Thursday, January 8, 2015

Bill Gates anywa maji ya kinyesi

Bill Gates anywa maji yaliotengezwa kutokana na kinyesi
Mmiliki wa kampuni ya Microsoft Bill Gates amekunywa maji yaliotengenezwa kutokana na kinyesi cha binaadamu kama maonyesho ya teknolojia mpya itakayoweza kutoa maji safi katika mataifa yanayoendelea.Mwanzilishi huyo wa Microsoft amesema kuwa ataisambaza mitambo ya teknolojia hiyo mpya kote duniani baada ya kuifanyia majaribio mwishoni mwa mwaka huu.Teknolojia hiyo imeungwa mkono na shirika la WaterAid ambalo limesema kuwa itasaidia sana katika maeneo ya miji.Kulingana na shirika hilo la hisani takriban watu millioni 748 hawana maji safi ya kunywa.katika kanda ya video iliyowekwa katika blogu yake,Bwana Bill Gates alishuhudia kinyesi cha Binaadamu kikiingizwa katika mtambo huo kabla ya kunywa maji yaliokuwa yakitoka kutoka kwa kikombe.''Maji hayo ni mazuri sana ikilinganishwa na maji yoyote yale niliokunywa,na baada ya kusomea teknolojia hii nitayanywa kila siku.Maji haya ni salama kabisa'',aliandika katika blogu yake.Kulingana na mtengenezaji wa mtambo huo Peter Janicki,maji taka hayo huchemshwa kabla ya mvuke wa maji hayo kutengwa na taka ngumu.Taka hizo ngumu baadaye huwekwa katika moto na kutoa mvuke unaoendesha mashine zinazotoa nguvu za umeme kwa mtambo huo na pia kwa wakazi wa eneo hilo.Maji hayo baadaye hutiwa ndani ya mtambo wa kusafisha maji ili kutoa maji safi ya kunywa.''lakini kwa nini mtu awe na wazo la kubadilisha uchafu kuwa maji ya kunywa na umeme'',aliuliza Gates.Jibu aliloandika ni kwamba kwa sababu magonjwa yanayosababishwa na mazingira machafu huwaua watoto 700,000 kila mwaka na huwakinga wengine wengi dhidi ya kuathirika kiakili na kimwili.

No comments:

Post a Comment