Wednesday, December 31, 2014

Risala ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Ali mMohamed Shein,ya kuukaribisha mwaka mpya 2015.


Ndugu Wananchi,
Kwa neema na fadhila za Mwenyezi Mungu, Subhana Wataala tunaukaribisha mwaka mpya wa 2015 Miladiya na kuuaga mwaka 2014 tukiwa na utulivu na amani nchini. Inatubidi tumshukuru Mola wetu kwa kutujaaliya uhai hadi sasa na tumuombe Mwenyezi Mungu awarehemu wenzetu tuliokuwa nao mwaka jana na miaka iliyopita ambao wameshatangulia mbele ya haki.

Kwa kawaida binadamu wengi huupokea mwaka mpya kwa kujipangia maazimio mapya. Hivyo si vibaya, lakini ni vyema pia kutafakari na kuzingatia yaliyopita. Kwa kufanya hivyo, tutaweza kutathmini mafanikio na utekelezaji wa maazimio na dhamira tulizozipanga kwa mwaka uliopita na tuweze kujipanga upya kwa Mwaka Mpya.

Ndugu Wananchi,
Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia hali ya amani, salama na utulivu ambayo imetuwezesha kupata mafanikio katika mambo yetu mbali mbali tuliyojipangia katika mwaka uliopita.  Ili tuweze kufanya tathmini ya kina na kuhakikisha kuwa tunapiga hatua kubwa zaidi ya maendeleo katika mwaka ujao, hatuna budi kuiendeleza hali ya amani na utulivu tuliyonayo kwa faida ya kila mmoja wetu.  Tunaona, tunasoma na tunasikia kwenye vyombo vya habari, shida, taabu na hasara za maisha zinazowakuta watu wa sehemu mbali mbali za dunia kutokana na kutokuwepo kwa amani.  Mwenyezi Mungu atuepushe na hali hio na atujaali tuendelee kuitunza amani, tukae salama na tudumishe utulivu tulionao.
Ndugu Wananchi,
Kutokana na hali ya amani na utulivu nchini, tulifaulu kuwa na usimamizi mzuri wa utekelezaji wa mipango mikubwa ya maendeleo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ikiwemo Dira ya Maendeleo ya mwaka 2020, MKUZA II, Malengo ya Milenia ya 2015 na Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2010 - 2015.Katika mwaka uliopita, tulipata mafanikio mengi na makubwa katika nyanja za uchumi, siasa na maendeleo ya jamii.  Aidha, tuliweza kudumisha mshikamano na umoja katika jamii.  Ni matumaini yangu kwamba sote tunaukaribisha mwaka mpya tukiwa na dhamira na matumaini ya kuyaendeleza mafanikio haya.
Ndugu Wananchi,
Katika risala hii fupi ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2015, hivi leo, sitazungumzia mafanikio tuliyoyapata ya kila sekta lakini, apendapo Mola mafanikio hayo nitayazungumza katika hotuba yangu ya kuadhimisha mwaka 51 wa Mapinduzi Matukufu ya Januari 12, 1964.  Naomba niseme tu kwamba uchumi wetu umeimarika na kukuwa kwa kiasi cha kuridhisha.  Ukuaji wa uchumi ni suala la msingi kwa sababu ndio kigezo cha maendeleo ya nchi zote.  Mafanikio hayo yametokana na juhudi za pamoja za serikali wakiwemo, viongozi na wafanyakazi wote wa sekta zote na wananchi wote kwa jumla.  Nachukua fursa hii kutoa pongezi na shukurani zangu za dhati kwa wote hao.Aidha, nashukuru kuwa mwaka uliopita tuliendelea kushirikiana na washirika wetu wote wa maendeleo na waliendelea kutusaidia kwa kutupa misaada, mikopo na ushauri wa kitaalamu kwenye fani mbali mbali.  Kwa niaba ya wananchi wote, natoa shukurani zetu za dhati kwa washirika wetu hao na tutaendelea kuudumisha na kuukuza ushirikiano huu, hasa katika nyanja za uchumi na maendeleo ya jamii kwa faida yetu sote.
Ndugu Wananchi,
Kwa masikitiko makubwa katika mwaka tunaouaga tulishuhudia ongezeko la vitendo vya udhalilishaji wa wanawake na watoto vinavyofanywa na watu wachache katika jamii yetu ambavyo ni vya uvunjaji wa sheria na vinakwenda kinyume na maadili yetu, dini, mila, desturi na silka zetu.  Vitendo hivyo vimeendelea kuongezeka pamoja na juhudi zinazochukuliwa na Serikali za kuvidhibiti kwa njia mbali mbali.
Sisi wazee na walezi wa watoto, tuna wajibu mkubwa wa kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya watu wanaofanya vitendo hivyo.  Kama nilivyoeleza katika hotuba yangu ya tarehe 6 Disemba, 2014 katika uzinduzi wa kampeni ya kupiga vita ukatili na udhalilishaji wa wanawake na watoto kwamba kuanzia mwaka huu na miaka miwili ijayo, ni kipindi cha kuvitokomeza vitendo vya udhalilishaji kijinsia nchini kwetu.  Leo nairudia tena kauli yangu hio na natoa wito kwa wananchi wote tuazimie kuufanya mwaka mpya wa 2015 ni mwema na utakaokuwa na mafanikio katika kupinga udhalilishaji wa wanawake na watoto.  Tufanye juhudi hizi kwa kushirikiana katika familia, mitaa, vijiji na miji yetu yote. Kila mmoja wetu ana wajibu wake katika jambo hili.  Kwa hivyo, wazee, vijana, viongozi wa dini, siasa na jamii yote tushirikiane kuyapiga vita maovu haya katika jamii bila ya khofu au kuoneana muhali. Tusiwaonee haya watu wachache wanaowahadaa vijana wetu na kuwanyanyasa wanawake.  Nilisema siku ya uzinduzi wa kampeni ya kupiga vita ukatili na udhalilishaji wa wanawake na watoto, narudia kusema tena leo, wito wangu kwenu nyote, tuseme sasa na iwe basi.  Tusemeni kwa maneno na kwa vitendo.  Inshaallah Mwenyezi Mungu Karim atusaidie katika dhamira zetu za kuyapinga maovu haya ya udhalilishaji wanawake na watoto.
