Wednesday, December 31, 2014

AJALI YA MOTO HANDENI

Lori la mafuta likiteketea kwa moto mara baada ya kugonga nguzo ya umeme maeneo ya Amasia huko Handeni mkoani Tanga 


Wananchi wakishuhudia moto mkubwa uliozuka katika ajali hiyo

CCM kutumia panga la 2005


Dar es Salaam. Vigezo 13 vilivyowekwa na CCM katika Uchaguzi Mkuu wa 2005 kumpima mwanachama anayefaa kugombea urais, ndivyo vitakavyotumika kuwaengua makada wanaoendelea kujitokeza kuwania nafasi hiyo mwakani, imefahamika.
Vigezo hivyo vinaonekana kuwa kizingiti kwa baadhi ya makada wa chama hicho ambao tayari wametangaza na wengine wanaotajwa kutaka nafasi hiyo ya juu nchini, ukiachilia mbali mnyukano unaotarajiwa kutoka vyama vya upinzani vinavyoonekana kupata nguvu.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula amelithibitishia gazeti hili kwamba, “Sifa hizo 13 zilizotumika mwaka 2005 na 2010 ndizo zitakazotumika pia mwaka 2015 na wala hakutakuwa na maboresho wala nyongeza ya aina yoyote.”
Vigezo hivyo viliwekwa ili kuhakikisha chama hicho kinampata mgombea asiyetiliwa shaka juu ya vitendo vya uadilifu, mwenye uzoefu wa uongozi serikalini, atakayedumisha muungano, mwenye upeo wa masuala ya kimataifa, mtetezi wa wanyonge, asiyejilimbikizia mali na mwajibikaji, mambo ambayo hata hivyo, bado yameibua mjadala iwapo yanazingatiwa au la.
Pia anayetakiwa lazima awe mwenye kuzitetea sera za CCM, anayekubalika na wananchi, asiye na hulka ya udikteta au ufashisti, mwenye uwezo wa kufanya uamuzi wa busara na kiwango cha elimu ya chuo kikuu au inayolingana nayo.
Licha ya vigezo hivyo, baadhi ya makada waliokwishajitokeza na wengine wanaotajwa wanaonekana dhahiri kukosa baadhi sifa hizo na wengine wako ‘kifungoni’ kwa miezi 12 baada ya kupewa onyo kali kwa kufanya kampeni mapema na kujihusisha na vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya chama na jamii.
Vigogo wa CCM ambao wanatajwa kutaka kupewa ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho ambao iwapo watachukua fomu, watatazamwa kwa vigezo hivyo ni Mbunge wa Nzega, Dk Khamis Kigwangalla, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba ambao wamekwishatangaza kuwania nafasi hiyo.
Wengine ambao wanatajwa ingawa hawajatangaza nia hadharani ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa; Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa; Bernard Membe; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu); Stephen Wasira na aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.
Wachambuzi wanavyosema
Akizungumzia vigezo hivyo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Danford Kitwana alisema CCM inajua kuwa hakuna mgombea anayeweza kuwa na sifa zote 13, kwa hiyo inapaswa iangalie ni nani anawazidi wengine.
“Kigezo cha kuwa na sifa ya maadili ndicho kinachowakwamisha wengi, pia hakuna mgombea anayeweza kuwa na sifa zote zilizowekwa na chama, mwingine anaweza kuwa na sifa saba, nne au tano.
“Wakitumia mfumo wa kuwatazama wagombea wao kwa idadi ya sifa, mtu mwenye sifa nyingi ndiye asimamishwe kugombea.”Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Dk Emmanuel Mallya alisema Tanzania inahitaji kuongozwa na rais mwenye historia ya uadilifu wa matumizi ya fedha za umma.
