Tuesday, December 30, 2014

Simba yamfukuza kazi kocha Patrick Phiri .

Siku chache baada ya kupoteza mchezo wake wa nane katika mfululizo wa ligi kuu ya Tanzania bara klabu ya Simba imeamua kumfukuza kazi kocha wake mkuu Mzambia Patrick Phiri baada ya kuwa naye kwa muda wa miezi minne tangu alipojiunga na timu hiyo katikati ya mwezi wa saba .
Phiri amefukuzwa kazi baada ya mabosi wa simba kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo ambayo imefanya usajili mkubwa wakati ligi iliposimama hali iliyopandisha matarajio ya mashabiki na viongozi hali iliyobadilika wakati walipocheza mchezo wao dhidi ya Kagera .
Phiri amefukuzwa kazi pamoja na msaidizi wake wa kwanza ambaye ni nahodha wa zamani wa timu hiyo Suleiman Matola ambaye amekuwa na timu hiyo kwa muda mrefu tangu wakati wa Dravko Logarusic na kabla ya hapo alikuwa akiifundisha timu ya vijana .
                  Kocha Mzambia Patrick Phiri akiwa mazoezini wiki chache kabla ya kufukuzwa kazi
Maamuzi hayo yalifanyika usiku wa jana kuamkia leo kwenye kikao kilichofanyika kwenye hoteli ya Double Tree Masaki jijini Dar-es-salaam ambapo viongozi wa juu wa klabu hiyo kwa kauli moja walikubaliana kuwafukuza kazi makocha hao wawili .
Tetetsi zaidi zinahabarisha kuwa nafasi ya Patrick Phiri itakwenda kwa kocha raia wa Serbia ambaye ni Goran Kapunovic  huku msaidizi wake akitarajiwa kuwa kocha Mrwanda Jean Marie Ntagwabira .
Taarifa zaidi zinasema kuwa Suleiman Matola ataendelea kuwa ndani ya klabu ya Simba ambapo atarudi kwneye nafasi yake ya zamani kama kocha wa timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 .

No comments:

Post a Comment