Ndugu Wananchi,
Pamoja na hayo niliyoyaeleza, natoa wito kwa wazazi na walezi wa watoto wetu kuwatunza na kuwapa malezi mema. Ni vyema tukawaandalia watoto wetu mazingira mazuri yakuyaendeleza maisha yao, nyumbani na mitaani.  Juhudi za kila mmoja wetu na juhudi za pamoja zinahitajika katika kuwapa watoto na vijana malezi mazuri, wayapende masomo yao na wafuate tabia njema za wazazi na walezi wao ili wajipambe nazo na zije ziwafae katika maisha yao.  Wazazi na Walezi wafuatilie kwa karibu nyendo za watoto wao, nani wanajumuika nao na nani wanashirikiana nao.
Ndugu Wananchi,
Kuhusu vijana, nawasihi waupokee mwaka mpya kuwa ni wa matumaini na matarajio mema.  Wasivunjike moyo kwa sababu ya uchache wa ajira ziliopo Serikalini na katika sekta binafsi.  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambua hali hiyo kama nilivyowaeleza vijana katika ufunguzi wa maonesho ya fursa ya ajira kwa vijana katika Hoteli ya Bwawani siku ya tarehe 22 Novemba, 2014. Hali hii inawakumba vijana wengi katika nchi nyingi duniani.  Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Kazi Duniani ya mwaka 2013, kuhusu ajira inakisiwa kuwa vijana milioni 73.4   duniani hivi sasa hawana ajira.  Idadi   hii   ni ongezeko la vijana milioni 3.5 kwa mwaka, tangu mwaka 2007.
Licha ya maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia yaliyofikiwa na mataifa mengi ya Ulaya, yaliyopelekea kuwepo kwa viwanda vya aina mbali mbali, bado tatizo la ajira kwa vijana, linaendelea kuwepo na katika baadhi ya nchi ni kubwa kuliko ilivyo katika nchi zetu za Afrika.  Ziko baadhi ya nchi za Ulaya zaidi ya asilimia 30 ya vijana wake hawana ajira.  Katika utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya uliofanywa mwaka 2009/2010. Zanzibar ilikisiwa kuwa na asilimia 17.1 ya vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 wasiokuwa na ajira.  Nataka vijana muyazingatie haya ninayoyaeleza, kwani huu ndio ukweli.
Katika jitihada za kuwawezesha vijana kujiajiri, tumeanzisha mfuko maalum wa kuwawezesha vijana kujiajiri kupitia miradi watakayokuwa nayo.  Kwa hivyo, mwaka 2015 uwe wa vijana kujishajihisha kutumia fursa zilizopo kujiendeleza na kujiajiri.  Serikali inayo wataalam wa kutosha wenye uwezo wa kutoa ushauri ufaao kwa vijana.
Ndugu Wananchi,
Katika mwaka tunaoukaribisha nchi yetu itakuwa na matukio kadhaa makubwa ikiwemo Kura ya Maoni ya Katiba iliyopendekezwa na Uchaguzi Mkuu. Mambo mengine muhimu tutakayokuwa nayo ni kukamilisha utekelezaji wa Mipango ya Milenia ya 2015, MKUZA II na Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2010-2015.  Mambo haya yote yanataka ushiriki wenu wananchi, ambao hautoweza kupatikana bila ya kudumisha amani na utulivu, utii wa sheria, mshikamano na kuvumiliana.  Sote kwa pamoja tunao wajibu wa kuyafanikisha mambo hayo kwa kuzingatia utekelezaji wa sera na mipango iliyowekwa. 
Ndugu Wananchi,
Kwa kumalizia, risala yangu ya Mwaka Mpya, nakumbusha kwamba, tarehe 12 Januari tutaadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, 1964.  Tutaanza sherehe za maadhimisho tarehe 02Januari kwa shughuli mbali mbali na natoa wito kwenu wananchi ili mshiriki kwa wingi katika shughuli hizi.  Aidha, kama kawaida yetu natoa wito tujitokeze na tushiriki kwa wingi katika kuzifanikisha sherehe hizi za mwaka huu. 
Ndugu Wananchi,
Kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, natoa salamu za mwaka mpya kwenu wananchi wote wa Zanzibar na Tanzania Bara na kwa ndugu na marafiki wetu wote kokote walipo.  Aidha, natoa salamu hizi kwa viongozi wa nchi marafiki na washirika wetu wa maendeleo na mashirika ya kimataifa kupitia mabalozi na wawakilishi wao waliopo nchini. Mwenyezi Mungu aujaalie mwka wa 2015 uwe wa kheri, Baraka, neema nyingi na amani, umoja na utulivu uendelee kudumu nchini kwetu. Tuendelee kupendana na kusaidiana katika kuyaendeleza maisha yetu.
Mungu atupe Baraka za Mwaka Mpya 2015
Ahsanteni

Kuhusu huyu aliyeuwawa kwa risasi Mahakamani Dar es salaam leo.

