Leo katika kikao cha Bunge Dodoma, kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu moja ya swali ambalo liliulizwa ni ishu ya chama cha CCM kuwatumia wanafunzi katika sherehe za chama hicho zilizofanyika Songea mwisho wa wiki iliyopita.
“Tumeambiwa kwamba tustumie wanafunzi kushiriki katika masuala ya kisiasa hasa katika vyuo na mashule. Hivi karibuni mkuu wa Mkoa wa Ruvuma pamoja na viongozi wa Ruvuma wamewatumia wanafunzi wa Manispaa ya Songea kushiriki katika maamuzi ya miaka 38 ya Chama cha Mapinduzi… Kwa nini msitumie wanachama wenu kwenye sherehe hizo mnaenda kutumia wanafunzi”— Susan Lyimo.
“Unajua mtoto wa nyoka ni nyoka, chama kina mfumo wake ambao umeshuka mpaka kwenye ngazi ya kitu kinaitwa chipukizi, ni watoto ambao wamezaliwa kutokana na wazazi wana CCM ndio maana chama kiliwatumia. Wao walichokuwa wanafurahia pale ni ile parade na kuonekana wamepiga sare ile basi…”—Waziri Mkuu Pinda.
“Nimesikitishwa sana na ajibu ya Waziri Mkuu. Pamoja na watoto hao kuwa wadogo lakini utatambua kwamba baadhi ya watoto hawa vilevile wazazi wao ni wanachama wa vyama vya upinzani, sikubaliani na wewe kwamba watoto hawa wazazi wao ni wa chama cha mapinduzi…” MbungeSusan Lyimo.
“Na mimi naheshimu sana maelezo ya mama Susan… Kiachieni chama na utaratibu wake waendelee nao mimi sioni kama kuna tatizo…”—Waziri Mkuu Pinda.
“Waziri Mkuu amehararisha jambo ambalo nikinyume na haki za binadamu… kuwalazimisha watu kwenda kwenye shughuli, tuna barua ambayo Mkuu wa Mkoa alimwandikia Afisa Elimu kuwalazimisha vijana wa Songea Boys na Songea Girls wavae sare za CCM na walimu waende kule kwa lazima … Mwongozo wangu ni kwamba Waziri Mkuu afute kauli hapa”—Felix Mkosamali.
“Wale watoto waliambiwa waombe wenyewe, jioni saa kumi baada ya masomo yao nd’o walifanya gwaride lile sio wakati wa kazi n ahata sherehe yenyewe imefanyika siku ya jumapili ambayo sio siku ya kazi…”
No comments:
Post a Comment