Mchezaji wa Azam FC, Aggrey Morris alipiga kiwiko Emmanuel Okwikatika mechi iliyowakutanisha Simba vs Mtibwa, kitendo ambacho kilipelekea Okwi kuzimia uwanjani na kupelekwa hospitali, kitendo kingine kilikuwa kikimhusisha mchezaji wa Mbeya City Juma Nyosso ambaye alionekana akimshika makalio mchezaji wa Simba Elias Maguri.
Baada ya mjadala mkubwa kwenye magazeti na mitandaoni hatimaye leo hii Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
imewafungia kati ya mechi tatu na nane wachezaji Juma Nyoso wa Mbeya City na Aggrey Morris wa Azam kutokana na makosa ya kinidhamu waliyoyafanya wakiwa uwanjani.
Nyoso ambaye alilalamikiwa na TFF kwa kumfanyia vitendo vya udhalilishaji mshambuliaji Elias Maguri wa Simba amefungiwa mechi nane za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).
Akiwa mbele ya Kamati hiyo jana (Februari 5 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Nyoso alikiri kufanya na pia amemuomba radhi mchezaji Magurikwa kitendo hicho.
Akisoma uamuzi huo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Wakili Jerome Msemwa alisema kitendo kilichofanywa na Nyoso ni kosa kubwa la kudhalilisha utu wa mtu na ni mfano mbaya kwenye mchezo wa mpira wa miguu.
Naye Morris amefungiwa mechi tatu za VPL baada ya kutiwa hatiani kwa kumpiga mshambuliaji Emmanuel Okwi wakati timu hizo zilipopambana kwenye mechi ya ligi iliyochezwa Januari 25 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment