Mwaandishi wetu Liwale…. Wananchi wa kata ya Kipule kijiji cha Makinda wilaya Liwale mkoani Lindi wamemtimua mbunge wa viti maalum,zainabu Kawawa kwa madai kufanya mkutano wa kutangaza nia ya kuomba ubunge katika jimbo hilo kabla ya muda wa kufanya hivyo haujafika. Tukio hilo limetokea juzi(alhamisi) majira ya saa nane mchana baada ya mbunge huyo kufika kijijini hapo kwa lengo la kukutana na mwenyekiti wa kijiji Salum Kachwele ili kumtaka aitishe mkutano wa wajumbe wa serikali ya kijiji na baadhi ya wananchi hasa wazee maarufu ikiwa ni kuwashaawishi ili wamwuunge mkono katika harakati zake za kuwania ubunge wa jimbo hilo. Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Salum Kachwele alisema mbunge huyo alifika kijiji hapo akiwa na mpambe wake Mkopora Mkopara na kumuomba awaite wajumbe wa serikali ya kijiji pamoja na wazee maarufu ili azungumze nao jambo ambalo alidai hakulikubali kwani kabla ya harakati hizo za ubunge Kawawa hajawahi kufanya kikao chochote wala kutembelea katika kijiji hicho. Kachwela alisema kabla zoezi la kukutana na wanachi hao halijafanikiwa lilikuja kundi kubwa la wananchi likiongozwa na vijana wakizomea wakiwa na mawe na magongo waliotokea kwenye mkutano wa chama cha wananchi cuf waliokuwa kwenye mkutano wakuwashukuru wananchi kwa kukichangua cha hicho kwenye uchagunzi wa serikali uliopita na kumtaka mbunge huyo kuondoka katika eneo mara moja. Kwa upande wake mbunge Zainabu kawawa alikiri kutembelea kijiji hapo ila alikataa kufanya kikao na wananchi hao na kutokea tukio la kufukuzwa na kueleza kuwa yeye alikwenda kufanya ziara ya kikazi ya kuwatembelea wapiga kura kuhamasisha maendeleo. ‘Ndugu yangu hayo maneno sio kweli mimi nilikwenda kijiji hapo kufanya kazi za kibunge sio kufanya kampeni kama ilivyoelezwa na hao watu wasionitakia mema’ukweli ni kwamba mti wenye matunda matamu ndiyo unapigwa mawe alisema Kawawa.SAUTI YA KUSINI
karibuni sana wasomaji wa blog hii usikubali kupitwa na habari tanzania na hata nje ya tanzania.
Saturday, January 10, 2015
zainabu Kawawa apigwa mawe

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment