Mhashamu Baba Askofu Dr.Valentine Mokiwa, Askofu wa Dayosisi ya
Dar es Salaam;
Kasisi Mkuu Kiongozi Canon John Mlekano;
Katibu Mkuu wa Dayosisi ya Dar es salaam- Canon John Senyagwa,
Wakuu wa Majimbo mliopo hapa,
Ndugu waumini;
Wageni waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Bwana Asifiwe....!
Shukrani kwa Mwaliko
Nakushukuru sana Baba Askofu Mokiwa, viongozi wenzako pamoja
na waumini wote wa Dayosisi ya Dar es Salaam kwa kunialika kuja
kushiriki nanyi katika maadhimisho haya ya kihistoria ya Jubilei ya Miaka
Hamsini ya Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar Es Salaam.
Nawapongeza sana waumini wa Dayosisi ya Dar es Salaam kwa ku-
timiza nusu karne tangu ianzishwe. Miaka hamsini si haba, ni umri wa
timiza nusu karne tangu ianzishwe. Miaka hamsini si haba, ni umri wa
makamo, na kwa kipimo chochote kile ni umri mrefu. Umri huu ni kipimo
cha ukomavu wa Dayosisi ya Dar es Salaam. Ni miaka 50 ya uinjilisti, up-
onyaji na huduma kwa jamii. Mafanikio haya ya Dayosisi ni kielelezo cha
onyaji na huduma kwa jamii. Mafanikio haya ya Dayosisi ni kielelezo cha
uimara wa Kanisa la Anglikana. Hatuna shaka kuwa mmeweza kudumu
kwa muda huo kutokana na misingi imara ya kiroho na uongozi uliojeng-
wa juu ya miamba iliyowatangulia. Hatuwezi kuzungumzia mafanikio ya
wa juu ya miamba iliyowatangulia. Hatuwezi kuzungumzia mafanikio ya
Dayosisi hii bila kumtaja Baba Askofu John Sepeku na wenzake waliolijen-
ga Kanisa hili.
ga Kanisa hili.
Kanisa la Kianglikana la Tanzania ni miongoni mwa majimbo mawili
tu ya kianglikana duniani kuwa na muungano wa mapokeo mawili ya
kanisa Anglikana - yaani High Church (lililokuwa na mrengo wa kikatoli-
ki) na Low Church (lililokuwa na mrengo wa kiinjili). Kanisa la Kiang-
likana la Tanzania na lile la Burma pekee ndio yaliyoweza kuunganisha
ki) na Low Church (lililokuwa na mrengo wa kiinjili). Kanisa la Kiang-
likana la Tanzania na lile la Burma pekee ndio yaliyoweza kuunganisha
mapokeo haya mawili na hatimaye kuwa na kitabu cha sala kimoja, litru-
gia moja, na uongozi mmoja wa Askofu Mkuu ambao unasomwa katika
gia moja, na uongozi mmoja wa Askofu Mkuu ambao unasomwa katika
parokia zote. Ndio maana haishangazi kuwa kanisa Anglikana la Tanzania
lilisimama imara bila hofu kupinga ndoa za jinsia moja hata pale makanisa
mengine ya Anglikana duniani yalipoamua kufanya hivyo. Mlinipa faraja
kubwa, maana kupitia kwenu ile sauti ya Serikali, na sauti ya watanzania
kukataa shinikizo kutoka nje ya nchi la kukubali ndoa za jinsia moja lilipa-
ta nguvu na mwangwi mkubwa. Mlinitia nguvu sana pale niliposimama
ta nguvu na mwangwi mkubwa. Mlinitia nguvu sana pale niliposimama
kidete kuwaambia rafiki zetu wa nje kuwa katika hilo la ndoa za jinsia
moja, Tanzania tunaomba tukubaliane kutokukubaliana.
