NIPASHE
Uchaguzi wa Serikali za mitaa,vijiji na vitongoji ulifanyika nchini kote jana huku ukitawaliwa na kasoro na vurugu kubwya zilizosababishapolisi kutumia risasi za moto na baadhi ya wapigakura kuchapana makonde jijini Dar es salaam.
Vurugu hizo zilitokana na uchaguzi huo kugubikwa na kasoro nyingi na hivyo kusababisha baadhi ya vituo kulazimika kuahirisha uchaguzi huo hadi wiki ijayo.
Baadhiya kasoro zilizoibuka zilitokana na baadhi yavituo kuchanganya majina ya wagombea,kuchelewa kuanza kwa uchaguzi,kukosekana kwa vifaa vya kupigia kura pamoja na baadhi ya wagombea kuwahujumu wengine.
Uchaguzi huo ulipangwa kuanza saa2 asubuhi lakini maeneo mengi ulichelewa kuanza kutokana na vifaa kuchelewa kufika vituoni.
Katika kituo cha Kimara bucha kulitokea vurugu kubwa baada ya mawakala kugombea kuwasaidia wapigakura kuweka alama ya vyema kwa wagombea na baadhi ya watu kutakakurudia kup[iga kura hali iliyosababisha msimamizi wa kituo hicho kupigwa na wapigakura kutokanana na kukerwa na kitendo cha baadhi yawatu kurudia kupiga kura.
NIPASHE
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele ambaye pia ni Mbunge wa Shinyanga mjini amevamiwa na kundi la vibaka wakati akienda Zahanati kupatiwa matibabu na kisha kuporwa vitu mbalimbali mjini Shinyanga.
Masele alisema tukio hilo lilitokea juzi saa4 usiku wakati akienda kupatiwa matibabu ya matatizo ya koo katika Zahanati ya Bakwata na gafla alivamiwa na kundi la watu wapatao 30 na kumpora mali zake.
Alisema akiwa na Naibu Katibu mkuu CCM Zanzibar,Vuai Aly wakipata chakula cha usiku hotelini gafla alijisikia vibaya na kuamua kwenda kwenye Zahanati hiyo kupatiwa matibabu na ndipo alipata mkasa huo wakati akiwa njiani.
Masele alikanusha tuhuma alizozushiwa na wananchi kuwa kuporwa huko kunatokana na yeye kugawa rushwa kwa wananchi wakati wa kampeni Serikali za mitaa ili wananchi wawachague wagombea wa CCM.
MTANZANIA
Katibu wa CCM kata ya Narungombe Lindi Mohamed Pilipili amevamiwa na kupigwa hadi kuzimia na mabaunsa kwa madai ya kufanya kampeni ya nyumba kwa nyumba usiku.
Tukio hilo lilitokea juzi usiku katika kitongoji cha Chikwale baada ya kundi la mabaunsa kumvamia na kumpiga Katibu huyo pamoja na Mwenyekiti wa CCM wa kata hiyo Seleman Lukuche.
Akizungumzia tukio hilo Lukeche alisema ilikua saa 3 usiku wakitoka Ruangwa kupeleka taarifa za mwenendo wa uchaguzi pamoja na majina ya mawakala wa CCM ndipo walipovamiwa na kundi hilo la mabaunsa10waliodai wao wanadhibiti .vitendo vya ryushwa ambao walianza kuwapiga bila kutaka maelezo.
Katika tukio jingine mgombea wa nafasi ya uenyekiti kata ya Mkwajuni amepigwa na watu wanaodaiwa wafuasi wa CUF kwa madai kuwa alikwenda kwenye eneo la Mjimwema kupanga mikakati ya kuiba kura.
UHURU
Muda wowote kuanzia sasa Rais Jakaya Kikwete atatoa na kutangaza uamuzi wake kuhusiana na baadhi ya watendaji wakiwemo Mawaziri kuhusishwa katika kashfa ya wizi wa fedha za Tegeta Escrow.
Wiki iliyopita Rais alipokea na kupiia ripoti iliyowasilishwa kwake,nyaraka na ushauri uliotolewa katika maazimio ya Bunge kuhusu akaunti ya Tegeta Escrow.
Kikwete ambaye alianza kazi Desemba 8 mwaka huu baada ya mapumziko kutokana na kufanyiwa upasuaji alisema atatoa uamuzi wake ndani ya wiki hii.
Alisema atatolea maamuzi mambo ambayo yanamuhusu yeye moja kwa moja na yale yanayohusu Serikali atatolea uamuzi na maelekezo ya namna ya kuyashughulikia.
Bunge lilitoa maazimio mbalimbali kwa Serikali ikiwemo kuitaka mamlaka ya uteuzi kuwawajibisha ikiwani pamoja na kuwavua nyadhifa zao Waziri wa Nishatina Madini,Mwanasheria mkuu,Waziri wa nyumba na maendeleo ya makazi,Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na madini na wengineo.
No comments:
Post a Comment