi ya kuachana nae.
Goran Kopunovic (wa pili upande wa kushoto kwenye mstari wa mwisho) akiwa na kikosi cha klabu ya Ferencvaros ya nchini Hungary kwenye msimu wa mwaka 1995/96.
Goran Kopunovic (wa pili upande wa kushoto kwenye mstari wa mwisho) akiwa na kikosi cha klabu ya Ferencvaros ya nchini Hungary kwenye msimu wa mwaka 1995/96.
Kocha huyo mpya ni raia wa Serbia na aliwahi kucheza kwenye michuano mikubwa ya ligi ya mabingwa barani Ulaya akiwa na timu ya Ferencvaros ya nchini Hungary na mara ya mwisho alikuwa amefundisha klabu ya Polisi ya huko Rwanda.
Simba itaingia uwanjani usiku wa leo kucheza mechi yake ya kwanza ya kombe la mapinduzi dhidi ya timu ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar.

Mkusanyiko wa Stori zilizopewa Headlines kwenye Magazeti ya leo Tanzania January 1, 2015

TANZANIA DAIMA
Mbunge wa Kigoma  Kusini David Kafulila amesema kuwa mwaka 2015 ni mgumu kwani Serikali ipo taabani kifedha kiasi cha kusitisha kandarasi ya barabara kutokana na ukata.
Alisema Mamlaka ya Mapato Tanzania wanakusanya bilioni 800 kwa mwezi wakati mahitaji ya mishahara pekee ni takribani bilioni 500 na kwamba kiasi cha bilioni 300 kinachosalia hakitoshi hata kununua karatasi na mafuta ya kuendesha ofisi za Serikali nchi nzima.
Alisema Serikali iko katika hali mbaya wakati iko kwenye kutaka kutekeleza mambo makubwa yanayohitaji fedha uku mwaka huu ukiwa ni wa uchaguzi ambao ni muhimu kwa nchi yoyote duniani.
MTANZANIA
Hali si shwari ndani ya chama cha Alliance for Change ACT baada ya kuwafukuza uanachama aliyekua Katibu mkuu wake Samson Mwigambana mshauri wa chama hicho Profesa Kitila Mkumbo.
Mbali na hao viongozi wengine waliovuliwa nyadhifa zao ni pamoja na aliyekua Makamu Mwenyekiti bara Shabaan Mambo,Mwenyekiti wa Wazee Wilson Muchumbusi na katibu wa vijana Philip Malaki.
Mwenyekiti wa ACT Kadawi Lukas alisema  uamuzi huo umefikiwa baada ya kuitishwa kikao cha kamati kuu kilichofanyika jana.
Tumewavua uongozo na kuwafukuza uanachama Kitila na Mwigamba kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya kutumia madaraka vibaya kwa kukabidhi chama kwa mafisadi.
Alisema viongozi hao walisaini makubaliano ya kuendesha shughuli za chama  ikiwemo kusimamia mikutano na uchaguzi bila kushirikisha viongozi wengine.
NIPASHE
Ulazaji wa bomba la maji la Mamlaka ya majisafi na majitaka Dar es salaam Dawasa katika mradi wa Ruvu chini kuanzia Bagamoyo hadi Dar umekamilika kwa asilimia 93.
Mradi huo unatarajiwa kukamilika March na utakua ukitoa maji lita milioni 270 kwa siku katika maeneo mbalimbali ya Jiji na sehemu ambazo bomba linapita.
Dawasa imesema kuwa mradi huo umefikia hatua hiyo baada ya jitihada za  kutatua mgogoro huo  kwa kuzungumza na wakazi ambao bomba hilo linapita ambao walifungua kesi mahakamani kuupinga wakidai walipwe fidia.
Menejamradi huo Romanus Mwangingo alisema kuwa mradi huo unatazamiwa kukamilika baada ya kulaza bomba katika maeneo yote.
NIPASHE