“Tunahitaji kiongozi anayeweza kusimamia fedha za umma, si mtu anayenunua vitu ovyo bila kujali Hazina kuna kiasi gani, hilo ni tatizo kubwa,” alisema Dk Mallya.
Aliongeza kuwa, kiongozi huyo lazima awe mchapakazi anayeweza kuwaletea wananchi maendeleo, lakini watu wengi wamekuwa wakisema wanamtaka mtu mwadilifu bila kuzungumzia uwezo wake wa kufanya kazi.
Mwalimu mstaafu wa shule ya msingi, Rehema Mathayo alisema kutokana na baadhi ya viongozi ndani ya CCM kukumbwa na kashfa za ufisadi, anayetaka kugombea urais lazima awe ‘msafi’ ndani na nje ya chama.
“Mshindi ndani ya chama ni mtu atakayekuwa amewashinda wenzake kwa kuwa na maadili mazuri na asiwe na doa lolote la kujishughulisha na ‘dili’ za ajabu,” alisema Rehema.
Mwalimu huyo aliongeza kuwa mgombea huyo lazima awe na uzoefu mkubwa wa masuala la kimataifa kwa kuwa hata kama atakuwa na maadili, kama hafahamu namna ya kuwaunganisha wananchi na jumuiya za kimataifa, hatakuwa na manufaa.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dk Ernest Mwasalwiba alisema kutokana na kuporomoka kwa maadili hususan kwa viongozi wa umma, vitendo vya rushwa na kadhia mbalimbali, rais ajaye anatakiwa kuhakikisha yale anayoyasema ndiyo anayatenda na Watanzania hawahitaji Rais dikteta.
“Masuala ya maadili, rushwa, yote haya yanazuiwa mpaka sasa lakini suala ni usimamizi tu... ni wakati sasa wa rais ajaye kuonyesha ajenda yake itakuwa ipi, anapokuwa amesema kitu kila mtu lazima afuate mfano akisema anachukia rushwa na maadili kwa yaheshimiwe isiwe ni mjadala kila mtu anafuata kuanzia chini hadi juu.
“Dikteta siyo kiongozi tunayemtaka, bali tunataka kiongozi atakayesimamia sheria na mifumo iliyopo iweze kufanya kazi ipasavyo... mfano Rais Jakaya Kikwete kipindi anaingia aliingia na kaulimbiu ya ‘Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya’ ambayo ilifuatwa hadi na viongozi wa halmashauri.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dk Romanus Dimoso alisema: “Sifa za rais huwa zinajulikana. Tunahitaji rais ajaye anayejua hali ya kisiasa ilivyo kwa sasa, hatutaki rais ambaye hatambui mchango unaotolewa na vyama vingi vya siasa na jinsi atakavyoweza kufanya navyo kazi hususan kwa kuhakikisha demokrasia inazingatiwa.”
Aliongeza: “Je, malengo ya anayetaka urais yale ya kuhakikisha ifikapo mwaka 2025 nchi hii inafikia uchumi wa kati. Amejipanga vipi kama mtumishi wa kwanza wa Taifa hili kutufikisha huko?... Hatutaki mtu awe rais tu kwa jina.”
Rais mstaafu wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Primus Saidia alisema: “Tunahitaji rais anayeweza kufanya uamuzi mgumu kwa mustakabali wa Taifa, asiwe rais wa maneno maneno, bali wa vitendo. Anasema dawa hospitalini hakuna na kesho zinakuwapo.“Tunataka mtu mwenye historia ya uongozi, ameshawahi kufanya nini katika kuboresha sekta ya afya, elimu, uchumi na kijamii? Alishafanya maamuzi magumu yapi ambayo kila mmoja aliyaona na aliyaheshimu?”

