Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Ndege wan Kijeshi mjini Riyadh, Saudi Arabia, asubuhi ya leo, Jumapili, Januari 25, kuhani kifo cha Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud aliyefariki Alhamisi na kuzikwa
Ijumaa ya wiki iliyopita. Baada ya kuhani msiba wa Mfalme Abdullah, Rais Kikwete ataendelea na safari yake kwenda nchi za Ujerumani na Ufaransa kwa ziara za kikazi.
Ijumaa ya wiki iliyopita. Baada ya kuhani msiba wa Mfalme Abdullah, Rais Kikwete ataendelea na safari yake kwenda nchi za Ujerumani na Ufaransa kwa ziara za kikazi.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
akiwasili mjini Riyadh, Saudi Arabia,asubuhi ya leo, Jumapili, Januari
25, 2015, kuhani kifo cha Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud
aliyefariki Alhamisi na kuzikwa Ijumaa ya wiki iliyopita.
Baada ya
kuhani msiba wa Mfalme Abdullah, Rais Kikwete ataendelea na safari yake
kwenda nchi za Ujerumani na Ufaransa kwa ziara za kikazi.
Mjini
Berlin, Ujerumani ambako Rais Kikwete alitarajiwa kuwasili kesho,
Jumatatu, Januari Ishirini na Sita, akitokea Riyadh, Saudi Arabia,
anatarajiwa kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Global Alliance for
Vaccines and Immunization (Gavi Alliance) ambako viongozi mbali mbali
duniani watajadili jinsi ya kuboresha mipango ya utoaji chanjo kwa
watoto wadogo hasa katika nchi zinazoendelea.
Baada ya
kumaliza ziara yake Ujerumani, Rais Kikwete atakwenda Ufaransa ambako
miongoni mwa mambo mengine atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi
wa Ufaransa.
Aidha, Rais Kikwete atafungua jengo jipya la Ubalozi wa Tanzania katika Ufaransa na pia nyumba ya balozi.
Rais
Kikwete baada ya kumaliza ziara zake za kikazi katika Ujerumani na
Ufaransa atakwenda Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa
Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU).
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
25 Januari, 2015
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
25 Januari, 2015
No comments:
Post a Comment