Wednesday, December 31, 2014

Stori zote muhimu zilizoandikwa kwenye Magazeti ya leo Tanzania Dec 31, 2014 Nimekuwekea hapa

JAMBOLEO
Mtu mmoja aliyekua ameandaliwa mazishi baada ya madai kuwa amefariki Wilayani Kiteto, Manyara ameonekana hai na kushangaza waombolezaji waliokua wanajiandaa na mazishi hayo.
Akizungumza kwa njia ya simu Diwani wa Kata Matui Othamn Kidawa alisema walipata taarifa za kuuawa kwa ndugu huyo na wenzake shambani na kuamua kuubeba mwili wa marehemu.
“Tulipofika shambani tulikuta uharibifu mkubwa uliofanywa na watu wanaodaiwa kuwa ni wafugaji na kuteketeza nyumba nne kwa moto na mali zote zilizokuwemo ndani”alisema.
Alisema wakiwa na askari waliokua na taarifa za kifo na wananchi waliofanikiwa kumpata majeruhi mmoja na baadaye Hassan Abdalah alidaiwa kufa.
Kwa mujibu wa Abdalah alisema alinusurika kuuawa baada ya kuvamiwa saa mbili usiku na wamasai waliowataka waondoke eneo hilo kwa madai kuwa ni eneo la malisho.
Alisema alipokua njiani alipokea taarifa kwa njia ya simu kuwa ndugu zake wameandaa mazishi kwa ajili yake na tayari walichimba kaburi na maandalizi mengine.
NIPASHE
Mtotomwenye ulemavu wa ngozi ‘Albino’ Pendo Emannuel mwenye miaka minne ameibiwa katika kijiji chaoWilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza akiwa amelala na wazazi wake.
Kamanda wa Polisi Mwanza ValentinoMlowola alisema tukio hilo lilitokea Desemba 27 baada ya watu haokuvunja mlango kwa kutumia jiwe maarufu Fatuma nakuingia ndani.
Alisema watu hao baada ya kumchukua mtoto waliondoka kwa kasi wakitumia pikipiki na kutokomea pasipojulikana na askari kupata taarifa majira ya saa 7 usiku na kuanza kumsaka.
Mlowola alisema askari wake kwa kushirikiana na familia hiyo itamsaka mtoto huyo popote pale aidha akiwa amekufa ama mzimana kuhakikisha wahusika wanachukuliwa hatua kali.
NIPASHE
Kikao baina ya Waziri Mwakyembe na wadau wa Bandari ya Dar es salaam kimeibua ufisadi unaodaiwa kufanywa na kampuni ya kupakua na kupakia mizigo bandarini yaTICTS ambao umekua ukiwaumiza wateja wanaotumia bandari hiyo.
Ufisadihuo ambao uliibuliwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha wakala wa forodha na uondoshaji wa shehena Tanzania TAFFA,Edward Urio unadaiwa kufanywa na TICTS kwa kuwatoza wateja wa bandari hiyo viwango vya ubadilisha dola ya Marekani kwenda Shilingi ya Tanzania kinyume cha utaratibu wa nchi.
Waziri Mwekyembe amemwagiza Mtendaji mkuu wa TICTS na menejimenti yake kwenda ofisini kwake leo wakiwa na maelezo ya kutosha kwanini wanakiuka taratibu za nchi na wameanza lini kufanya hivyo.
Kabla ya kutoa maelezohayo Mwakyembe alitaka kujua kutoka Sumatra kamawanataarifa na kashfa hiyo na walithibitisha wanazo na kwamba wamekwisha kuindikia TICTS barua kuhusiana na suala hilo na Meneja wa TICTS alithibitisha kupokea barua hiyo.
MWANANCHI
Mkazi wa Geita aliyekua mjamzito wa miezi saba Meleciana Kubezya mwenye miaka 35 ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na watu wasiofahamika chanzo kikitajwa kuwa ni imani za kishirikina na kugombania mashamba ya urithi.
