Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania IPTL chini ya uongozi wa kampuni ya Pan African Power PAP imetangaza kushusha bei ya umeme kwa asilimia 20 baada ya kufanya marekebisho makubwa ya mitambo yake mwaka jana.
Mbali na hilo pia imetangaza kuw abei ya umeme inatarajiwa kushuka kulingana na kushuka kwa bei ya mafuta mazito.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPTL/PAP Harbinder Seth alisema bei ya umeme iliyotangazwa na kampuni yake kwa Tanesco itakua chini ya bei ya awali iliyokokotolewa ya senti 23 dola za Marekani kwa kilowati pamoja na kupatikana umeme wa uhakika.
“Tukiwa tunaukaribisha mwaka 2015 IPTL inajivunia kutangaza kuwa imefanikiwa kufanya marekebisho makubwa ya mashine zake ya saa 36,000 ya kufanya kazi,zoezi lililokamilika mwaka jana.
Alisema sehemu ya ahadi ya PAP kwa APTL inaendeshwa vizuri kwa ufanisi ambapo wakati umefika sasa kwa Tanesco kuwa na uhakika wa kupata umeme wa megawati 100 katika gridi ya Taifa wakati wote utakapohitajika.
MTANZANIA
Makada wa CCM Bernad Membe na January Makamba ambao wametangaza nia ya kuwania kiti cha Urais mwaka huu,wameanza kuonyesha hofu kuhusu nafasi hiyo ya juu ya nchi.
Membe ambaye ni Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa na Makamba ambaye ni Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia wamepatwa na wasiwasi kutokana na uwepo wa taarifa za matumizi makubwa ya fedha katika kusaka nafasi hiyo.
Membe alisema Taifa linakabiliwa na mambo makubwa mawili hatari ambayo ni rushwa na mmomonyoko wa kimaadili.
Alisema wapo watu wenye fedha nyingi na uwezo wa kununua mtu yoyote ili kufanikisha mipango yao ya kuingia madarakani jambo ambalo halikubaliki.
Kwa upande wa Makamba amewataka Watanzania kuepuka watu wanaotumia fedha nyingi kutafuta uongozi kutokana na kile alichosema,wakifanikiwa kupata uongozi hawatatawala kwa haki.
Alisema Taifa likipata kiongozi wa aina hiyo hataweza kuhukumu kwa haki na pia anaweza kuigawa nchi na watu wake.
HABARILEO
Familia zinazotumia maziwa ya kopo aina ya Lactogen,ambayo yamesajili hapa nchini kwa ajili ya kutumiwa na watoto wachanga,zina hali ngumu baada ya kuadimika,huku ikielezwa kuwa yatazidi kuadimika kwa zaidi ya miezi miwili ijayo.
Uchunguzi umebaini kuadimika kwa maziwa hayo yanayotengenezwa nchini Ufaransa kunafanya baadhi ya familia kununua kwa bei kubwa na wengine kulazimika kubadili aina ya maziwa kwa watoto wao.
Mmoja wa wauzaji wa maziwa hayo kwa rejareja alisema tatizo hilo lilianza kujitokeza mwanzoni mwa mwezi Disemba mwaka jana na kufanya bei yake kupanda kutoka 15,000kwa kopo hadi 20,000.
Kwa upande wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kupitia Ofisa habari wake Gaudensia Simwanza mamlaka yake inasimamia ubora wa bidhaa za maziwa ya watoto na wamekua wakiendesha operesheni ya kuondoa bidhaa hizo feki.
HABARILEO
Ukatili wa kijinsia unaendelea kutikisa Mkoa wa Mara ambapo mwanamke mmoja Rhobi Mwita amelazwa katika hospitali teule ya Mkoa ya Bunda baada ya kupigwa na kujeruhiwa vibaya kwa kuingizwa chuma sehemu za siri na mume wake Mwita Chacha kutokana na wivu wa mapenzi.
Akisimulia mkasa huo akiwa hospitalini,mwanamke huyo alisema siku hiyo mumewe ambaye alikua amelala kwa mke mkubwa alifika nyumbani na kumkuta akiwa anakamua ng’ombe maziwa.
