Thursday, January 1, 2015

Simba kumtambulisha mrithi wa Phiri.

Klabu ya Simba ya jijini Dar-es-salaam iko mbioni kuingia mkataba ba kocha mpya kutoka Serbia baada ya kumalizana na kocha Mzambia Patrick Phiri ambaye alifukuzwa kazi siku chache zilizopita .
Kocha huyo Goran Kapunovic aliingia nchini Tanzania akitua kwenye uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere hapo jana saa 1 asubuhi na alikuja kupokewa na viongozi wa Simba akiwemo mjumbe wa timu hiyo Colin Firsch .
Simba ilimfukuza Phiri mapema wiki hii baada ya klabu hiyo kutoridhika na kiwango cha timu hiyo kufuatia mfululizo wa matokeo mabaya hasa kwenye mchezo wake wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar ambapo wekundu wa msimbazi walifungwa 1-0 .
Moja ya vichwa vya habari vya magazeti ya michezo hapa nchini ambavyo vimebeba 'story' kuhusu kocha mpya wa Simba.
Moja ya vichwa vya habari vya magazeti ya michezo hapa nchini ambavyo vimebeba story kuhusu kocha mpya wa Simba.
Simba kwa sasa iko visiwani Zanzibar ambako inashiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi huku ikiwa chini ya kocha msaidizi wa timu hiyo Suleiman Matola ambaye ataiongoza timu hiyo hadi hapo kocha mpya atakapoungana rasmi na kikosi chao.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kilichomo ndani ya klabu hiyo ambacho hakikuwa tayari kunukuliwa Phiri tayari ameagana na wachezaji wa timu hiyo baada ya maamuzi ya kuachana nae.
Goran Kopunovic (wa pili upande wa kushoto kwenye mstari wa mwisho) akiwa na kikosi cha klabu ya Ferencvaros ya nchini Hungary kwenye msimu wa mwaka 1995/96.
Goran Kopunovic (wa pili upande wa kushoto kwenye mstari wa mwisho) akiwa na kikosi cha klabu ya Ferencvaros ya nchini Hungary kwenye msimu wa mwaka 1995/96.
Kocha huyo mpya ni raia wa Serbia na aliwahi kucheza kwenye michuano mikubwa ya ligi ya mabingwa barani Ulaya akiwa na timu ya Ferencvaros ya nchini Hungary na mara ya mwisho alikuwa amefundisha klabu ya Polisi ya huko Rwanda.
Simba itaingia uwanjani usiku wa leo kucheza mechi yake ya kwanza ya kombe la mapinduzi dhidi ya timu ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar.

No comments:

Post a Comment