Diwani wa Kata ya Bukombe alisema mauaji hayo yalitokea saa 2 usiku wakati mjamzito huyo akiwa nyumbani kwake na watoto wake wakati watu hao walipokua wakipita huku wakitafuta ng’ombe wao aliyepotea.
Alisema binti wa marehemu alisema hawajaona ng’ombe aliyepotea ndipo watu hao walipomba maji ya kunywa kwa madai wamechoka sana kutokana na kuwatafuta kwa muda mrefu na alipokwenda kufata maji ndipo walitumia muda huo kumuua mama yake.
“Walipogundua amepoteza maisha walikimbia kusikojulikana na wakati wanampiga aliwauliza kwa nini mnanipiga…?,kosa langu ni lipi kwanini mnaniua,lakini hauaji hao hawakutaka kumsikiliza…
MWANANCHI
Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mbeya imegundua viwanja na nyumba zaidi ya 10 za Serikali zikitumiwa na watu binafsi katika mazingira ya kutatanisha.
Nyumba zilizoubwa na utata huo zipo maeneo ya Uzunguni,Uhindini na Mwanjelwa moja ikiwa na vyumba vitano pamoja na maduka.
Pia imegundua mashamba yake yalilimwa mazao mbalimbali na watu binafsi katika maeneo ya Foresy ya zamani na mpya.
Katibu Tawala msaidizi Hamis Kaputa jana kuwa taarifa zaidi ya nyumba hizo zitatolewa na aliyekua Mwenyekiti wa tume ya uchunguzi ambaye kwa sasa yupo likizo.
Alisema taarifa ya tume ilishaandaliwa na kupelekwa kwa Waziri mkuu Pinda ambaye ndiye aliyetaka apatiwe matokeo ya kazi hiyo.
MWANANCHI
Mvua kubwa isiyotabirika inatarajiwa kunyesha sehemu mbalimbali nchini hasa ukanda wa Pwani ya Kaskazini maeneo ya jijini Dar es salam,Unguja na Pemba pia katika ukanda wa Kaskazini Mashariki kwa Mikoa ya Kilimanjaro,Arusha na Manyara.
Akitoa taarifa hiyo ya hali ya Hewa,Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA Agnes Kijazi alisema mvua ya msimu katika maeneo hayo inatarajiwa kuisha leo.
Hata hivyo alisema mvua kubwa ya nje ya msimu inatarajia kuanza kipindi cha Januari 2015 na itaikumba pia Mikoa ya Mwanza,Kagera,Shinyanga na Geita.
Alisema mvua hiyo inasababishwa na ongezeko la joto linalolifanya anga kushindwa kutengeneza unyevunyevu ambao hugeuka kuwa mvua.
“Ninawashauri wananchi kuchukua hatua za kujikinga na athari za kiafya na mazingira zinazoweza kusababishwa na ongezeko la joto linaloendelea sambamba na mvua kubwa kunyesha”alisema.
MTANZANIA
Aliyekua Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijukaamesema hayuko tayari kujiuzulu ujumbe wa kamati kuu ‘CC’ ya Chama cha Mapinduzi.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya Rais Kikwete kutangaza kumfuta kazi katika mkutano wake na wazee wa Dar es saalam uliofanyika Decemba22 mwaka huu.
Karibu msaidizi Kazi maalum wa Tibaijuka,Nassor Hussein alisema suala la Tibaijuka kujiuzulu nafasi yake ya Ujumbe wa CCM lipo chini ya viongozi wa Kitaifa wa Chama hicho ambao hao ndio watakaoamua.
“Tibaijuka hayupo tayari kujiuzulu kwa sasa ujumbe wa kamati kuu,anachosubiri ni uamuzi wa Chama,jambo hilibado lipo kwa wakubwa na ni siri kwa kuwa lipo kiutendaji,hivyo litaamuliwa na kamati kuu ya chama husika”alisema

No comments:

Post a Comment