Hukumu imetolewa!Je unamkumbuka yule mfanyakazi wa ndani nchini Uganda aliyemtesa mtoto? sasa atahukumiwa kifungo cha miaka minne.
Jolly Tumuhirwe mwenye miaka 22 amehukumiwa adhabu hiyo baada ya kuthibitika kumtesa mtoto wa miezi minne aliyejulikana kwa jina la Arnella.
Awali msichana huyo alisema alifanya hivyo ili kulipiza kisasi baada ya mama wa mtoto huyo kumpiga,hata hivyo mama huyo alikana kumpiga.
Mwendesha mashtaka Lilian Buchan alimwambia dada huyo anastahili adhabu hiyo kutokana na kosa hilo la kumtesa kikatili mtoto asiye na hatia.
Katika video hiyo iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuthibitika kuwafikia watu zaidi ya milioni 40 iliweza kumwonyesha binti huyo akimwadhibu mtoto huyo bila huruma huku akitumia tochi kumpiga sehemu za makalio akiwa hana nguo.
No comments:
Post a Comment