Tuesday, December 30, 2014

uwanja wa ndege wa JK AIBU



ulikua unavuja wakati mvua inanyesha.

Simba yamfukuza kazi kocha Patrick Phiri .

Siku chache baada ya kupoteza mchezo wake wa nane katika mfululizo wa ligi kuu ya Tanzania bara klabu ya Simba imeamua kumfukuza kazi kocha wake mkuu Mzambia Patrick Phiri baada ya kuwa naye kwa muda wa miezi minne tangu alipojiunga na timu hiyo katikati ya mwezi wa saba .
Phiri amefukuzwa kazi baada ya mabosi wa simba kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo ambayo imefanya usajili mkubwa wakati ligi iliposimama hali iliyopandisha matarajio ya mashabiki na viongozi hali iliyobadilika wakati walipocheza mchezo wao dhidi ya Kagera .
Phiri amefukuzwa kazi pamoja na msaidizi wake wa kwanza ambaye ni nahodha wa zamani wa timu hiyo Suleiman Matola ambaye amekuwa na timu hiyo kwa muda mrefu tangu wakati wa Dravko Logarusic na kabla ya hapo alikuwa akiifundisha timu ya vijana .
                  Kocha Mzambia Patrick Phiri akiwa mazoezini wiki chache kabla ya kufukuzwa kazi
Maamuzi hayo yalifanyika usiku wa jana kuamkia leo kwenye kikao kilichofanyika kwenye hoteli ya Double Tree Masaki jijini Dar-es-salaam ambapo viongozi wa juu wa klabu hiyo kwa kauli moja walikubaliana kuwafukuza kazi makocha hao wawili .
Tetetsi zaidi zinahabarisha kuwa nafasi ya Patrick Phiri itakwenda kwa kocha raia wa Serbia ambaye ni Goran Kapunovic  huku msaidizi wake akitarajiwa kuwa kocha Mrwanda Jean Marie Ntagwabira .
Taarifa zaidi zinasema kuwa Suleiman Matola ataendelea kuwa ndani ya klabu ya Simba ambapo atarudi kwneye nafasi yake ya zamani kama kocha wa timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 .

Kwa dalili hizi huenda ndege ya AirAsia ilianguka eneo hili…

                             Baadhi ya wahusika wa vikosi vya Utafutaji wa ndege hiyo, Indonesia.

vyombo mbalimbali vya habari vya Kimataifa vimeanza kuripoti kuhusu kinachoendelea kwa sasa katika hatua za utafutaji wa ndege ya AirAsia QZ8501 iliyopotea siku ya juzi December 28 ikitokea Indonesia kwenda Singapore.
Vikosi vya utafutaji vimetoa taarifa kwamba kuna mabaki mbalimbali ya ndege ambayo yamepatikana yakiwa yanaelea juu ya maji ya bahari katika eneo ambalo ndege hiyo ilipoteza mawasiliano.
Mkurugenzi wa Shirika la anga Indonesia Djoko Murjatmodjo amesema kuna baadhi ya vitu vimeonekana ikiwemo mwili wa mtu mmoja ukiwa unaelea baharini pamoja na mabaki ambayo bado hawajathibitisha kama ni ya ndege hiyo ambayo ni mlango wa abiria na mlango wa sehemu ya kupakilia mizigo.


Nimekuwekea hapa Stori muhimu zilizopewa Headlines kwenye Magazeti ya Leo Tanzania December 30, 2014