 Saa kadhaa zilizopita Polisi walimfyatulia risasi mtuhumiwa aliejaribu kutoroka baada ya kufikishwa kwenye Mahakama ya Kisutu Dar es salaam asubuhi ya December 31 2014.
Muda mfupi baadae Polisi ikatoa taarifa kwamba mtuhumiwa wa dawa za kulevya aliyeuwawa ni Abdul Koroma raia wa Sierra Leone na aliuwawa kwa risasi wakati akitoroka Mahakamani.




Panapo Fuka Moshi Kuna Moto..Habari za Millard Ayo Kujimilikisha Mrembo Jokate

Hakika hata siku moja huwezi kuuficha moto, kwani moshi lazima utakuumbua tu. Baada ya kuumizwa na aliekuwa mpenzi wake Millard Ayo baada ya kumfumania live Mwanza, Millard aliamua kukaa single kwa muda mtefu na kutokuwa na wazo la kupenda tena.

Mapenzi yake kwa Jokate yalianza kwa kificho na kwa usiri mkubwa hatimai imedhihilika kuwa mapenzi hayana siri baada ya kuanza kutoa picha zao ktk mitandao na kuonekana sehemu tofauti wakiwa wote, hasa ktk tuzo za Afrimama zilizofanyika South Africa.

Hii ni couple nzuri yenye kujua maisha hasa katika suala zima la kutafuta pesa licha ya kujituma kwa juhudi katika kazi zao.
Ikumbukwe Jokate ame sign mkataba usiokuwa na kikomo na kampuni ya wachina yenye thamani ya Tshs 8.2 billion

Stori zote muhimu zilizoandikwa kwenye Magazeti ya leo Tanzania Dec 31, 2014 Nimekuwekea hapa

