Alhamisi ya February 05, nimekuwekea Hekaheka ya leo inatokea Dodoma inahusu baba alijifungia ndani akimpiga mtoto wake wa miezi 8, mke wake alipomtaka afungue mlango alitishia kumuua.
Mama wa mtoto huyo alipoona hali hiyo alikimbilia kituo cha Polisi ili kupata msaada, askari aliyefika aliingia ndani ya chumba hicho kwa ili amuokoe mtoto huyo, baba huyo alimkata kwa mapanga hadi kufariki.
Shuhuda wa tukio hilo amesema kuwa Polisi huyo alifanikiwa kuingia kwenye chumba hicho na kumuokoa mtoto huyo lakini wakati anatoka nje aliteleza na kuanguka ndipo baba huyo alipopata nafasi ya kumshambulia kwa panga hadi kufariki.
Baada ya kusababisha mauaji hayo mtuhumiwa alikimbia, Jeshi la Polisi wanamtafuta na taarifa kuhusu hali ya mtoto huyo ni kwamba anaendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment