Wednesday, December 17, 2014

Zile Stori zilizopewa nafasi kwenye Magazeti ya leo Tanzania December 17 nimekuwekea hapa mtu wangu



MTANZANIA
Matumizi ya shirika la Maendeleo ya Mafuta Tanzaniua TPDC ambayo pamoja na mambo mengine yameinisha mishahara inayotaka iidhinishiwe na Mamlaka ya udhibiti wa huduma za maji na nishati EWURA ili ianze kutumika Januari mwakani,imebainika ni kufuru.
Kwa mujibu wa Baraza la Uashauri la Watumiaji wa  wa huduma zinazodhibitiwa na EWURA,mishara ambayo TPDC inataka EWURA iipitishe  ili iweze kutumika mwakani ni shilingi milioni 36 kwa Mkurugenzi wa Shirika hilo.
Maofisa wengine walioombewa mishahara ni mkurugenzi na makamu wa vitengo milioni 28,maofisa waandamizi milioni 16.2,wahasibu,maofosa rasilimali watu,ofisa masoko,ugavi milioni 12.6,wahudumu,madereva na makatibu Muhtasi milioni 5.4.
“Mishahara inayopendekezwa ni mikubwa,utetezi wa TPDC kuwa viwango vya mishahara ni kwa mujibu wa soko la ajira katika sekta za mafuta mna gesi haujitoshelezi kwa sababu hauelezei soko hilo ni kwa nchi zipi”inasema sehemu ya nyaraka hiyo.
Msemaji wa Ewura Stella Lupimo alikiri nyaraka hiyo ni ya Baraza hilo na alisema mapendekezo hayo yaliwasilishwa kwenye mkutano wa taftishi wa kujadili mapendekezo ya TPDC uliofanyika November 27 mwaka huu.
MTANZANIA
Klabu ya Yanga imemsainisha Mshambuliaji wa kimataifa Hamis Tambwe mkataba wa mwaka mmoja kwa dau la kiasi cha dola 20,000 za kimarekani sawa na milioni 34.3 za kitanzania.
Imeelezwa kuwa Yanga iliahidi kumlipa mshahara wa dola 2,000 kwa mwezi pamoja na kumpa nyumba ya kuishi maeneo ya Sinza jijini Dar es salaam,mshahara ambao ni mara mbili wa ule aliokua akilipwa Simba wa milioni 1.3.
Usajili wa Tambwe ambao ni raia wa Burundi aliachwa na Simba kwa madai ya kushuka kiwango chake amewashanga wengi kutokana na mashabiki wengi wa Simba kumkubali baada ya kuibuka mfungaji bora wa ligi kuu Tanzania bara msimu uliopita.
Chanzo cha uhakika kilisema Simba imekubali kumlipa mshambuliaji huyo dola 6,000 kama stahiki zake baada ya kuvunja mkataba wake kama ilivyofanya kwa kiungo Pierre Kwizera ambaye nae ni raia wa Burundi ambaye hakupata mafanikio yoyote tangu asajiliwe kwenye timu hiyo.
NIPASHE
Baada ya kufanya vibaya katika uchaguzi wa Serikali za mitaa,vitongoji na vijiji Mkoani Shinyanga baadhi ya wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM wamefikia hatua ya kurushiana matusi na kuvuana nguo hadharani.
Katibu wa siasa na uenezi wa Chama hicho Wilayani Shinyanga Charles Shigino alisema baada ya CCM kufanya vibaya katika kata ya Ngokolo na Chadema kuchukua mitaa sita kati ya saba,wanachama wameanza kumtuhumu kwa kusababisha matokeo mabaya.
Wakati akiingia ofisini alikutana na Katibu wa jumuiya ya vijana UVCCM Zawadi Nyambo na kumzuia kuingia ofisini huku akimrushia maneno ya matusi hali iliyosababisha mtafaruku mkubwa na kujaza watu.
Alisema baada ya kushindwa kuvumilia matusi hayo aliamua kukabiliana nae huku watu wakiingia hali iliyosababisjha nguo kumvuka na kubaki mtupu.
MWANANCHI
Mwenyekiti mwenza wa Umoja wa katiba ya wananchi Ukawa Freeman Mbowe amesema Umoja huo utafanya tathimni ya maeneo ambayo wangeweza kushinda na kusimamisha mgombea mmoja kila eneo ili kuwachukulia hatua wale wote waliokiuka makubaliano yao.