MWANANCHI
Mkazi wa Wilaya ya Kilombero,Morogoro Amon Nyenja amefariki dunia baada ya kuchomwa na kisu na anayedhaniwa kuwa ni hawara wa mke wake mdogo.
Ofisa Mtendaji wa kata ya Mang’ula Shabaan Lichaula  na Mkuu wa kituo cha Polisi Nkilijia Lazaro walisema Polisi inamshikilia mwanamke huyo ambaye ni mke wa marehemu wakati wakimsaka mtuhumiwa.
Lichaula alidai marehemu katika kumtafuta mkewe alimkuta amesimama mahali na mwanaume huyo na baadaye mwanamke huyo alikimbia na kutokomea na marehemu kuamua kumvaa mgoni wake lakini alizidiwa baada ya mtu huyo kumchoma kisu cha ubavuni hadi utumbo kutoka nje.
Alisema baada ya marehemu kuchomwa kisu alipiga kelele za kuomba msaada na wasamaria wema walijitokeza na kumwahisha hospitali na alifariki dunia baada ya kufanyiwa huduma ya kwanza wakati akihamishiwa katika hospitali Mtakatifu Fransis,Ifakara kwa matibabu zaidi.
MWANANCHI
Washtakiwa 11 wa kesi ya mauaji ya kukusudia ya aliyekua mjumbe wa tume ya mabadiliko  ya Katiba,Dk Sengondo Mvungi jana waligoma kwa muda kuondoka kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu wakishinikizwa kuelezwa lilipo jalada la kesi yao na hatua ilipofia.
Hilo lilitokea jana saa nne asubuhi ,muda mfupi  baada ya wakili wa serikali,Peter Njikekumweleza Hakimu Hellen Liwa kuwa kesi hiyo ilifika mbele yake kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wake bado haujakamilika na kuomba ipangwe tarehe nyingine.
Mshtakiwa Masunga Makenza alidai hafahamu sheria ,kesi hiyo ni ya muda mrefu na akahoji jalada likienda kwa DPP linatakiwa kukaa kwa muda gani.
Makenza alidai kuwa kesi hiyo ni ya kubambikiwa na kwamba ingekuwa halisi,upande wa mashtaka ungekuwa umekwishakamilisha upelelezi na kwamba wapotayari kushtakiwa ila kama upande wa mashtaka umeshindwa kukamilisha upelelezi mahakama iwaachie huru na ikikamilisha iwakamate tena.
MWANANCHI
Ikiwa imebaki takribani miezi 1o kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu mwakani,Chama cha CCM kinaonekana kuteswa na tuhuma za rushwa inayodaiwa kutolewa na makada wake wanaotajwa kutaka kuwania nafasi mbalimbali ukiwemo urais.
Hali hiyo inabainishwa nabaadhi ya makada wa Chama hicho katika ngazi mbalimbali ambao wameamua kulalamika waziwazi kupitia vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii.
Moja ya kauli ni iliyotolewa na Mbunge wa Bukoba Mjini Khamis Kagasheki kwenye akaunti yake ya Twitter akisema “Mgawo wa Xmass na mwaka mpya kwa wajumbe wa husika wa CCM ni kucheza na ugumu wa maisha uliopo,ni ununuzi wa nafasi na si uwezo wa ongozi, aibu”.
Alipotakiwa kufafanua Kagasheki alisema hakumtaja mtu licha ya kwamba wapo wengi wanaotoa zawadi,lakini baada ya kuandika kwenye mtandao ameandamwa na baadhi ya watu huku wengine wakimtolea lugha chafu.
“Hii ni line yangu naitumia kutoa mawazo siku zote,lakini nashangaa leo watu wameshikia kidedea maoni hayo mpaka wengine wanatumia lugha kali..sijamtaja mtu kwa sababu najua wapo wengi wanaotoa zawadi”alisema.
HABARILEO
Msichana mmoja mkazi wa mtaa wa Zaire Mkoani Arusha,amelazwa katika hospitali ya Mount Meru Arusha chini ya ulinzi mkali wa polisi baada ya kujizalisha mwenyewe kisha kumtumbukiza mtoto kwenye ndoo ya maji.