Tunapojitokeza kwa kutimiza miaka 50 ya Dayosisi ya Dar es
Salaam , hatuna budi kukumbushana kuwa safari bado ni ndefu. Tulipoto-
ka kweli ni mbali, tunapokwenda ni mbali zaidi. Ipo zaidi ya miaka 50
ka kweli ni mbali, tunapokwenda ni mbali zaidi. Ipo zaidi ya miaka 50
mingine mbele ya Kanisa hili. Hivyo leo tunaianza safari mpya, katika
mwaka mpya na matumaini mapya. Sisi katika Serikali tunayo matumaini
makubwa na safari yenu. Katika miaka 50 ya uhai wa Dayosisi,
Tumeshuhudia kazi zenu na huduma zenu. Siku zote mmeshirikiana na
Serikali katika kutoa huduma za jamii na kuilea amani yetu.
Napenda kuwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na
Kanisa la Anglikana pamoja na madhehebu mengine ya dini kuboresha
maisha ya Watanzania. Tutaendelea kupokea ushauri wenu na kuwashirik-
isha katika mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya nchi yetu na
isha katika mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya nchi yetu na
watu wake. Naomba muendelee kushirikiana na Serikali katika kutoa
huduma kwa wananchi. Muendelee kutumia mtandao wenu mpana uliopo
nchi nzima kwa ustawi na maendeleo ya nchi yetu. Lengo letu libaki kuwa
moja daima na milele.
Maombi kwa Viongozi wa Dini
Mhashamu Baba Askofu Dr. Mokiwa,
viongozi wa dini mliopo;
Mabibi na Mabwana;
Mwaka huu wa 2015 ni mwaka wa kipekee sio tu kwa Kanisa lenu
linaloadhimisha miaka 50 ya Dayosisi ya Dar es Salaam, bali pia kwa
watanzania wote. Mwaka huu una mambo makubwa mawili yaliyo mbele
yetu yaani kura ya maoni ya Katiba Inayopendekezwa na uchaguzi mkuu
wa Rais, Wabunge na Madiwani. Kama ilivyo kwa Dayosisi yenu, Taifa
letu nalo linaianza safari ya miaka 50 ijayo na kufika kwetu huko ku-
tategemea na jinsi tunavyoianza safari yenyewe.
tategemea na jinsi tunavyoianza safari yenyewe.
Nchi yetu inapita katika kipindi cha majaribu makubwa na mitihani
mikubwa. Tunalo tatizo la mmomonyoko wa maadili katika ngazi zote
kuanzia familia, shule, ofisi na serikalini. Tunalo tatizo la ufisadi, ukatili
dhidi ya vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi, na tunalo pia tatizo
la umasikini. Tunalo tatizo la kupoteza uvumilivu wa kidini na kisiasa.
Watanzania wengi wamefika mahala wanaanza kukata tamaa na kupoteza
matumaini. Changamoto hizi zinawasumbua pia viongozi wa dini zetu
zote. Waumini wamekata tamaa na kupoteza hofu ya Mungu. Kumekuwe-
po na wengi sasa wanaokimbilia kwenye nguvu za giza, uganga na una-
jimu. Tunahitaji kutoka hapa. Tunajiuliza wote, tunatokaje?
po na wengi sasa wanaokimbilia kwenye nguvu za giza, uganga na una-
jimu. Tunahitaji kutoka hapa. Tunajiuliza wote, tunatokaje?
Baba Askofu Dr. Mokiwa;
Ndugu zangu;
Habari njema ni kuwa, nyakati za majaribu hazidumu. Mashaka na
majaribu humfika mwanadamu ili kumuimarisha kila anapoukaribia
mwisho mwema. Majaribu ni kipimo cha imani. Tunaletewa majaribu ili
tuyashinde sio tuyakimbie. Tunayo fursa muhimu mbele yetu, kura ya
maoni ya Katiba Inayopendekezwa na muhimu zaidi Uchaguzi Mkuu wa
Oktoba 2015. Sote tumefuatilia kwa makini mchakato wa Katiba na
tumeshiriki kwa hatua mbalimbali. Tumebakiza hatua moja muhimu, nayo
ni kupiga kura ya maoni tarehe 31 Aprili, 2015. Sote tujiandae kuipigia
kura na sote tutoke tukafanye uamuzi sahihi.