Wenyeviti wa Umoja huo walisaini makubaliano kadhaa yakiwemo ya kusimamisha mgombea mmoja atakayeungwa mkono na Ukawa katika chaguzi zote kuanzia Serikali za mitaa hadi uchaguzi mkuu ujao.
Hata hivyo katika uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika jumapili,baadhi ya maeneo kila chama kilisimamisha mgombea wake na matokeo yake kuipa CCM kushinda kwa urahisi.
Mbowe alisema viongozi wote kutoka vyama hivyo walihusika kukiuka makubaliano hayo na watawachukulia hatua za kinidhamu na tathmini itakayofanyika ndani ya umoja huo itakua nafasi muhimu ya kujipanga kufanikiwa katika uchaguzi mkuu ujao.
MWANANCHI
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imewataka wamiliki wa vyombo vya moto visivyotumika kufuta usajili wake ili kuiwezesha Serikali kuwa na kumbukumbu sahihi ya vyombo vya moto vinavyofanya kazi.
Akizungumza jana na Gazeti hili Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipakodi Richard Kayombo alisema lengo la agizo hilo ni kuondoa kumbukumbu za malipo kwa vyombo wasivyotumia.
“Uamuazi huu tunaufanya ili kuwasaidia wamiliki wa vyombo hivyo kuondokana na usumbufu kwani tusipofanya hivyo TRA itaendelea kuweka kumbukumbu ya kodi zake”alisema Kayombo.
Alisema mmliki anayetaka kufuta usajili wa chombo chake atalazimika kwenda Polisi na kupewa cheti kutoka polisi makao makuu ya Usalama Barabarani.
MWANANCHI
Watoto wa Watanzania waliokua wameungana kifua ambao walikua wakitumia maini na mapafu yaliyounganika,mvungu mmoja wa moyo na mmeng’enyo wa chakula wamefanyiwa upasuaji na kutenganishwa huko India.
Pacha hao wa kile Abriana na Adriana wenye umri wa miezi minne walifanyiwa upasuaji huo November 17 katika Hospitali ya Apollo.
Daktari aliyesimamia upasuaji huo Ks Sivakumar alisema upasuaji huo ulichukua zaidi ya saa 20 na walilazimika kutumia muda huo kutokana na jinsi pacha hao walivyokua wameungana na haikua kazi ndogo kuwarudisha kwenye hali yao ya kawaida.
“Huu ni upasuaji wa kwanza na wa aina hii kufanikiwa kwani wengi tuliokua tukiwafanyia walikua wakipoteza maisha,hivyo tunajivunia kwa hili,jumla ya madaktari 50 waliobobea katika taaluma mbalimbali tulifanikiwa kufanya upasuaji huu kutokana na kuwa ni mkubwa”alisema SivaKumar.
TANZANIA DAIMA
Mwananchi wa Chama cha Mapinduzi CUF Ibrahim Lipumba amesema Waziri mkuu Mizengo Pinda ni mzigo usiobebeka  katika Serikali ya Rais Kikwete na hafai kuwa rais kwani ameshindwa katika kila jambo analosimamia.
Kutokana na hali hiyo amemtaka Rais Kikwete aachane na Pinda kwani atamsababisha kumaliza muda wake wa urais vibaya.
Alisema uchaguzi wa Serikali za mitaa uliokua katika  chini ya ofisi ya Waziri mkuu umekua sehemu nyingine ya matumizi mabaya ya fedha za Serikali huku wakijua kuwa Serikali haipo tayari kuona mabadiliko kupitia masanduku ya kura.
“Pinda na Ghasia waachia madaraka,wameshindwa kusimamia uchaguzi huu,wameruhusu Wakurugenzi kuwa sehemu ya watatufa mafanikio ya CCM badala ya kusimamia majukumu ya wananchi,kuchagua viongozi wanaowataka,hili linamuharibia rais Kikwete zaidi na anaweza asimalize muda wake akiwa na chembe ya usafi”alisema Lipumba.
Alisema waziri Mkuu amekua na mambo mengi yasiyoeleweka na ameshindwa kusimamia misingi ya kiuongozi na kwamba hali hiyo inatoa unafuu kwa wapinzani kushinda chama tawala iwapo CCM itampitisha kuwa mgombea wao.

No comments:

Post a Comment