Mwanamuziki Profesa J akiimba katika uzinduzi huo.
Mwanamuziki Vanessa Mdee akiimba katika uzinduzi huo.
Tigo
Tanzania leo imetangaza rasmi uzinduzi wa Muziki wa Tigo ujulikanao kama
"Tigo Music" kwa kushirikiana na Deezer, ambayo ni huduma ya kimataifa
inayorusha muziki itakayowapa Watanzania muziki usiokuwa na kikomo.
Kutakuwa
na hafla ya uzinduzi kwa ajili ya Tigo Music katika viwanja vya Leaders
Club Dar es Salaam Tarehe 24 Januari ambapo wananchi watatumbuizwa na
nyimbo tofauti tofauti kutoka kwa wasaniii 18 wa hapa nchini kama
Diamond Platinum, Ali Kiba, Professor J, Weusi, Msondo, Ben Paul,
Shillole Linah, Christian Bella, AY hao ni kati ya 18.
Kuanzia
Januari 24, wateja wa Tigo wenye vifurushi vya malipo ya kabla ya
intaneti wana uwezo wa kupata nyimbo milioni 36 za wasanii wa Kitanzania
na Afrika kwa ujumla katika simu zao za mkononi za smartphone.
Vilevile, Tigo itatafuta miziki mipya ya kusisimua ya wasanii wa ndani
kupitia ushirikiano mpya na kampuni ya Africa Music Rights, ambayo
inawezesha, kutafuta na kusimamia haki za muziki katika bara la Afrika,
Meneja
Mkuu wa Tigo Bi, Cecile Tiano alisema, 'Tuna furaha kuwa kampuni ya
kwanza ya mawasiliano Tanzania kuwapa wateja wetu muziki usiokuwa na
kikomo". Muziki unajukumu kubwa katika Tanzania yetu tajiri na tamaduni
tofauti kama starehe katika matukio ya kijamii na hata wakati binafsi.
Haya ni mafanikio makubwa kwetu tukitarajia watu zaidi na zaidi kutumia
smartphones katika sehemu hii ya dunia'.
"Kama
bidhaa yenye maisha ya kidijitali, lengo letu ni kuiwezesha tasnia ya
muziki kwa kujenga jukwaa ambalo si tu linaruhusu kupata nyimbo za
wasanii wa ndani kwa urahisi, lakini pia linawapa mafunzo wanamuziki
wetu kwenye masuala muhimu kama vile haki miliki na masoko. Hii ni njia
yetu ya kusaidia vipaji vya wasanii na kukuza tasnia ya muziki wa ndani,
"aliongeza.
Kuanzishwa
kwa Muziki wa Tigo (Tigo Music) nchini Tanzania kumetokana na mafanikio
ya uzinduzi nchini Amerika ya Kusini mwaka 2012 pamoja na Ghana mwaka
2014, na. Tangu kuanzishwa kwake imekuwa ni sehemu muhimu kwa maisha ya
kidijitali ya watu ya kila siku na hii inaendana na matukio ya muziki wa
ana kwa ana yaliyowahi kufanywa na wanamuziki mashuhuri duniani, pamoja
na yale yaliyorekodiwa ndani ya studio.
Kama
bidhaa, Tigo music imeongezeka kwa kiasi kikubwa huko Colombia kama nchi
inayoongoza kwa huduma ya urushwaji wa muziki, wakiwa na watumiaji
600,000 wakisikiliza kwa wastani nyimbo zaidi ya 400 na masaa 40 ya
muziki kila mwezi.
Urushwaji
wa muziki ni eneo linalokua kwa haraka sana katika tasnia ya muziki
kimataifa, na bidhaa ya muziki tayari imekuwa ya pili kimaarufu kwenye
vipengele vya simu za mkononi katika Afrika.
No comments:
Post a Comment