Fursa nyingine muhimu ni uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015. Uch-
aguzi wa mwaka huu ni muhimu sana kwani tunachagua Rais mpya
aguzi wa mwaka huu ni muhimu sana kwani tunachagua Rais mpya
atakayeunda Serikali mpya ya awamu ya tano. Rais wa awamu ya tano
atategemewa kuendeleza mema ya awamu ya nne na awamu zilizopita, na
kutoa majawabu kwa changamoto za sasa na zijazo na kutusogeza karibu
zaidi na Tanzania njema tunayoitamani, Tanzania yenye neema tele.
Hatuko mbali na nchi yetu hiyo ya ahadi. Serikali ya awamu ya nne ime-
fanya mengi sana makubwa ya kujenga misingi ya kutufikisha huko.
Tumepanua nafasi za elimu, afya na huduma za jamii, tumejenga miun-
dombinu ya kutuwezesha kufika huko, uchumi umekuwa sana lakini
dombinu ya kutuwezesha kufika huko, uchumi umekuwa sana lakini
umasikini haujapungua kulingana na kasi ya kukua kwa uchumi. Bahati
nzuri tunazo rasilimali zinazoweza kutuvusha katika hatua hii ya mwisho
kuifikia neema mbele yetu.
Wengine wetu tumejiuliza sana, nini basi kinasimama kati yetu na
neema iliyo mbele yetu ikiwa uchumi unakua na tumewekeza katika mi-
undombinu muhimu na rasilimali tunazo? Yako majawabu mengi tofauti.
undombinu muhimu na rasilimali tunazo? Yako majawabu mengi tofauti.
Jawabu moja ambalo linasemwa na kukubalika na wengi ni kuwa,kina-
chosimama mbele yetu, na kati ya umasikini wetu na neema iliyo mbele
chosimama mbele yetu, na kati ya umasikini wetu na neema iliyo mbele
yetu ni rushwa na ufisadi. Wako wanaotoboa mtumbwi wetu tunaosafiria
pamoja na jitihada zetu za kupiga makasia.
Mimi sipendi rushwa na ufisadi. Nashukuru Mungu kuwa rushwa,
ufisadi na mafisadi hawanipendi zaidi. Siwaonei wivu wale wanaopend-
waa mafisadi, natosheka kupendwa na wale wenye mapenzi mema na taifa
waa mafisadi, natosheka kupendwa na wale wenye mapenzi mema na taifa
letu. Jukumu la kuzuia ufisadi ni la kila mmoja wetu katika kila eneo lake
na kwa nafasi yake. Sio jukumu la viongozi pekee, au chama fulani pekee,
maana mafisadi wako kote katika ngazi zote. Naamini, mwaka huu, wengi
wetu tukisema hivyo, tukasimama katika mstari huo, na tukaenenda
hivyo, ufisadi hauwezi kutushinda. Kila mmoja na asipuuze udogo wa
sauti yake,au uchache wetu dhidi ya wale waovu, maana hata mwale
mdogo wa mshumaa hufukuza giza.
Baba Askofu,
Kwa kuwa uchaguzi kwa nchi yeyote ile ni jambo kubwa, naomba
Kanisa na waumini kwa ujumla waliombee taifa letu ili Mwenyezi Mungu
atuongoze kuchagua viongozi wenye uwezo, busara na hekima ya kutatua
changamoto zinazolikabili taifa. Tuchague viongozi waadilifu, wazalendo,
wachapa kazi, wasio na uchu wa madaraka kwa ajili ya kujinufaisha wao
binafsi na marafiki zao.
Ninawasihi viongozi wa dini muongeze juhudi za kuhubiri umoja
na kutoa mafundisho ya kuhimiza udugu na mshikamano miongoni mwa
waumini na watanzania kwa ujumla. Watu wapendane na washirikiane
bila kujali itikadi za vyama vyao au ushabiki walionao kwa wagombea.