Mbunge waviti maalum kupitia UVCCM Mkoa wa Arusha Catherine Magige amelalamikiwa kwa kuwagombanisha viongozi wa Jumuiya ya wanawake UWT Mkoa wa Arusha  kutokana na kinachodaiwa kuwa ni mbio zake za ubunge kupitia Jumuiya hiyo.
Mgongano huo unadaiwa kutokana na ukiukwaji wa kanuni  kilichofanywa na Mbunge huyo kwa kugawa zawadiza vitenge na mchele kwa ajili ya sikukuu za Krismass kwa viongozi wa Jumuiya hiyo bila kuutaarifu uongozi wa juu.
Pia kamati hiyo imemfungia ofisi Katibu wake Stamil Dendegu kwa tuhuma za kumruhusu Magige kugawa zawadi na kumkaimisha  ofisi katibu wa UWT Wilaya ya Arusha Fatma Hassan.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Arusha Flora Zelote alikanusha kusimamishwa kazi kwa katibu wake wala kuwepo kwa kikao kilichomjadili yeye.
NIPASHE
Siku chache baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu kutangaza nia ya kuwania Urais, Sheikh Shariff Matongo ameibuka na kusema mmoja wa viongozi anayewania nafasi hiyo ya juu atafariki dunia.
Sheikh Shariff alitoa utabiri huo  juu ya ndoto zilizomjia usiku na kuoteshwa mambo zaidi ya matano yatakayoikabili nchi mwaka huu.
Alisema atakayefariki dunia ni yule mgombea anayewania nafasi ya urais ambaye alishawahi kuwa kiongozi katika nyadhifa mbalimbali kupitia CCM.
Ndoto yangu nilioteshwa sikukaa nayo peke yangu niliwaeleza Masheikh mbalimbali kutoka Abu Dhabi, Nigeria na kupata ushauri wao na wakaniambia suala hilo nisikae nalo bali niwashirikishe Watanzania wenzangu“alisema.
MWANANCHI
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge yahesabu za Serikali Zitto Kabwe amesema atamuunga mkono kiongozi wa kambi ya upinzani Freeman Mbowe pale atakapowasilisha hoja yake bungeni kuhusu ufisadi wa zaidi ya trilioni 1 katika mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam.
Najua bado mnalia kuhusu bombala kupeleka gesi Dar es salaam,machozi yenu yatafutika kwani tayari habari ya ufisadi mkubwa katika ujenzi wa bomba hilo zimeanza kuchomoza.”– Zitto.
Kiongozi wa Upinzani Mbowe ametamka mara kadhaa kuwa atatoa hoja kuhusu ufisadi kuhusu ujenzi wa bomba hilo,na pale atakapohitaji msaada wetu tutamsaidia,tunaamini gharama za mradi huu zimezishwa mara mbili na inawezekana kabisa kuwa zaidi ya dola milioni 600 sawa na zaidi ya trilion 1“alisema Zitto.
Alisema katika miakaya hivi karibuni Mkoa wa Mtwara umechukua sura mpya baada ya kugundulika kuwa na gesi na wananchi wameonekana kuwa wanaweza kupigania maslahi ya Taila lao.
MWANANCHI
Timu ya Makachero wa Polisi kutoka Dar es salaam imewasili Mwanza kuongeza nguvu za kumsaka mtoto mlemavu wa ngozi Pendo Emmanuel anyesadikiwa kutekwa akiwa nyumbani kwao.
Polisi wametangaza dau la milioni 3 kwa atakayewezesha kutoa taarifa za waliohusika kufanya tukio hilo la kumteka mtoto huyo.
Hata hivyo taarifa zilipatikana jana zinasema tayari watu sita wameshikiliwa na polisi wakishusishwa na tukio hilo akiwemo baba wa mtoto huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Valentino Mlowola  ataiongoza timu hiyo inayowashirikisha pia Makachero wa Mkoani Mwanza kuhakikisha mtoto huyo anapatikana aidha akiwa amekufa ama akiwa hai.