JAMBOLEO
Mtu mmoja aliyekua ameandaliwa mazishi baada ya madai kuwa amefariki Wilayani Kiteto, Manyara ameonekana hai na kushangaza waombolezaji waliokua wanajiandaa na mazishi hayo.
Akizungumza kwa njia ya simu Diwani wa Kata Matui Othamn Kidawa alisema walipata taarifa za kuuawa kwa ndugu huyo na wenzake shambani na kuamua kuubeba mwili wa marehemu.
“Tulipofika shambani tulikuta uharibifu mkubwa uliofanywa na watu wanaodaiwa kuwa ni wafugaji na kuteketeza nyumba nne kwa moto na mali zote zilizokuwemo ndani”alisema.
Alisema wakiwa na askari waliokua na taarifa za kifo na wananchi waliofanikiwa kumpata majeruhi mmoja na baadaye Hassan Abdalah alidaiwa kufa.
Kwa mujibu wa Abdalah alisema alinusurika kuuawa baada ya kuvamiwa saa mbili usiku na wamasai waliowataka waondoke eneo hilo kwa madai kuwa ni eneo la malisho.
Alisema alipokua njiani alipokea taarifa kwa njia ya simu kuwa ndugu zake wameandaa mazishi kwa ajili yake na tayari walichimba kaburi na maandalizi mengine.
NIPASHE
Mtotomwenye ulemavu wa ngozi ‘Albino’ Pendo Emannuel mwenye miaka minne ameibiwa katika kijiji chaoWilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza akiwa amelala na wazazi wake.
Kamanda wa Polisi Mwanza ValentinoMlowola alisema tukio hilo lilitokea Desemba 27 baada ya watu haokuvunja mlango kwa kutumia jiwe maarufu Fatuma nakuingia ndani.
Alisema watu hao baada ya kumchukua mtoto waliondoka kwa kasi wakitumia pikipiki na kutokomea pasipojulikana na askari kupata taarifa majira ya saa 7 usiku na kuanza kumsaka.
Mlowola alisema askari wake kwa kushirikiana na familia hiyo itamsaka mtoto huyo popote pale aidha akiwa amekufa ama mzimana kuhakikisha wahusika wanachukuliwa hatua kali.
NIPASHE
Kikao baina ya Waziri Mwakyembe na wadau wa Bandari ya Dar es salaam kimeibua ufisadi unaodaiwa kufanywa na kampuni ya kupakua na kupakia mizigo bandarini yaTICTS ambao umekua ukiwaumiza wateja wanaotumia bandari hiyo.
Ufisadihuo ambao uliibuliwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha wakala wa forodha na uondoshaji wa shehena Tanzania TAFFA,Edward Urio unadaiwa kufanywa na TICTS kwa kuwatoza wateja wa bandari hiyo viwango vya ubadilisha dola ya Marekani kwenda Shilingi ya Tanzania kinyume cha utaratibu wa nchi.
Waziri Mwekyembe amemwagiza Mtendaji mkuu wa TICTS na menejimenti yake kwenda ofisini kwake leo wakiwa na maelezo ya kutosha kwanini wanakiuka taratibu za nchi na wameanza lini kufanya hivyo.
Kabla ya kutoa maelezohayo Mwakyembe alitaka kujua kutoka Sumatra kamawanataarifa na kashfa hiyo na walithibitisha wanazo na kwamba wamekwisha kuindikia TICTS barua kuhusiana na suala hilo na Meneja wa TICTS alithibitisha kupokea barua hiyo.
MWANANCHI
Mkazi wa Geita aliyekua mjamzito wa miezi saba Meleciana Kubezya mwenye miaka 35 ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na watu wasiofahamika chanzo kikitajwa kuwa ni imani za kishirikina na kugombania mashamba ya urithi.
Diwani wa Kata ya Bukombe alisema mauaji hayo yalitokea saa 2 usiku wakati mjamzito huyo akiwa nyumbani kwake na watoto wake wakati watu hao walipokua wakipita huku wakitafuta ng’ombe wao aliyepotea.
Alisema binti wa marehemu alisema hawajaona ng’ombe aliyepotea ndipo watu hao walipomba maji ya kunywa kwa madai wamechoka sana kutokana na kuwatafuta kwa muda mrefu na alipokwenda kufata maji ndipo walitumia muda huo kumuua mama yake.
“Walipogundua amepoteza maisha walikimbia kusikojulikana na wakati wanampiga aliwauliza kwa nini mnanipiga…?,kosa langu ni lipi kwanini mnaniua,lakini hauaji hao hawakutaka kumsikiliza…
MWANANCHI
Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mbeya imegundua viwanja na nyumba zaidi ya 10 za Serikali zikitumiwa na watu binafsi katika mazingira ya kutatanisha.
Nyumba zilizoubwa na utata huo zipo maeneo ya Uzunguni,Uhindini na Mwanjelwa moja ikiwa na vyumba vitano pamoja na maduka.
Pia imegundua mashamba yake yalilimwa mazao mbalimbali na watu binafsi katika maeneo ya Foresy ya zamani na mpya.
Katibu Tawala msaidizi Hamis Kaputa jana kuwa taarifa zaidi ya nyumba hizo zitatolewa na aliyekua Mwenyekiti wa tume ya uchunguzi ambaye kwa sasa yupo likizo.
Alisema taarifa ya tume ilishaandaliwa na kupelekwa kwa Waziri mkuu Pinda ambaye ndiye aliyetaka apatiwe matokeo ya kazi hiyo.
MWANANCHI
Mvua kubwa isiyotabirika inatarajiwa kunyesha sehemu mbalimbali nchini hasa ukanda wa Pwani ya Kaskazini maeneo ya jijini Dar es salam,Unguja na Pemba pia katika ukanda wa Kaskazini Mashariki kwa Mikoa ya Kilimanjaro,Arusha na Manyara.
Akitoa taarifa hiyo ya hali ya Hewa,Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA Agnes Kijazi alisema mvua ya msimu katika maeneo hayo inatarajiwa kuisha leo.
Hata hivyo alisema mvua kubwa ya nje ya msimu inatarajia kuanza kipindi cha Januari 2015 na itaikumba pia Mikoa ya Mwanza,Kagera,Shinyanga na Geita.
Alisema mvua hiyo inasababishwa na ongezeko la joto linalolifanya anga kushindwa kutengeneza unyevunyevu ambao hugeuka kuwa mvua.
“Ninawashauri wananchi kuchukua hatua za kujikinga na athari za kiafya na mazingira zinazoweza kusababishwa na ongezeko la joto linaloendelea sambamba na mvua kubwa kunyesha”alisema.
MTANZANIA
Aliyekua Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijukaamesema hayuko tayari kujiuzulu ujumbe wa kamati kuu ‘CC’ ya Chama cha Mapinduzi.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya Rais Kikwete kutangaza kumfuta kazi katika mkutano wake na wazee wa Dar es saalam uliofanyika Decemba22 mwaka huu.
Karibu msaidizi Kazi maalum wa Tibaijuka,Nassor Hussein alisema suala la Tibaijuka kujiuzulu nafasi yake ya Ujumbe wa CCM lipo chini ya viongozi wa Kitaifa wa Chama hicho ambao hao ndio watakaoamua.
“Tibaijuka hayupo tayari kujiuzulu kwa sasa ujumbe wa kamati kuu,anachosubiri ni uamuzi wa Chama,jambo hilibado lipo kwa wakubwa na ni siri kwa kuwa lipo kiutendaji,hivyo litaamuliwa na kamati kuu ya chama husika”alisema

Rekodi ya List ya Collabo za Muziki zilizofanya vizuri mwaka 2014 iko hapa mtu wangu

Ikiwa imebaki saa chache kumaliza mwaka, tathimini bado zinafanyika kwa mambo ambayo yametokea mwaka mzima.
Burudani mara zote imekuwa karibu na maisha yetu, ikiwemo muziki.
Kwenye rekodi mbalimbali zilizovunjwa kwa kufanya vizuri mwaka huu, ipo hii ya list yaTop Ten ya zile Collabo zitakazokumbukwa zaidi kwa kufanya vizuri Mwaka 2014 kwenye muziki.
  1. Hangover- Psy feat. Snoop Dogg.
  2. Flawless (Remix)- Beyonce feat. Nicki Minaj.
  3. Sing- Ed Sheeran feat. Pharrell Williams.
  4. Uptown Funk- Mark Ronson feat. Bruno Mars.
  5. Bang Bang- Jessie J feat. Ariana Grande & Nicki Minaj.
  6. Love Never Felt So Good- Michael Jackson feat. Justin Timberlake.
  7. Can’t Remember to Forget You- Shakira feat. Rihanna.
  8. Fancy- Iggy Azalea feat. Charli XCX.
  9. Dark Horse- Katy Perry feat. Juicy J.
  10. Ew!- Jimmy Fallon feat. Will.i.am.
Kilichonishtua kwenye list hii kuna majina machache sana ya mastaa.
Kwako mtu wangu, nikikuomba uangalie muziki wa Bongo 2014 halafu uniandalie list ya Top 3 ya Collabo ulizozipenda utaipangaje? Nitafurahi ukiniandikia.

