Bunge jipya la Marekani linakutana Jumanne huku wa-Republican wakidhibiti mabaraza yote mawili, la wawakilishi na senate, na wa-conservative wakiwa na azma ya kubadilisha baadhi ya sera za Rais Barack Obama.
Kiongozi ajaye wa walio wengi katika baraza la seneti, Mitch McConnell alizungumza na kituo cha televisheni cha CNN nchini Marekani, Jumapili alisema kwa sababu wamarekani walipiga kura kwa serikali iliyogawanyika, bunge linalodhibitiwa na Republican na Rais mdemocratic, haimaanishi kuwepo na mvutano.
McConnell alisema wapiga kura wanataka muafaka na maendeleo kwenye masuala muhimu. Kiongozi huyo wa Republican anasema kazi kubwa ya kwanza kwa baraza la seneti itakuwa kuidhinisha bomba la mafuta la Keystone. Wafuasi wanasema litabuni nafasi zaidi za ajira na uhuru wa nishati kwa Marekani.
Wapinzani wa Democrat wanaita hili ni janga la kimazingira linasubiri kutokea na licha ya yote hayo lakini nafasi chache za ajira zitakuwa za muda. Wa-Republican katika mabaraza yote pia wataangalia kutengua sahihi ya Rais Barack Obama ya mageuzi ya huduma za afya na kuzuia amri yake ya kiutendaji kwenye suala la uhamiaji.
Rais Barack Obama
Bwana Obama alisema atatumia kura ya turufu kwenye miswaada ya Republican asiyofurahishwa nayo. Hata kama wapo wengi kwenye mabaraza yote wa-Republican huwenda wasiwe na kura za kutosha kubadili matokeo ya kura ya turufu itakayotumiwa.(MM)
No comments:
Post a Comment