Baba mwenye nyumba ambayo binti huyo alikua amepanga chumba cha kuishi,Ruben Mollel alisema msichana huyo alikua anajulikana kwa jina la Dada Pendo na kwamba maisha yake hayakua wazi.
“Alipokuja kupanga hapa alidai yeye ni mwanafunzi,ila hivi karibuni alionekana kuwa mjamzito,hakuna kilichojulikana tena hadi jana ambapo nyumba hii ilizingirwa na wanakijiji ambao hatimaye waligundua kitoto kilichadhaniwa kuwa ni chake kikiwa kimezamishwa kichwa chini kwenye ndoo ya maji”alisema baba huyo mwenye nyumba.
Taarifa za uwezekano wa kuwepo mtoto huyo ndani ya nyumba ya dada huyo ziliibuliwa na mpangaji mwenzake Mama Martha ambaye alidai kuwa alisikia sauti ya mtoto akilia usiku kucha na baadaye kutoweka majira ya asubuhi.
Baada ya juhudi za kuchunguza walikuta kichanga hicho cha kiume kikiwa ndani ya ndoo na tayarikilikua kimefariki dunia huku mama yake akiwa katika hali mbaya kutokana na kujizalisha mwenyewe.
HABARILEO
Mvua iliyonyesha jijini Dar es salam imeleta balaa baada ya kuua watu wawili katika maeneo tofauti ya jiji hilo likiwemo tukio la mtoto wa miaka minne kufa baada ya kuzidiwa na maji yaliyoingia ndani ya nyumba wakati akiwa amelala.
Kwa mujibu wa Taarifa ya kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar Camilius Wambura alisema matukio hayo yalitokea jana mchana kwenye maeneo mawili tofauti.
Tukio la kwanza lilitokea eneo la Tandale ambapo mtoto Nasma Ramadhani akiwa amelala ndani ya nyumba yao maji ya mvua yaliingia ndanina kumzidia nguvu hadi kufariki na mwingine bibi kizee kufariki eneo la Mwananyamala aliyeangukiwa kichwani na ukuta wa nyumba yake na kumsababishia mauti.
Wambura alisema madhara mengine ni maji kujaa kwenye ameneo mbalimbali ikiwemo Mikocheni zilizopo ofisi za Tanesco,Kinondoni jirani na TMJ hivyo kuleta usumbufu wa Magari na watukuvuka eneo hilo.
MTANZANIA
Iliyokua ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Iringa iko katika matengenezo baada ya Wizara ya Maliasili kuridhia itumike kama jengo la Makumbusho ya Taifa.
Mkuu wa Wilaya hiyo na msaidizi wake  wamehamia katika jengo jipya lililojengwa kwa zaidi ya shilingi bilioni 1.8 katika eneo la Mawelewele mjini hapa.
Ukarabati wa jengo hilo lililojengwa na Serikali ya Ujerumani  zaidi ya miaka 114 iliyopita utafanywa na mradi wa kuendeleza utamaduni Nyanda za juu Kusini.
“Mradi huu wa Utalii ambao ni wa mamilioni ya pesa utahusisha ukarabati na uhifadhi wa iliyokua boma ya Iringa enzi za Utawala wa Kijerumani”alisema Meneja mradi Jan Kuever.
NIPASHE
Shinikizo dhidi ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospter Muhongo  limezidi kushika kasi baada ya Jukwaa la Katiba Tanzania JUKATA kumuomba Rais Kikwete kumwajibisha ili kupisha nafasi hiyo ili ichukuliwe na mtumishi mwenye sifa ya kutumikia umma.
Kikwete alisema katika hotuba yake kupitia wazee wa Mkoa wa dar es salaam kuwa amemuweka kiporo Muhongo kwa siku mbili hadi tatu kwa kuwa uchunguzi dhidi yake ulikua unaendelea.
Hatahivyo tangu siku hiyo zimeshapita siku tisa bila rais  kutangaza hatma ya Muhongo kama anatimuliwa ama anabaki katika nafasi yake.
Jukata wamemuomba Kikwete wamemuomba Kikwete kuchukua hatua dhidi ya Waziri huyo kutokana na kuhusishwa na kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow.

