Friday, February 6, 2015

Mgogoro wa Ukraine

Waasi wa Ukraine
Nchi za magharibi zimependekeza mipango mipya kumaliza mgogoro kati ya serikali ya Ukraine na waasi wanaoungwa mkono na Urusi.
Rais wa Ukraine Petro Poroshenko amesema mapendekezo mapya yaliyotolewa na kiongozi wa Ujerumani Kansela Angela Merkel, na rais wa Ufaransa Bwana Francois Hollande, yameongeza matumaini ya kumaliza mapigano.
Mpango huo utawasilishwa kwa Urusi Ijumaa, ambako Urusi imeahidi mazungumzo yenye manufaa. Lakini hatua ya Urusi kuwaunga mkono waasi wa Ukraine imeshutumiwa na Marekani.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry, ambaye anazuru Ukraine ameitaka Urusi kuwaondoa wapiganaji wake na zana za kivita kutoka Ukraine na kuiruhusu Ukraine kulinda mipaka yake.
Seneta wa chama cha Republican kutoka jimbo la Ohio, Rob Portman, amesema Ukraine inataka msaada zaidi kutoka nchi za magharibi ili kujilinda dhidi ya mashambulio ya waasi:

No comments:

Post a Comment