Mkusanyiko wa Stori zilizopewa Headlines kwenye Magazeti ya leo Tanzania January 1, 2015

TANZANIA DAIMA
Mbunge wa Kigoma  Kusini David Kafulila amesema kuwa mwaka 2015 ni mgumu kwani Serikali ipo taabani kifedha kiasi cha kusitisha kandarasi ya barabara kutokana na ukata.
Alisema Mamlaka ya Mapato Tanzania wanakusanya bilioni 800 kwa mwezi wakati mahitaji ya mishahara pekee ni takribani bilioni 500 na kwamba kiasi cha bilioni 300 kinachosalia hakitoshi hata kununua karatasi na mafuta ya kuendesha ofisi za Serikali nchi nzima.
Alisema Serikali iko katika hali mbaya wakati iko kwenye kutaka kutekeleza mambo makubwa yanayohitaji fedha uku mwaka huu ukiwa ni wa uchaguzi ambao ni muhimu kwa nchi yoyote duniani.
MTANZANIA
Hali si shwari ndani ya chama cha Alliance for change ACT baada ya kuwafukuza uanachama aliyekua Katibu mkuu wake Samson Mwigambana mshauri wa chama hicho Profesa Kitila Mkumbo.
Mbali na hao viongozi wengine waliovuliwa nyadhifa zao ni pamoja na aliyekua Makamu Mwenyekiti bara Shabaan Mambo,Mwenyekiti wa Wazee Wilson Muchumbusi na katibu wa vijana Philip Malaki.
Mwenyekiti wa ACT Kadawi Lukas alisema  uamuzi huo umefikiwa baada ya kuitishwa kikao cha kamati kuu kilichofanyika jana.
“Tumewavua uongozo na kuwafukuza uanachama Kitila na Mwigamba kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya kutumia madaraka vibaya kwa kukabidhi chama kwa mafisadi.
Alisema viongozi hao walisaini makubaliano ya kuendesha shughuli za chama  ikiwemo kusimamia mikutano na uchaguzi bila kushirikisha viongozi wengine.
NIPASHE
Ulazaji wa bomba la maji la Mamlaka ya majisafi na majitaka Dar es salaam Dawasa katika mradi wa Ruvu chini kuanzia Bagamoyo hadi Dar umekamilika kwa asilimia 93.
Mradi huo unatarajiwa kukamilika Machi na utakua ukitoa maji lita milioni 270 kwa siku katika maeneo mbalimbali ya Jiji na sehemu ambazo bomba linapita.
Dawasa imesema kuwa mradi huo umefikia hatua hy baada ya jitihada za  kutatua mgogoro huo  kwa kuzungumza na wakazi ambao bomba hilo linapita ambao walifungua kesi mahakamani kuupinga wakidai walipwe fidia.
Menejamradi huo Romanus Mwangingo alisema kuwa mradi huo unatazamiwa kukamilika baada ya kulaza bomba katika maeneo yote.
NIPASHE
Mbunge waviti maalum kupitia UVCCM Mkoa wa Arusha Catherine Magige amelalamikiwa kwa kuwagombanisha viongozi wa Jumuiya ya wanawake UWT Mkoa wa Arusha  kutokana na kinachodaiwa kuwa ni mbio zake za ubunge kupitia Jumuiya hiyo.
Mgongano huo unadaiwa kutokana na ukiukwaji wa kanuni  kilichofanywa na Mbunge huyo kwa kugawa zawadiza vitenge na mchele kwa ajili ya sikukuu za Krismass kwa viongozi wa Jumuiya hiyo bila kuutaarifu uongozi wa juu.
Pia kamati hiyo imemfungia ofisi Katibu wake Stamil Dendegu kwa tuhuma za kumruhusu Magige kugawa zawadi na kumkaimisha  ofisi katibu wa UWT Wilaya ya Arusha Fatma Hassan.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Arusha Flora Zelote alikanusha kusimamishwa kazi kwa katibu wake wala kuwepo kwa kikao kilichomjadili yeye.
NIPASHE
Siku chache baada ya Waziri wa Maliasiki na Utalii Lazaro Nyalandu kutangaza nia ya kuwania Urais,Sheikh Shariff Matongo ameibuka na kusema mmoja wa viongozi anayewania nafasi hiyo ya juu atafariki dunia.
Sheikh Shariff alitoa utabiri huo  juu ya ndoto zilizomjia usiku na kuoteshwa mambo zaidi ya matano yatakayoikabili nchi mwaka huu.
Alisema atakayefariki dunia ni yule mgombea anayewania nafasi ya urais ambaye alishawahi kuwa kiongozi katika nyadhifa mbalimbali kupitia CCM.
“Ndoto yangu nilioteshwa sikukaa nayo peke yangu niliwaeleza Masheikh mbalimbali kutoka Abu Dhabi,Nigeria na kupata ushauri wao na wakaniambia suala hilo nisikae nalo bali niwashirikishe Watanzania wenzangu”alisema.
MWANANCHI
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge yahesabu za Serikali Zitto Kabwe amesema atamuunga mkono kiongozi wa kambi ya upinzani Freeman Mbowe pale atakapowasilisha hoja yake bungeni kuhusu ufisadi wa zaidi ya trilioni 1 katika mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam.
“Najua bado mnalia kuhusu bombala kupeleka gesi Dar es salaam,machozi yenu yatafutika kwani tayari habari ya ufisadi mkubwa katika ujenzi wa bomba hilo zimeanza kuchomoza.
“Kiongozi wa Upinzani Mbowe ametamka mara kadhaa kuwa atatoa hoja kuhusu ufisadi kuhusu ujenzi wa bomba hilo,na pale atakapohitaji msaada wetu tutamsaidia,tunaamini gharama za mradi huu zimezishwa mara mbili na inawezekana kabisa kuwa zaidi ya dola milioni 600 sawa na zaidi ya trilion 1″alisema Zitto.
Alisema katika miakaya hivi karibuni Mkoa wa Mtwara umechukua sura mpya baada ya kugundulika kuwa na gesi na wananchi wameonekana kuwa wanaweza kupigania maslahi ya Taila lao.
MWANANCHI
Timu ya Makachero wa Polisi kutoka Dar es salaam imewasili Mkoani Mwanza kuongeza nguvu za kumsaka mtoto mlemavu wa ngozi Pendo Emmanuel anyesadikiwa kutekwa akiwa nyumbani kwao.
Polisi wametangaza dau la milioni 3 kwa atakayewezesha kutoa taarifa za waliohusika kufanya tukio hilo la kumteka mtoto huyo.
Hata hivyo taarifa zilipatikana jana zinasema tayari watu sita wameshikiliwa na polisi wakishusishwa na tukio hilo akiwemo baba wa mtoto huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Valentino Mlowola  ataiongoza timu hiyo inayowashirikisha pia wamachero wa Mkoani Mwanza kuhakikisha mtoto huyo anapatikana aidha akiwa amekufa ama akiwa hai.