“Baada ya kufika nyumbani alimuuliza binti yetu niko wapi,alipoambiwa ninakamua ng’ombe alinifuata na kuanza kunigombeza kuwa usiku wa siku hiyo niliingiza mwanaume na kufanya nae tendo la ndoa,nilijitetea sijafanya hivyo lakini akaanza kunishambilia kwa kipigo na kuninyonga shigo kwa kutumia kitenge hadi nikaanguka na kupoteza fahamu”alisema mwanamke huyo.
“Nilipozinduka nikajikuta mimi na binti yetu wa miaka 13 tumefungwa mikono huku nikiwa na chuma aina ya nondo sehemu za siri,baadaye akatufungulia na kuanza kutupiga tena kabla ya kutokomea.
Muuguzi wa zamu katika hospitali hiyo Ester Maduhu alisema mwanamke huyo alipokelewa akiwa na hali mbaya na kwamba kwa sasa hali yake inaendelea vizuri.
MWANANCHI
Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia chama cha NCCR-Mageuzi David Kafulila amesema kama upinzani utashindwa kuchukua nchi mwaka huu,basi CCM itaendelea milele kuongoza Tanzania.
Oktoba mwaka huu Tanzania inaingia kwenye kinyang’anyiro cha cha uchaguzi wa Rais,wabunge na madiwani baada ya Rais Kikwete kumaliza muda wake.
Kafulila alisema Watanzania watendelea kubaki maskini huku keki ya Taifa ikiliwa na vigogo wachache.
“Huu ni wakati wa kuajingalia…watu wanalalamika kila siku,hali ya umaskini inaongezeka na kila kukicha ni kilio,sasa ni wakati wa kufanya uamuzi”alisema Kafulila.
Alisema umaskini wa Mtanzania unachangiwa kwa kiasi kikubwa na wezi wa rasilimali za nchi,huku Watanzania walio wengi wakitaabika.
“Mimi nasema upinzani ukiingia Ikulu haya yote yatamalizika,kila Mtanzania atafurahi rasilimali zake,lakini waking’ang’ania CCM watabakia hivyo”alisema.
Alisema ikiwa watashindwa kuitoa CCM na ikafanya vizuri katika kila eneo,Watanzania hasa wapinzani watabaki kwenye uongozi wa mitaa,vijiji na vitongoji walivyopata katika uchaguzi uliopita kwa miaka mitano mingine.
MWANANCHI
Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein amesema mpango wa ujenzi wa uwanja wa ndege kisiwani Pemba,ikiwemo uwekaji wa taa unatarajia kuanza utekelezaji wake mwaka huu.
Shein alitangaza mpango huo wakati akizindua maegesho na njia ya kupita ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Karume Mkoa wa Mjini Magharibi ikiwa ni maazimisho ya 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Alisema tayari Serikali imepanga kujenga kiwanja hicho mwaka huu ni pamoja na kukiweka taa ili ndege zitoe huduma saa 24.
Alisema tayari washirika wa maendeleo wameshajitokeza kutoka Uturuki ili kusaidia ujenzi huo.
MWANANCHI
Licha ya kushuka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola ya Marekani,benki kuu ya TanzaniaBoT imepata faida ya zaidi ya bilioni37 kwa mwaka 2013/14.
Ripoti yake ya mwaka iliyotolewa mwishoni mwa mwaka jana inaonyesha kulikua na faida ya takribani bilioni 195 ikilinganishwa na ile ya msimu uliopita huku hukiwa na ufanisi katika kipengele cha biashara ya fedha za kigeni.
“Katika faida hiyo kuna 37.22 bilioni ambazo zinatokana na faida ya sarafu ya nje zilizopo,hii ni tofauti na mwaka jana kwani kulikua na hasara ya bilioni41.89″inasema ripoti hiyo.
Wakati BoT ikipata faida sekta nyingine za uchumi zinaendelea kuathirika na kuongeza gharama za maisha kwa wananchi mfano nishati ya mafuta ambayo bei yake katika soko la dunia imeshuka ilhali hapa nchini hali ikiendelea kutoonyesha matumaini.
No comments:
Post a Comment