SAA 24 ZA BURUDANI DAR LIVE, NJOO TUFUNGE NA KUFUNGUA MWAKA 2015


Rais mpya wa Tunisia kuapishwa


 Rais mteule wa Tunisia Beji Caid Essebsi anatarajiwa kuapishwa baada ya kushinda uchaguzi wa kwanza uliokuwa huru nchini humo.
Alimshinda rais aliyekuwa mamlakani Moncef Marzouk.
Ushindi wake unaaminisha kwamba Tunisia ndilo taifa ambalo limejinasua kutoka utawala wa kiimla hadi ule wa kidemokrasia.
Siku ya jumatatu,tume ya uchaguzi ilithibitisha kuwa bwana Essebsi alishinda kura ya raundi ya pili dhidi ya Marzouk.
Rais huye mteule ataapishwa katika bunge la wawakilishi wapwa ambapo chama chake Nidaa Tounes kimepata wabunge wengi.
Tayari maandalizi ya kumuapisha yamekamilika mjini Tunis.
Hatua hiyo hiyo itafikisha tamati mvutano wa demokrasia wa miaka minne ya ghasia zilizoghubika taifa hilo zilizopeleekea kung'olewa kwa utawala wa Rais Zine el-Abedine Ben Ali.
Bwana Essebsi alihudumu katika utawala wa Ben Ali, pamoja na uongozi wa rais wa zamani Habib Bourguiba.                                


AJALI YA MOTO HANDENI

Lori la mafuta likiteketea kwa moto mara baada ya kugonga nguzo ya umeme maeneo ya Amasia huko Handeni mkoani Tanga 


Wananchi wakishuhudia moto mkubwa uliozuka katika ajali hiyo

CCM kutumia panga la 2005


Dar es Salaam. Vigezo 13 vilivyowekwa na CCM katika Uchaguzi Mkuu wa 2005 kumpima mwanachama anayefaa kugombea urais, ndivyo vitakavyotumika kuwaengua makada wanaoendelea kujitokeza kuwania nafasi hiyo mwakani, imefahamika.
Vigezo hivyo vinaonekana kuwa kizingiti kwa baadhi ya makada wa chama hicho ambao tayari wametangaza na wengine wanaotajwa kutaka nafasi hiyo ya juu nchini, ukiachilia mbali mnyukano unaotarajiwa kutoka vyama vya upinzani vinavyoonekana kupata nguvu.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula amelithibitishia gazeti hili kwamba, “Sifa hizo 13 zilizotumika mwaka 2005 na 2010 ndizo zitakazotumika pia mwaka 2015 na wala hakutakuwa na maboresho wala nyongeza ya aina yoyote.”
Vigezo hivyo viliwekwa ili kuhakikisha chama hicho kinampata mgombea asiyetiliwa shaka juu ya vitendo vya uadilifu, mwenye uzoefu wa uongozi serikalini, atakayedumisha muungano, mwenye upeo wa masuala ya kimataifa, mtetezi wa wanyonge, asiyejilimbikizia mali na mwajibikaji, mambo ambayo hata hivyo, bado yameibua mjadala iwapo yanazingatiwa au la.
Pia anayetakiwa lazima awe mwenye kuzitetea sera za CCM, anayekubalika na wananchi, asiye na hulka ya udikteta au ufashisti, mwenye uwezo wa kufanya uamuzi wa busara na kiwango cha elimu ya chuo kikuu au inayolingana nayo.
Licha ya vigezo hivyo, baadhi ya makada waliokwishajitokeza na wengine wanaotajwa wanaonekana dhahiri kukosa baadhi sifa hizo na wengine wako ‘kifungoni’ kwa miezi 12 baada ya kupewa onyo kali kwa kufanya kampeni mapema na kujihusisha na vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya chama na jamii.
Vigogo wa CCM ambao wanatajwa kutaka kupewa ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho ambao iwapo watachukua fomu, watatazamwa kwa vigezo hivyo ni Mbunge wa Nzega, Dk Khamis Kigwangalla, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba ambao wamekwishatangaza kuwania nafasi hiyo.
Wengine ambao wanatajwa ingawa hawajatangaza nia hadharani ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa; Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa; Bernard Membe; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu); Stephen Wasira na aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.
Wachambuzi wanavyosema
Akizungumzia vigezo hivyo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Danford Kitwana alisema CCM inajua kuwa hakuna mgombea anayeweza kuwa na sifa zote 13, kwa hiyo inapaswa iangalie ni nani anawazidi wengine.
“Kigezo cha kuwa na sifa ya maadili ndicho kinachowakwamisha wengi, pia hakuna mgombea anayeweza kuwa na sifa zote zilizowekwa na chama, mwingine anaweza kuwa na sifa saba, nne au tano.
“Wakitumia mfumo wa kuwatazama wagombea wao kwa idadi ya sifa, mtu mwenye sifa nyingi ndiye asimamishwe kugombea.”Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Dk Emmanuel Mallya alisema Tanzania inahitaji kuongozwa na rais mwenye historia ya uadilifu wa matumizi ya fedha za umma.
“Tunahitaji kiongozi anayeweza kusimamia fedha za umma, si mtu anayenunua vitu ovyo bila kujali Hazina kuna kiasi gani, hilo ni tatizo kubwa,” alisema Dk Mallya.
Aliongeza kuwa, kiongozi huyo lazima awe mchapakazi anayeweza kuwaletea wananchi maendeleo, lakini watu wengi wamekuwa wakisema wanamtaka mtu mwadilifu bila kuzungumzia uwezo wake wa kufanya kazi.
Mwalimu mstaafu wa shule ya msingi, Rehema Mathayo alisema kutokana na baadhi ya viongozi ndani ya CCM kukumbwa na kashfa za ufisadi, anayetaka kugombea urais lazima awe ‘msafi’ ndani na nje ya chama.
“Mshindi ndani ya chama ni mtu atakayekuwa amewashinda wenzake kwa kuwa na maadili mazuri na asiwe na doa lolote la kujishughulisha na ‘dili’ za ajabu,” alisema Rehema.
Mwalimu huyo aliongeza kuwa mgombea huyo lazima awe na uzoefu mkubwa wa masuala la kimataifa kwa kuwa hata kama atakuwa na maadili, kama hafahamu namna ya kuwaunganisha wananchi na jumuiya za kimataifa, hatakuwa na manufaa.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dk Ernest Mwasalwiba alisema kutokana na kuporomoka kwa maadili hususan kwa viongozi wa umma, vitendo vya rushwa na kadhia mbalimbali, rais ajaye anatakiwa kuhakikisha yale anayoyasema ndiyo anayatenda na Watanzania hawahitaji Rais dikteta.
“Masuala ya maadili, rushwa, yote haya yanazuiwa mpaka sasa lakini suala ni usimamizi tu... ni wakati sasa wa rais ajaye kuonyesha ajenda yake itakuwa ipi, anapokuwa amesema kitu kila mtu lazima afuate mfano akisema anachukia rushwa na maadili kwa yaheshimiwe isiwe ni mjadala kila mtu anafuata kuanzia chini hadi juu.
“Dikteta siyo kiongozi tunayemtaka, bali tunataka kiongozi atakayesimamia sheria na mifumo iliyopo iweze kufanya kazi ipasavyo... mfano Rais Jakaya Kikwete kipindi anaingia aliingia na kaulimbiu ya ‘Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya’ ambayo ilifuatwa hadi na viongozi wa halmashauri.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dk Romanus Dimoso alisema: “Sifa za rais huwa zinajulikana. Tunahitaji rais ajaye anayejua hali ya kisiasa ilivyo kwa sasa, hatutaki rais ambaye hatambui mchango unaotolewa na vyama vingi vya siasa na jinsi atakavyoweza kufanya navyo kazi hususan kwa kuhakikisha demokrasia inazingatiwa.”
Aliongeza: “Je, malengo ya anayetaka urais yale ya kuhakikisha ifikapo mwaka 2025 nchi hii inafikia uchumi wa kati. Amejipanga vipi kama mtumishi wa kwanza wa Taifa hili kutufikisha huko?... Hatutaki mtu awe rais tu kwa jina.”
Rais mstaafu wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Primus Saidia alisema: “Tunahitaji rais anayeweza kufanya uamuzi mgumu kwa mustakabali wa Taifa, asiwe rais wa maneno maneno, bali wa vitendo. Anasema dawa hospitalini hakuna na kesho zinakuwapo.“Tunataka mtu mwenye historia ya uongozi, ameshawahi kufanya nini katika kuboresha sekta ya afya, elimu, uchumi na kijamii? Alishafanya maamuzi magumu yapi ambayo kila mmoja aliyaona na aliyaheshimu?”

