Simanzi kubwa imeikumba familia ya waziri mkuu wa zamani wa Kenya Raila Amolo Odinga baada ya kutoka kwa taarifa ya kifo cha mtoto mkubwa wa mwanasiasa huyo mashuhuri nchini Kenya asubuhi ya leo .
Mtoto huyo anayefahamika kwa jina la Fidel Odinga alikutwa akiwa amefariki dunia kitandani kwake asubuhi ya leo (jumapili) baada ya kurudi nyumbani kwake alfajiri akiwa anatoka kukutana na rafiki zake .
Mara ya mwisho Fidel aliripotiwa kukutana na baba yake usiku wa jumamosi kabla ya kuagana na kwenda kukutana na rafiki zake katika sehemu ambayo haijawekwa wazi na baada ya hapo alirudi nyumbani kupumzika hadi mauti yalipomkumba .
Hadi mauti yanamkumba Fidel Odinga alikuwa na umri wa miaka 42 na Polisi nchini Kenya wameanza uchunguzi wa kifo cha mtoto huyo wa mwanasiasa maarufu nchini Kenya huku bado kukiwa hakuna taarifa zozote kuhusiana na chanzo cha kifo chake .
Fidel ameacha mke mmoja na mtoto mmoja mwenye umri wa miaka miwili ambaye alizaa na mke wake Getachew Bekele ambaye ni raia wa Eritrea .
Saa chache baada ya habari za kifo cha Fidel makundi tofauti ya watu yalianza kufanya maandamano na vurugu maeneo ya Ngong nje kidogo ya Jiji la Nairobi wakipiga kelele za ‘Nani amemuua Fidel’ wakimaanisha kuwa kifo chake kimesababishwa na mtu huku wakishindwa kutaja sababu au chanzo kamili .
No comments:
Post a Comment