HABARILEO
Mahakama ya Mkoa wa Tabora imemuhukumu Mwinjilisti wa kanisa la Menonite Ipuli kifungo cha miaka 30 kwa tuhuma za kumbaka msichana wa miaka 16.
Hakimu mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Tabora Joctan Rushelwa alisema kifungo hicho kiwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo.
Alisema kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo hakukuwa na shaka yoyote ndio maana wameamua kutoa adhabu hiyo kwa mshtakiwa huyo.
Licha ya kutoa hukumu hiyo mshtakiwa hakuonyesha kuumizwa na adhabu hiyo hata baada ya kutakiwa kusema lolote na kusema atakata rufaa tu mara baada ya hukumu yake kutoka.
TANZANIA DAIMA
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema yeye ni mtu mwadilifu ambaye hajawahi kutoa wala kupokea rushwa kwa mtu katika maisha yake yote.
Pinda amesisitiza kwamba ana hakika kuwa hata siku moja hawezi kukamatwa kwa kosa la kupokea rushwa,isipokua kuna watu wanamchafua mara baada ya kutangaza nia yake ya kuvaa viatu vya Rais Kikwete.
Alisema kuwa wako baadhi ya watu walipanga kumchafua kwa kutaka kumsingizia wakati wa mkutano wa 16 na 17 Bungeni kwamba anahusika na uchotwaji wa fedha za Escrow.
“Nilishangaa sana watu ambao walitaka kunichafua kwa kunihusisha na fedha za Escrow,mimi sihusiki na wala sitahusika hata siku moja katika kupokea na kutoa rushwa mahali popote pale”alisisitiza Pinda.
NIPASHE
Mwanafunzi wa Darasa la pili katika shule ya msingi Ungindoni kata ya Mji mwema Dar es salaam anadaiwa kuchomwa moto na mama yake mkubwa sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kutumia jalo.
Mtoto huyo alifanyiwa ukatili huo siku ya krismasi akidaiwa kula vipande viwili vya nyama na hivyo kupewa adhabu na mama yake huyo kwa kuchomwa moto kwenye paja,mikono,magoti na miguu.
Mmoja wa shuhuda wa tukio hilo alisema majirani walibaini kujeruhiwa kwa mtoto huyo mara baada ya kutoka nje na kuonekana akichechemea na alipoulizwa alisema amechomwa na na mama yake huku akionyesha maeneo alikofanyiwa ukatili huo.
Mama mkubwa Rachel alipoulizwa sababu ya kufanya hivyo alisema alichukua uamuzi huo baada ya kubaini alikula mboga na alipoulizwa alikana.
“Nakiri nimekosea kumpiga lakini mara kwa mara nimekua nikimuonya aache tabia ya wizi lakini amekua hasikii”alisema Rachel.
NIPASHE
Askofu msaidizi wa kanisa jimbo kuu Dar es salaam Eusebius Nzigilwa amevunja ukimya kuhusu mgao wa sh.milioni 40.4 alioupata kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya VIP Engineering& Marketing limited James Rugemalira.
Ukimya wa askofu Nzigilwa unatokana na sakata la uchotwaji wa zaidi ya bilioni 300 kutoka katika akaunti ya Tegeta Escrow iliyokua katika benki kuu ya Tanzania BoT.
Alisema kiutaratibu siyo vibaya waumini kutoa michango na matoleo kwa kanisa na watumishi wake.
Alisema aliombwa akaunti yake na Rugemarila mwanzoni mwa mwezi Februari na kwamba hakuwahi kufahamu kiasi cha fedha kilichowekwa kwenye akaunti yake hadi alipoangalia taarifa ya benki Februari 27 iliyoonyesha aliingiziwa milioni 40.4.
“Niliwasiliana na Rugemarila na kumwambia nimeona kiasi kikubwa cha fedha katika akaunti yangu,naye akaniambia hayo ni matoleo yake ambayo anaamini yatasaidia katika shughuli za kitume na kiuchungaji,,nikamshukuru kwa ukarimu huo mkubwa”alisema askofu huyo.
MTANZANIA
Siku chache baada ya kutangaza nia ya kugombea Urais katika uchaguzi mkuu,Waziri wa Nishati na Madini Lazaro Nyalandu ameadhimisha sherehe za kuuaga mwaka katika kanisa la Efatha huku mchungaji wa kanisa hilo Josephat Mwingira,akimtabiria ushindi wa safari aliyoianza.
Mwingira alisema neno hilo ni la kinabii na kusisitiza hakuna wa kumzuia kwa kuwa ukuu umeariwa juu yake.
Mwingira ambaye alisema neno hilo linatoka kwa bwana,alisisitiza kuwa vikwazo juu ya Nyalandu havitakuwepo tena.
“Hakuna atakayekuzuia tena,ni wakati wa wana wa Mungu kuinuka,hakuna atakayekukandamiza tena,mimi baba yako nitatangulia mbele yako niseme kitu,neno hili la kinabii litasababisha yale yaliyokua mbali yawe karibu na yaliyokua hayawezekani yatawezekana”alisema Nabii huyo.
MWANANCHI
Simba wanne waliotoka nje ya hifadhi ya Taifa ya Tarangire na kuingia eneo la kijiji cha Kibaoni, Manyara wameuawa kwa kuchomwa mikuki na wananchi.
Kijiji hicho kipo hatua chache kutoka ndani ya hifadhi hiyo ambayo ni mojawapo ya vivutio vya utalii wa Tanzania na mara nyingi wayamapori huzagaa mitaani hasa kipindi cha masika kuepuka majani marefu hifadhini.
Tukio hilo ambalo lilielezwa kuwa ni janga kubwa katika sekta ya utalii nchini,lilitokea jana alfajiri hadi saa 6 mchana na mizoga saba ya Simba ilipatikana huku mmoja akiaminika kufia kwenye vichaka baada ya kukimbia alipojeruhiwa.
Waziri wa Maliasili Lazaro Nyalandu ameziagiza mamlaka zinazohusika kuwasaka na kuwatia mbaroni wahusika kuwaongoza wanakijiji hao kuua Simba hao kinyume na utaratibu.
MWANANCHI
Wakati Watanzania wengi wakiwa na matumaini ya utawala bora kwa mwaka 2015,ripoti mpya ya utafiti wa hali ya rushwa inaonyesha vitendo vya rushwa vitaendelea au kupungua ikilinganishwa na mwaka jana.
Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa na asasi ya ConcernFor Development Initiatives in Afrika ForDIA kwa kushirikiana na mtandao wa Uwazi TRAFO wananchi wanane kati ya kumi wanaamini hali ya rushwa iliongezeka mwaka jana.
Pamoja na vitendo hivyo kuendelea kuathiri maisha na upatikanaji wa huduma za jamii nchini,Watanzania tisa kati ya 100 waliripoti Takururu au Polisi hali ambayo ilitokana na wengi kutokua na imani na mamlaka hizo.
Vitendo hivyo vimeifanya Tanzania kushika nafasi ya pili katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya Burundi huku viashiria vya uwezekano wa kutokea rushwa navyo vikipanda.
No comments:
Post a Comment