Wednesday, January 7, 2015

8 HOI KUNYWA MAZIWA YENYE SUMU

WATU wanane wa familia tatu tofauti, wakiwemo wanafunzi wa shule ya msingi, wamelazwa katika Hospitali ya Misheni ya Malkia wa Ulimwengu Puma wilayani Ikungi mkoani hapa baada ya kunywa maziwa yanayodhaniwa kuwa na sumu.
Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Teule, Dk Corbinian Nyenyembe alisema wagonjwa hao wanaotoka kijiji cha Nkuhi wilayani humo.(MM)
Dk Nyenyembe alisema wagonjwa hao wanatoka familia tatu tofauti, ambapo kati yao wamo wanafunzi watatu wa shule ya msingi Mayuta wilayani Ikungi.
Alitaja wagonjwa hao kuwa ni Eliua Yeremiah (14), Nicodemus Yeremiah (11), Shukuru Yeremiah (09), Muntimbo Martin (22), Winfrida Boniface (22), Josephine Martin (20), Richard Njiku (22) na Naomi Njiku (20).
Akisimulia kisa hicho, mzazi wa wanafunzi waliolazwa, Jeremiah Alute alisema siku ya tukio, mmoja wa watoto wake alikwenda kununua maziwa nyumbani kwa Muntimbo (ambaye naye amelazwa pamoja na mkewe) na walipokunywa, walianza kuhara na kutapika ovyo

No comments:

Post a Comment