Tuesday, December 30, 2014

uwanja wa ndege wa JK AIBU



ulikua unavuja wakati mvua inanyesha.

Simba yamfukuza kazi kocha Patrick Phiri .

Siku chache baada ya kupoteza mchezo wake wa nane katika mfululizo wa ligi kuu ya Tanzania bara klabu ya Simba imeamua kumfukuza kazi kocha wake mkuu Mzambia Patrick Phiri baada ya kuwa naye kwa muda wa miezi minne tangu alipojiunga na timu hiyo katikati ya mwezi wa saba .
Phiri amefukuzwa kazi baada ya mabosi wa simba kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo ambayo imefanya usajili mkubwa wakati ligi iliposimama hali iliyopandisha matarajio ya mashabiki na viongozi hali iliyobadilika wakati walipocheza mchezo wao dhidi ya Kagera .
Phiri amefukuzwa kazi pamoja na msaidizi wake wa kwanza ambaye ni nahodha wa zamani wa timu hiyo Suleiman Matola ambaye amekuwa na timu hiyo kwa muda mrefu tangu wakati wa Dravko Logarusic na kabla ya hapo alikuwa akiifundisha timu ya vijana .
                  Kocha Mzambia Patrick Phiri akiwa mazoezini wiki chache kabla ya kufukuzwa kazi
Maamuzi hayo yalifanyika usiku wa jana kuamkia leo kwenye kikao kilichofanyika kwenye hoteli ya Double Tree Masaki jijini Dar-es-salaam ambapo viongozi wa juu wa klabu hiyo kwa kauli moja walikubaliana kuwafukuza kazi makocha hao wawili .
Tetetsi zaidi zinahabarisha kuwa nafasi ya Patrick Phiri itakwenda kwa kocha raia wa Serbia ambaye ni Goran Kapunovic  huku msaidizi wake akitarajiwa kuwa kocha Mrwanda Jean Marie Ntagwabira .
Taarifa zaidi zinasema kuwa Suleiman Matola ataendelea kuwa ndani ya klabu ya Simba ambapo atarudi kwneye nafasi yake ya zamani kama kocha wa timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 .

