Thursday, January 8, 2015

Kuna hii taarifa ya Askari aliyejiua ndani ya ghala la Silaha la Polisi, Mbeya

Police Line
Askari Polisi wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Mbozi, Patrick Kondwa amejiua kwa kujipiga risasi akiwa ndani ya ghala la kuhifadhia silaha katika kituo hicho.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo saa tisa usiku wa juzi kuamkia jana ambapo Askari huyo alikuwa lindo katika chumba hicho cha silaha.
Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini chanzo hasa cha tukio hilo.
Chanzo cha Habari: Gazeti la NIPASHE, January 08, 2014.

No comments:

Post a Comment