NYALANDU ATANGAZA RASMI KUWANIA URAIS 2015

                                                                Mbunge wa Singida Kaskazini, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ametangaza rasmi kuwania Urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu mwakani.

Amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuona kwamba anao uwezo wa kuiongoza Tanzania, katika harakati za kuwafikisha kwenye maendeleo endelevu wanayotaka Watanzania.

Amesema, yuko tayari kushindanishwa na Watanzania wengine watakaoona kuwa wanafaa kuwa Rais, lakini akisema kwanza kila atakayejitokeza itabidi kazi zake zipimwe kwa moto na endapo zitayeyuka hafai.

Nyalandu ambaye alitangaza uamuzi huo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo jimbo la Singida Kaskazini, alisema, yeye anaingia kwenye kinyang'anyiro akiwa kifua mbele kutokana na kuamini kwamba amekwishafanyakazi zilizotukuka.

"Kazi zangu nilizofanya zinajulikana na ninaziamini kwamba ni nzuri, hivyo yeyote atakayetaka urais apimanishwe na mimi kwa kupimwa kazi zetu kwa moto", alisema Nyalandu

Itakapofika siku ya siku, nitaenda Dodoma nikisindikizwa na wana Singida Mashariki, na wengine wengi kutoka pembe zote za Tanzania, kwenda Dodoma kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea Urais kwa tiketi ya CCM", alisema.

Mkutano huo wa jimbo ambao ulipambwa na shamrashamra mbalimbali zikiwemo za wasanii wakiwemo kina Rose Mhando, ulifurika maelfu ya wananchi waliohamasika kumsikiliza Nyalandu.

HABARI KATIKA PICHA, NYALANDU AKITANGAZA KUWANIA URAIS














Monday, December 29, 2014

Zaidi ya abiria mia moja wa ndege ya ATC wamekwama nchini Tanzania, baada ya safari zao kuarishwa. Wengi wao wakielekea nchini Comoros na wengine wakiwa katika safari za ndani, kuelekea Mtwara na Kigoma wamekwama kwa siku mbili mjini Dar es salaam.
Abiria hao imebidi wakodiwe hoteli ilivyo ada wakisubiri muafaka wa namna watakavyosafiri kuelekea Comoro. Sharifu Hashim, Balozi wa heshima wa Comoro huko Chicago nchini Marekani, anasema mambo yake mengi yamekwama kutokana na tukio hili na hajapata uhakika ataondoka lini
Zenabal Mwarabu yeye hofu yake ni kwa namna gani ataweza kuiwahi ndege aliyokuwa aunganishe Kisiwani Comoro kuelekea katika kisiwa kingine cha Rarinyo.
Msawi Seifu anasema ijapokuwa tatizo hili limetokea lakini Air Tanzania ni mkombozi kwa wana Comoro….Lily Fungamtama, Mkuu wa Kitengo cha Biashara amesema tayari Air Tanzania inashughulika kuhakikisha abiria wote wanasafiri mapema kesho .
Sikukuu za mwisho wa mwaka ndilo tatizo la kukwama kwa abiria hao,kwani marubani hawajarejea kazini tangu walipoondoka, na walitegemewa kurejea kazini tarehe 27 mwezi huu, baada ya sherehe za Christimas, lakini haikuwa hivyo na kusababisha sintofahamu hiyo.

Unafahamu jezi inayoongoza kwa ufungaji wa magoli mengi England? Rekodi iko hapa…

Katika hali ya kawaida namba zinazoandikwa kwenye jezi za wachezaji wa timu za mchezo wa soka huwakilisha nafasi wanazocheza uwanjani .
Namba hizi kiasili huendana na eneo ambalo mchezaji husika anapendelea kucheza kwa mfano jezi namba moja huvaliwa na kipa , jezi namba tisa huvaliwa na mshambuliaji na kadhalika na kadhalika.
Utamaduni huu umekuja kubadilika hivi karibuni ambapo Wachezaji wamekuwa na kawaida ya kuvaa jezi kutokana na ukaribu walio nao na namba fulani au wakati mwingine sababu za kihistoria na mazoea pia yamekuwa yakiongoza utamaduni wa kuvaa namba husika .
Mshambuliaji wa Ivory Coast, Wilfred Bony ni moja kati ya wachezaji wanaovaa jezi namba 10 wanaofanya vizuri kwenye ligi ya England .

