Wednesday, January 7, 2015

Gesi yaanza kutumika Tanzania

Mitambo ya gesi
Shirika la maendeleo ya Petrol nchini Tanzania limesema kuwa Mradi wa Gesi iliyogunduliwa kusini mwa nchi hiyo ,mkoani Mtwara umefikia asilimia 94 na tayari gesi hiyo imeanza kutumika katika baadhi ya maeneo.Hadi sasa kuna baadhi ya viwanda, na mashirika ambayo yameanza kutumia gesi hiyo asilia hatua inayodaiwa kupunguza gharama za upatikanaji wa Nishati kwa baadhi ya wakazi ambao wamekuwa wakitumia gharama kubwa ili kupata Nishati .Gesi yaweza kuwa ni mkombozi na rafiki kwa mwanamke kwa kumkomboa kutokana na matumizi ya mkaa na kuni kwa muda mrefu, hasa upande wa kuni, miaka kadhaa baadaye wanawake huwa na macho mekundu na hivyo kuhiziwa kuwa wachawi hasa kanda ya Ziwa Mkoani Mwanza Nchini Tanzania na kushuhudia mauaji ya vikongwe yasiyokwisha.Gesi ikiuzwa kwa gharama nafuu itamkomboa mwanamke na hatari ya kifo,kutokana na matumizi ya nishati ya jadi ,kuni yenye madhara maishani kutokana na dhana potufu ya ushirikina kwa mwanamke mwenye macho mekundu kudhaniwa ni mshirikiana.Nishati ya mkaa huharibu mazingira kutoakana na ukatwaji miti hovyo bila ya kupanda miti,lakini nishati hiyo imepanda bei hadi kufikia tshs elfu tisini kwa gunia lla lumbesa, na kuni nazo ni adimu mjini, lakini kijijini nafuu kiasi kama hakuna uharibifu mkubwa wa misitu.Suala la miradi mikubwa kama wa gesi hutawaliwa na rushwa na hivyo kuongeza bei ya nishati hiyo na kusababisha watu wa hali ya chini kutomudu kunufaika na nishati hiyo na kuonekana ni nishati ya baadhi ya watu .

No comments:

Post a Comment