Tukumbushane kuwa chaguzi zinakuja na kuondoka lakini amani
yetu, usalama wetu, udugu wetu na umoja wetu ndio nguzo kuu za uwepo
wa taifa letu. Tusikubali kupoteza kwa gharama yeyote tunu hii ya amani,
mshikamano na umoja wetu. Amani ya nchi yetu ikitoweka, umoja na
mshikamano wetu ukivunjika, hakuna atakayesalimika itaathiri wote
waliokuwamo na wasiokuwamo. Hivyo tunao wajibu wa kuidumisha
amani. Nasema hivyo kwa sababu nimeyaona mwenyewe kwa majirani
zetu.
Mhashamu Baba Askofu;
Ombi langu lingine kwenu - tuendelee kusaidiana kuilea nchi yetu
kiroho na kimaadili. Sisi tutaendelea kuhangaika na afya za miili na akili za
watu wetu. Tutaendelea kuwekeza katika afya,elimu na huduma za jamii.
Jitihada hizi za serikali ni kazi bure ikiwa dini zetu zote nchini haz-
itawekeza kwenye afya ya mioyo ya watu wetu. Maana binadamu hakami-
liki bila afya ya roho.
itawekeza kwenye afya ya mioyo ya watu wetu. Maana binadamu hakami-
liki bila afya ya roho.
Mimi naamini kwa dhati kuwa watu wakishika mafundisho ya
dini, wakamuogopa Mwenyezi Mungu, maovu mengi yatapungua.
Hayawezi kuisha kabisa lakini yatapungua sana. Ninyi viongozi wa dini
mnayo nafasi ya pekee kwa vile mnasikilizwa sana na waumini wenu. Ma-
neno yenu yanapokelewa vizuri kuliko wanasiasa au watu wengine.
neno yenu yanapokelewa vizuri kuliko wanasiasa au watu wengine.
Hivyo, tusaidiane kulea taifa letu ili lisiangamie. Hebu kila mmoja alime
mrsba wake. Najua ni kazi ngumu hususan katika kipindi hiki cha utan-
dawazi lakini tusichoke. Tuweke mkazo zaidi kwa vijana kwa sababu wao
dawazi lakini tusichoke. Tuweke mkazo zaidi kwa vijana kwa sababu wao
ndio wahanga wakubwa lakini pia wao ndio taifa la leo na kesho, ndio
warithi wa taifa letu. Tukiwaandaa vyema, mustakabali wa taifa letu na
watu wake utakuwa kwenye mikono salama. Tukishindwa leo, tutalia na
kusaga meno kesho. Taifa letu litakuwa mashakani.
Mwisho
Mhashamu Baba Askofu Dr. Mokiwa ;
Viongozi wa Kanisa la Anglikana ;
Ndugu waumini ;
Mabibi na Mabwana ;
Nimesema mengi, lakini nilidhani ni vizuri nikayaeleza hayo niliy-
oyaeleza kutokana na mazingira na nyakati zenyewe wakati tukishere-
hekea miaka 50 ya kanisa hili na tukizitazama nyakati muhimu kwa kanisa
oyaeleza kutokana na mazingira na nyakati zenyewe wakati tukishere-
hekea miaka 50 ya kanisa hili na tukizitazama nyakati muhimu kwa kanisa
na taifa zilizo mbele yetu. Nakushukuru kwa mara nyingine tena
Mhashamu Baba Askofu kwa uongozi wenu imara ambao umeliwezesha
kanisa katika kupata mafanikio makubwa sana katika miaka 50. Naomba
Mwenyezi Mungu awaongezee neema na karama ili kupata mafanikio zai-
di siku za usoni . Mimi nitakuwa nanyi bega kwa bega katika safari ya
di siku za usoni . Mimi nitakuwa nanyi bega kwa bega katika safari ya
kanisa hili huko mbele tuendako, kama nifanyavyo kwa makanisa na dini
nyingine kwa kuamini kuwa sote tunafanya kazi ya Mungu mmoja.
Naomba tuendelee kushirikiana kuleta maendeleo zaidi kwenye Dayosisi
yenu na nchi yetu kwa ujumla. Tukiunganisha nguvu zetu, daima ushindi
utapatikana. Basi tuamue sasa kuwa washindi.
Asanteni sana kwa kunisikiliza.
No comments:
Post a Comment