Katika hali ya kawaida namba zinazoandikwa kwenye jezi za wachezaji wa timu za mchezo wa soka huwakilisha nafasi wanazocheza uwanjani .
Namba hizi kiasili huendana na eneo ambalo mchezaji husika anapendelea kucheza kwa mfano jezi namba moja huvaliwa na kipa , jezi namba tisa huvaliwa na mshambuliaji na kadhalika na kadhalika.
Utamaduni huu umekuja kubadilika hivi karibuni ambapo Wachezaji wamekuwa na kawaida ya kuvaa jezi kutokana na ukaribu walio nao na namba fulani au wakati mwingine sababu za kihistoria na mazoea pia yamekuwa yakiongoza utamaduni wa kuvaa namba husika .
Mshambuliaji wa Ivory Coast, Wilfred Bony ni moja kati ya wachezaji wanaovaa jezi namba 10 wanaofanya vizuri kwenye ligi ya England .
Kiutamaduni kuna namba huvaliwa na wachezaji wa aina fulani, mfano wake ni jezi namba kumi ambayo siku zote imekuwa ikivaliwa na wachezaji wenye vipaji na ubora kuliko wote na mara nyingi huwezi kukuta mchezaji wa kawaida anavaa jezi namba kumi.
Hili limeweza kudhihirika msimu huu kwenye ligi ya England ambako wachezaji wanaovaa jezi namba 10 wameongoza kwa kung’aa hasa kwenye ufungaji wa mabao muhimu.
Takwimu zinaonyesha kuwa kati ya mabao 457 ambayo yamefungwa hadi sasa kwenye mechi za ligi kuu ya England mabao 56 yamefungwa na wachezaji wanaovalia jezi hii ambayo siku zote inahusishwa na ‘mafundi’ wa mpira.
Romelu Lukaku ni mchezaji mwingine anayevaa jezi namba 10.
Idadi ya mabao yaliyofungwa na wachezaji wanaovaa jezi namba 10 kwa ujumla ndio idadi kubwa ya mabao kufungwa na wachezaji wanaovaa namba zote ikifuatiwa na namba 9 ambao wachezaji wake wamefunga jumla ya mabao 38 ikiwa ni tofauti ya mabao 18 kati ya wachezaji wanaovaa jezi namba 9 na namba 10.
Katika kundi la wachezaji wanaovaa namba 10 wako nyota kama Eden Hazard, Wayne Rooney,Wilfred,Bony,,Jack,Wilshere,naRomelu,Lukaku huku Bony na Rooneywakiongoza orodha hiyo wakiwa wamefunga mabao 8.
Wafungaji Bora kuendana na namba za Jezi
1. Jezi namba 10 – Magoli 56
2. Jezi namba 9 – Magoli 38
3. Jezi namba 18 – Magoli 33
4. Jezi namba 19 – Magoli 32
5. Jezi namba 23 – Magoli 24
6. Jezi namba 11 – Magoli 23
6. Jezi namba 16 – Magoli 23
6. Jezi namba 17 – Magoli 23
7. Jezi namba 15 – Magoli 22
8. Jezi namba 21 – Magoli 19
*Takwimu hizi ni kwa msimu huu pekee.
No comments:
Post a Comment