Friday, February 6, 2015

SEMINA YA UBORESHAJI YA DAFTARI LA WAPIGA KURA MKOANI LINDI

Wasimamizi wa uchaguzi manispaa ya Lindi wakiwa kwenye semina ya maboresho ya daftari la wapiga kura yaliyokuwa yanaendeshwa na tume ya uchaguz
Afisa tume ya uchaguzi akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa uchaguzi na mafisa uchaguzi wilaya za mkoa wa Lindi kuhusu marekebisho ya tafutari la wapigakura 
Wasimamizi wa uchaguzi manispaa ya Lindi wakiwa kwenye semina ya maboresho ya daftari la wapiga kura yaliyokuwa yanaendeshwa na tume ya uchaguz

Mwaandishi wetuLindi

Vyama siasa mkoani Lindi vimeshauriwa kuteuwa mawakala
wa adilifu na 
waaminifu katika uchaguzi mkuu ujao ili kuepusha malalamiko
na migogoro 
isiyo na tija.
Wito huo ulitolewa   na katibu tawala wa mkoa huo Abdallah
Chikota wakati 
anafungua mafunzo ya uboreshaji daftarila wapiga kura kwa
 wasimamizi na Maafisa wa uchaguzi mkoani humo. 
Chikota alisema baadhi ya malalamiko na migogoro
 inayotokea mara kwa mara
 baada ya chaguzi inatokana na vyama kuwateua na
 kuwapeleka watu wasio 
makini,waaadifu na waaminifu kwenye vituo vya kupigia na
 kuhesabia kura. 
Alisema hali hiyo inasababisha malalamiko na migogoro
ambayo kama 
mawakala watakuwa makini inaweza kuepukwa.Alibanisha
 kwamba baadhi ya
 mawakala wanasahu wajibu wao na kujipa majukumu ya siyo
 wahusu ikiwamo kutoa maelekezo kwa wasimamizi.
Kitendo ambacho hakikubaliki kwa mujibu wa kanuni,taratibu
 na sheria.
"wakala hapaswi nasiowajibu wake kutoa maelekezo kwa
msimamizi wa 
uchaguzi kwani kufanya hivyo nikuingilia majukumu na utendaji
 ma tume,
" alisema Chikota.
Aliongeza kusema mawakala ambao sio makini,waadili na
waaminifu mara 
nyingi hupeleka takwimu za uongo kwa vyama vyao kutokana
 na kushindwa 
kujua na kutekeleza majukumu yao.
Aidha katibu tawala huyo aliwataka wasimamizi hao kuepuka
 upendeleo kwa
 chama chochote cha siasi kwani wanaweza pia kuwa chanzo
 cha malalamiko 
na migogoro." ninyi mnatakiwa kutenda haki kwani kama
waamuzi wa mchezo,
sasa kama mwamuzi anaipendelea timu mojawapo kwenye
mchezo nilazima 
yataibuka malalamiko na fujo ikitokea hivyo ni mwamuzi
 atakuwa
 amesababisha," aliongeza kusema Chikota.

ADVERTISEMENT

0 COMMENTS:

Post a Comment


:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-#=p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer 
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

No comments:

Post a Comment