Kwa dalili hizi huenda ndege ya AirAsia ilianguka eneo hili…

                             Baadhi ya wahusika wa vikosi vya Utafutaji wa ndege hiyo, Indonesia.

vyombo mbalimbali vya habari vya Kimataifa vimeanza kuripoti kuhusu kinachoendelea kwa sasa katika hatua za utafutaji wa ndege ya AirAsia QZ8501 iliyopotea siku ya juzi December 28 ikitokea Indonesia kwenda Singapore.
Vikosi vya utafutaji vimetoa taarifa kwamba kuna mabaki mbalimbali ya ndege ambayo yamepatikana yakiwa yanaelea juu ya maji ya bahari katika eneo ambalo ndege hiyo ilipoteza mawasiliano.
Mkurugenzi wa Shirika la anga Indonesia Djoko Murjatmodjo amesema kuna baadhi ya vitu vimeonekana ikiwemo mwili wa mtu mmoja ukiwa unaelea baharini pamoja na mabaki ambayo bado hawajathibitisha kama ni ya ndege hiyo ambayo ni mlango wa abiria na mlango wa sehemu ya kupakilia mizigo.


Nimekuwekea hapa Stori muhimu zilizopewa Headlines kwenye Magazeti ya Leo Tanzania December 30, 2014


MWANANCHI
Mkazi wa Wilaya ya Kilombero,Morogoro Amon Nyenja amefariki dunia baada ya kuchomwa na kisu na anayedhaniwa kuwa ni hawara wa mke wake mdogo.
Ofisa Mtendaji wa kata ya Mang’ula Shabaan Lichaula  na Mkuu wa kituo cha Polisi Nkilijia Lazaro walisema Polisi inamshikilia mwanamke huyo ambaye ni mke wa marehemu wakati wakimsaka mtuhumiwa.
Lichaula alidai marehemu katika kumtafuta mkewe alimkuta amesimama mahali na mwanaume huyo na baadaye mwanamke huyo alikimbia na kutokomea na marehemu kuamua kumvaa mgoni wake lakini alizidiwa baada ya mtu huyo kumchoma kisu cha ubavuni hadi utumbo kutoka nje.
Alisema baada ya marehemu kuchomwa kisu alipiga kelele za kuomba msaada na wasamaria wema walijitokeza na kumwahisha hospitali na alifariki dunia baada ya kufanyiwa huduma ya kwanza wakati akihamishiwa katika hospitali Mtakatifu Fransis,Ifakara kwa matibabu zaidi.
MWANANCHI
Washtakiwa 11 wa kesi ya mauaji ya kukusudia ya aliyekua mjumbe wa tume ya mabadiliko  ya Katiba,Dk Sengondo Mvungi jana waligoma kwa muda kuondoka kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu wakishinikizwa kuelezwa lilipo jalada la kesi yao na hatua ilipofia.
Hilo lilitokea jana saa nne asubuhi ,muda mfupi  baada ya wakili wa serikali,Peter Njikekumweleza Hakimu Hellen Liwa kuwa kesi hiyo ilifika mbele yake kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wake bado haujakamilika na kuomba ipangwe tarehe nyingine.
Mshtakiwa Masunga Makenza alidai hafahamu sheria ,kesi hiyo ni ya muda mrefu na akahoji jalada likienda kwa DPP linatakiwa kukaa kwa muda gani.
Makenza alidai kuwa kesi hiyo ni ya kubambikiwa na kwamba ingekuwa halisi,upande wa mashtaka ungekuwa umekwishakamilisha upelelezi na kwamba wapotayari kushtakiwa ila kama upande wa mashtaka umeshindwa kukamilisha upelelezi mahakama iwaachie huru na ikikamilisha iwakamate tena.
MWANANCHI
Ikiwa imebaki takribani miezi 1o kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu mwakani,Chama cha CCM kinaonekana kuteswa na tuhuma za rushwa inayodaiwa kutolewa na makada wake wanaotajwa kutaka kuwania nafasi mbalimbali ukiwemo urais.
Hali hiyo inabainishwa nabaadhi ya makada wa Chama hicho katika ngazi mbalimbali ambao wameamua kulalamika waziwazi kupitia vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii.
Moja ya kauli ni iliyotolewa na Mbunge wa Bukoba Mjini Khamis Kagasheki kwenye akaunti yake ya Twitter akisema “Mgawo wa Xmass na mwaka mpya kwa wajumbe wa husika wa CCM ni kucheza na ugumu wa maisha uliopo,ni ununuzi wa nafasi na si uwezo wa ongozi, aibu”.
Alipotakiwa kufafanua Kagasheki alisema hakumtaja mtu licha ya kwamba wapo wengi wanaotoa zawadi,lakini baada ya kuandika kwenye mtandao ameandamwa na baadhi ya watu huku wengine wakimtolea lugha chafu.
“Hii ni line yangu naitumia kutoa mawazo siku zote,lakini nashangaa leo watu wameshikia kidedea maoni hayo mpaka wengine wanatumia lugha kali..sijamtaja mtu kwa sababu najua wapo wengi wanaotoa zawadi”alisema.
HABARILEO
Msichana mmoja mkazi wa mtaa wa Zaire Mkoani Arusha,amelazwa katika hospitali ya Mount Meru Arusha chini ya ulinzi mkali wa polisi baada ya kujizalisha mwenyewe kisha kumtumbukiza mtoto kwenye ndoo ya maji.
Baba mwenye nyumba ambayo binti huyo alikua amepanga chumba cha kuishi,Ruben Mollel alisema msichana huyo alikua anajulikana kwa jina la Dada Pendo na kwamba maisha yake hayakua wazi.
“Alipokuja kupanga hapa alidai yeye ni mwanafunzi,ila hivi karibuni alionekana kuwa mjamzito,hakuna kilichojulikana tena hadi jana ambapo nyumba hii ilizingirwa na wanakijiji ambao hatimaye waligundua kitoto kilichadhaniwa kuwa ni chake kikiwa kimezamishwa kichwa chini kwenye ndoo ya maji”alisema baba huyo mwenye nyumba.
Taarifa za uwezekano wa kuwepo mtoto huyo ndani ya nyumba ya dada huyo ziliibuliwa na mpangaji mwenzake Mama Martha ambaye alidai kuwa alisikia sauti ya mtoto akilia usiku kucha na baadaye kutoweka majira ya asubuhi.
Baada ya juhudi za kuchunguza walikuta kichanga hicho cha kiume kikiwa ndani ya ndoo na tayarikilikua kimefariki dunia huku mama yake akiwa katika hali mbaya kutokana na kujizalisha mwenyewe.
HABARILEO
Mvua iliyonyesha jijini Dar es salam imeleta balaa baada ya kuua watu wawili katika maeneo tofauti ya jiji hilo likiwemo tukio la mtoto wa miaka minne kufa baada ya kuzidiwa na maji yaliyoingia ndani ya nyumba wakati akiwa amelala.
Kwa mujibu wa Taarifa ya kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar Camilius Wambura alisema matukio hayo yalitokea jana mchana kwenye maeneo mawili tofauti.
Tukio la kwanza lilitokea eneo la Tandale ambapo mtoto Nasma Ramadhani akiwa amelala ndani ya nyumba yao maji ya mvua yaliingia ndanina kumzidia nguvu hadi kufariki na mwingine bibi kizee kufariki eneo la Mwananyamala aliyeangukiwa kichwani na ukuta wa nyumba yake na kumsababishia mauti.
Wambura alisema madhara mengine ni maji kujaa kwenye ameneo mbalimbali ikiwemo Mikocheni zilizopo ofisi za Tanesco,Kinondoni jirani na TMJ hivyo kuleta usumbufu wa Magari na watukuvuka eneo hilo.
MTANZANIA
Iliyokua ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Iringa iko katika matengenezo baada ya Wizara ya Maliasili kuridhia itumike kama jengo la Makumbusho ya Taifa.
Mkuu wa Wilaya hiyo na msaidizi wake  wamehamia katika jengo jipya lililojengwa kwa zaidi ya shilingi bilioni 1.8 katika eneo la Mawelewele mjini hapa.
Ukarabati wa jengo hilo lililojengwa na Serikali ya Ujerumani  zaidi ya miaka 114 iliyopita utafanywa na mradi wa kuendeleza utamaduni Nyanda za juu Kusini.
“Mradi huu wa Utalii ambao ni wa mamilioni ya pesa utahusisha ukarabati na uhifadhi wa iliyokua boma ya Iringa enzi za Utawala wa Kijerumani”alisema Meneja mradi Jan Kuever.
NIPASHE
Shinikizo dhidi ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospter Muhongo  limezidi kushika kasi baada ya Jukwaa la Katiba Tanzania JUKATA kumuomba Rais Kikwete kumwajibisha ili kupisha nafasi hiyo ili ichukuliwe na mtumishi mwenye sifa ya kutumikia umma.
Kikwete alisema katika hotuba yake kupitia wazee wa Mkoa wa dar es salaam kuwa amemuweka kiporo Muhongo kwa siku mbili hadi tatu kwa kuwa uchunguzi dhidi yake ulikua unaendelea.
Hatahivyo tangu siku hiyo zimeshapita siku tisa bila rais  kutangaza hatma ya Muhongo kama anatimuliwa ama anabaki katika nafasi yake.
Jukata wamemuomba Kikwete wamemuomba Kikwete kuchukua hatua dhidi ya Waziri huyo kutokana na kuhusishwa na kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow.