Kiutamaduni kuna namba huvaliwa na wachezaji wa aina fulani, mfano wake ni jezi namba kumi ambayo siku zote imekuwa ikivaliwa na wachezaji wenye vipaji na ubora kuliko wote na mara nyingi huwezi kukuta mchezaji wa kawaida anavaa jezi namba kumi.
Hili limeweza kudhihirika msimu huu kwenye ligi ya England ambako wachezaji wanaovaa jezi namba 10 wameongoza kwa kung’aa hasa kwenye ufungaji wa mabao muhimu.
Takwimu zinaonyesha kuwa kati ya mabao 457 ambayo yamefungwa hadi sasa kwenye mechi za ligi kuu ya England mabao 56 yamefungwa na wachezaji wanaovalia jezi hii ambayo siku zote inahusishwa na ‘mafundi’ wa mpira.
                                  Romelu Lukaku ni mchezaji mwingine anayevaa jezi namba 10.

Idadi ya mabao yaliyofungwa na wachezaji wanaovaa jezi namba 10 kwa ujumla  ndio idadi kubwa ya mabao kufungwa na wachezaji wanaovaa namba zote ikifuatiwa na namba 9 ambao wachezaji wake wamefunga jumla ya mabao 38 ikiwa ni tofauti ya mabao 18 kati ya wachezaji wanaovaa jezi namba 9 na namba 10.
Katika kundi la wachezaji wanaovaa namba 10 wako nyota kama Eden HazardWayne Rooney,Wilfred,Bony,,Jack,Wilshere,naRomelu,Lukaku huku Bony na Rooneywakiongoza orodha hiyo wakiwa wamefunga mabao 8.

Wafungaji Bora kuendana na namba za Jezi

1. Jezi namba 10 – Magoli 56
2. Jezi namba 9 –  Magoli 38
3. Jezi namba 18 – Magoli 33
4. Jezi namba 19 – Magoli 32
5. Jezi namba 23 – Magoli 24
6. Jezi namba 11 – Magoli 23
6. Jezi namba 16 – Magoli 23
6. Jezi namba 17 – Magoli 23
7. Jezi namba 15 – Magoli 22
8. Jezi namba 21 – Magoli 19
*Takwimu hizi ni kwa msimu huu pekee. 



Imenyesha mvua kubwa leo Dar kwa zaidi ya saa mbili. Hii ni hali ya baadhi ya mitaa












Kazi yangu ni kuhakikisha haupitwi na chochote ndio maana natumia muda wangu kukusanyia matukio mbalimbali yanayojiri ambapo leo dec 29 Wakazi wa Dar es Salaam wamekumbwa na mafuriko kwenye maeneo mbalimbali.
Hizi ni baadhi ya picha kutoka maeneo  yaliyojaa maji zaidi ya saa mbili kama ambavyo unaona kwenye baadhi ya picha ya juu na hii inayofata hapa chini.







Taarifa ya kinachoendelea hivi sasa kuhusu ndege iliyopotea jana Indonesia


Chanzo cha habari kutoka nchini humo kinasema uchunguzi kuhusu ndege hiyo bado unaendelea huku wakitumia ndege za kijeshi kutoka Indonesia na Singapore Kusini Magharibi  mwa Pwani ya Borneo ambapo ilipoteza mawasiiano
Rubani wa ndege hiyo Captain Iriyanto

Bado jitihada za kuwatafuta abiria 162 waliokuwepo ndani ya ndege zinaendelea,na mpaka sasa hakuna mawasiliano yoyote,ilikua ikielekea Singapore.
Shughuli ya kutafuta ndege ya AirAsia ambayo ilipotea jana Jumapili imeendelea leo tena baada ya kusitishwa kwa muda.
Ndege hiyo ilikuwa safarini kwenda nchini Singapore ikitokea mji wa Surubaya nchini Indonesia na shughuli za kuitafua zinafanyika kwenye kisiwa cha Belitung.