Zitto Kabwe kuhusu Serikali kutekeleza maazimio yaliyotolewa na Bunge…

Mbunge wa Zitto Kabwe leo amewahutubia Wananchi wa Mtwara kupitia mkutano ulioitishwa na chama cha Wananchi CUF na kutoa ufafanuzi juu ya sakata la account ya Tegeta Escrow.
Akizungumzia sakata hilo Zitto Kabwe amesema kuwa baadhi ya viongozi waliohusika na sakata hilo ambao mpaka hivi sasa hawajachukuliwa hatua yoyote lazima wachukuliwe kwa kuwa serikali haiwezi kupingana na maazimio ya bunge.
“ Utekelezaji wa maamuzi ya Bunge hauna mjadala… sisi kama Wabunge wa Kambi ya Upinzani mwezi January kazi ya kwanza ni kupokea taarifa ya utekelezaji wa maamuzi ya Bunge… Tunachokitaka kila mtu aliyehusika kwenye Escrow ni lazima awajibike…“– Zitto Kabwe.
Sisi lazima tuutumie mwaka 2015 kama mwaka wa uwajibishaji, mwaka wa kuwajibishana… safari hii mmewawajibisha kwenye Seikali za Mitaa, hongereni sana, tunaenda kuwawajibisha kwenye Serikali kuu sasa…”– Zitto Kabwe.

Mwaka Mpya: Maafa China 35 wafariki

Umatti wa watu waliokanyagana na wengine kufa nchini China wakati wakiupokea mwaka mpya 2015
Sherehe za kuupokea mwaka mpya 2015 zimeguka kuwa majonzi baada ya watu thelathini na watano kufa kwenye taharuki ya kukanyagana kwenye msongamano wakati wakiiupokea mwaka mpya.
Maafa hayo yametokea katika mji Shanghai ambapo maelfu ya watu walikuwa wamekusanyika ili kuupokea mwaka mpya.
Chanzo cha taharuki hiyo bado haijafamika lakini vyombo vya habari vya nchi hiyo vimenukuliwa vikisema imetokana na maelfu ya watu kuzuiwa kugombea fedha bandia zilizotupwa eneo hilo kutoka katika jengo moja.

