Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania imetoa ripoti ya tathmini ya majaribio ya matumizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura (Pilot Registration) kwa mfumo wa Biometric Voters Registration (BVR) uliofanyika wiki moja iliyopita.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva amesema kwamba zoezi la Majaribio la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lilifanyika kwa siku saba (7) katika Kata za Bunju na Mbweni katika Jimbo la Kawe, Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam; Kata za Ifakara, Kakingiuka, Ipangala, Mlabani na Viwanja Sitini katika Jimbo la Kilombero Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro; na Kata za Ikuba, Usevya na Kibaoni katika Jimbo la Katavi, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi.
Katika zoezi hilo la majaribio Jumla ya BVR Kits 250 zilitumika katika Uboreshaji huo kwa mgawanyo ufuatao:- Halmashauri ya Kilombero BVR Kits 80, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele BVR Kits 80 na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni BVR Kits 90. Vituo katika Kata zote vilikuwa vinafunguliwa saa 2.00 asubuhi na kufungwa saa 12.00 jioni.
“Katika majaribibio hayo idadi kubwa ya watu ilijiokeza kujiandikisha Mkoa wa Dar es salaam, Kata za Bunju Wapiga Kura 15,123 waliandikishwa kati ya 27,148 na Kata ya Mbweni Wapiga Kura 6,200 waliandikishwa kati ya 8,278. Takwimu hizi za waliondikishwa inatokana na makisio ya watu tuliyokuwa tumejiwekea kutokana na matokeo ya sensa mwaka 2012″.Alisema Luuva
Mkoa wa Morogoro Kata za Ifakara, Kakingiuka, Ipangala, Mlabani na Viwanja Sitini Wapiga Kura walioandikishwa ni 19,188 wakati makisio yalikuwa watu 17,790 na Mkoa wa Katavi Halmashauri ya Mlele kata za Ikuba, Usevya na Kibaoni Wapiga Kura 11,210 waliandikishwa wakati makisio yalikuwa watu 11,394. Matokeo haya yanadhihirisha kuwa vifaa vya uandikishaji vilifanya kazi vizuri
Kwa upande mwingine Jaji Lubuva amesema majaribio ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika majimbo matatu yaliyotajwa yameonesha mafanikio pamoja na changamoto mbalimbali.
Akizungumzia Changamoto amesema , changamoto kadhaa wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo zimoenekana ambazo ni Matatizo yaliyotokana na ’Settings’ za BVR Kits,baadhi ya ”BVR Kits” zilitumia camera iliyo katika Laptop badala ya camera iliyowekwa kwa ajili ya kupiga picha. Uchukuaji wa alama za vidole (Automatic Process settings) ilisababisha Mfumokusimama(Crash).
Changamoto nyingine ni tatizo la kuchukua picha iwapo viwango vya ICAO vya ubora wa Picha havijafikiwaMatatizo yaliyosababishwa na Software. Fingeprint Scanner kusababisha Mfumo wa Uandikishaji kusimama (Crash) kutokana na SDK na za vifaa finger print scanner.
No comments:
Post a Comment