NYALANDU ATANGAZA RASMI KUWANIA URAIS 2015

                                                                Mbunge wa Singida Kaskazini, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ametangaza rasmi kuwania Urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu mwakani.

Amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuona kwamba anao uwezo wa kuiongoza Tanzania, katika harakati za kuwafikisha kwenye maendeleo endelevu wanayotaka Watanzania.

Amesema, yuko tayari kushindanishwa na Watanzania wengine watakaoona kuwa wanafaa kuwa Rais, lakini akisema kwanza kila atakayejitokeza itabidi kazi zake zipimwe kwa moto na endapo zitayeyuka hafai.

Nyalandu ambaye alitangaza uamuzi huo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo jimbo la Singida Kaskazini, alisema, yeye anaingia kwenye kinyang'anyiro akiwa kifua mbele kutokana na kuamini kwamba amekwishafanyakazi zilizotukuka.

"Kazi zangu nilizofanya zinajulikana na ninaziamini kwamba ni nzuri, hivyo yeyote atakayetaka urais apimanishwe na mimi kwa kupimwa kazi zetu kwa moto", alisema Nyalandu

Itakapofika siku ya siku, nitaenda Dodoma nikisindikizwa na wana Singida Mashariki, na wengine wengi kutoka pembe zote za Tanzania, kwenda Dodoma kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea Urais kwa tiketi ya CCM", alisema.

Mkutano huo wa jimbo ambao ulipambwa na shamrashamra mbalimbali zikiwemo za wasanii wakiwemo kina Rose Mhando, ulifurika maelfu ya wananchi waliohamasika kumsikiliza Nyalandu.

HABARI KATIKA PICHA, NYALANDU AKITANGAZA KUWANIA URAIS