presentation za funga mwaka ija

Papa: Mwaka mpya akemea ufisadi Roma

Papa Francis
Akizungumza katika Kanisa kuu la St. Peter Basilica, papa amesema rushwa ni shumbulizi dhidi ya maskini na wasiokuwa na uwezo ambapo ametaka mabadiliko ya kiroho na kimaadili katika mji huo.
Papa ambaye ndiye Askofu wa Rome amefanya utetezi dhidi ya maskini kama nguzo muhimu katika uongozi wake wa upapa.
Maafisa wa polisi kwa sasa wanawachunguza maafisa wa Roma wanaotuhumiwa kujihusisha na kundi la Mafia na ufisadi dhidi ya fedha za umma zikiwemo zilizotengwa kwa ajili ya kituo wahamiaji.

MOROGORO WASHEREKEA MKESHA WA MWAKA MPYA KWENYE MAFURIKO

morogoro
Mvua kubwa zilizonyesha kwa muda mfupi mjini Morogoro zimesababisha mafuriko baadhi ya barabara kushindwa kupitika na maji kujaa katika baadhi ya maduka. Wakazi wa mji wa Morogoro wakizungumzia mafuriko hayo wamelalamikia miundombinu mibovu ya barabara kutokana na kuziba kwa mitaro ambapo wameitaka halmasauri ya mji wa Morogoro kuzibua mitaro hiyo huku baadhi ya wafanyabiashara wakilalamikia kupata hasara.Katika hatua nyingine mto Kikundi uliopo mjini Morogoro umepoteza uelekeo na kumwaga maji katika soko kuu la mji wa Morogoro na kusababisha maji kujaa katika maduka huku baadhi ya magari yakiingia kwenye mitaro na baadhi ya bodaboda zikiwa na abiria zime zama katika maji na kulazimika kuvutwa.Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Morogoro Phimlemon Magesa akizungumzia alalamiko hayo ya wananchi hao amesema manispaa wanajitahidi kufanya usafi lakini tatizo liko kwa wananchi wenyewe kutupa taka kwenye mitaro na kusabisha mitaro hiyo kuziba na maji kupoteza ueleko na kujaa katika makazi ya wananchi.

Mfalme Abdullah wa Saudia alazwa

Mfalme Abdullah wa saudia alazwa hospitalini
Mfalme Abdullah wa Saud Arabia amelazwa hospitalini ili kufanyiwa ukaguzi.
Taarifa kutoka kwa makao ya mfalme huyo haikutoa maelezo yoyote kuhusu hali yake.
Soko la hisa la Saudia lilianguka baada ya habari hizo kutangazwa katikan runinga ya taifa.
Mfalme Abdullah aliye na umri wa miaka 90 ametawala ufalme wa taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta tangu mwaka 2005.

Tanzania imechaguliwa na shirikisho la mpira wa wavu Afrika (CAVB) kuwa wenyeji wa michuano ya kanda ya Tano ya Beach Volleyball ( mpira wa wavu ufukweni).

mazoezi yakiendelea

Michuano hiyo itakayofanyika kuanzia February 16-18 mwakani itakuwa ni sehemu ya kufuzu kwa michuano ya Olimpiki itakayofanyika Rio de Janeiro, Brazil mwaka 2016.
Mkurugenzi wa Kamisheni ya wavu ufukweni, Muharrami Mchume amesema wapo tayari kwa uwenyeji na kuongeza kuwa Kenya, Burundi, Somalia, Ethiopia, Djibouti na wenyeji Tanzania ndio nchi zitakazoshiriki.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuwa wenyeji wa michuano hiyo.
Mchezo wa mpira wa wavu sio maarufu sana nchini Tanzania licha ya kuwa na fukwe nyingi za bahari.
CAVB ipo katika jitihada za kuendeleza mchezo huo wa ufukweni na hivi karibuni liliendesha semina nchini Tanzania ambayo ilishirikisha washiriki kutoka zaidi ya nchi tano katika jitihada za kuukuza mchezo huo katika nchi za kanda ya tano hasa mashuleni.
Michuano hiyo inategemewa kufanyika katika fukwe za beach ya Mbalamwezi jijini Dar es Salaam.